Afisi ya Habari
Amerika
H. 19 Muharram 1446 | Na: 01 / 1446 H |
M. Alhamisi, 25 Julai 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bunge la Congress la Marekani Lamkaribisha Muuaji wa Gaza - Haishangazi
(Imetafsiriwa)
Mara tu baada ya matukio ya Oktoba 7, Amerika ilikusanya meli zake za kijeshi ili kuhakikisha kwamba Umma hautaingilia kati kukomesha mauaji ya kutisha yanayofanywa huko Gaza. Amerika iliwaunga mkono zaidi wateja wake katika eneo hilo miongoni mwa watawala wa Waarabu na Waislamu katika kuyafunga majeshi ya Ummah, kuwazuia kuja kuwasaidia watu katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. Umwagaji damu huko Gaza umeendelea kwa muda wa miezi kumi, huku watawala wateja waliofedheheshwa na kudhalilishwa waliopandikizwa kwa Ummah wakiwazuia wale wenye nguvu kuwasaidia, hadi dola ya Kizayuni, kwa msaada wa Marekani, ilipowamaliza wanawake, watoto na wanaume wasiokuwa na silaha wa Gaza.
Baada ya kukamilisha misheni hii chafu - au karibu hivyo - Amerika ilimleta muuaji wa Gaza, muuaji wa watoto, ili kumtuza kwa vitendo vyake viovu, kumkaribisha kwa heshima ya mapokezi ya shujaa. Alihutubia Bunge lao la Congress kwa lugha yao bila kigugumizi, akionyesha kwamba wao ni gora moja, sawa na ilivyoelezwa na gazeti la ‘The New York Times’, lililosema: “Alionekana kama rais wa Marekani anayetoa hotuba ya Muungano wa Majimbo.” Liliongeza kuwa Netanyahu “pia alipata nafasi katika matamshi yake ya kusifu uhusiano imara kati ya Marekani na Israel,” ikibainisha kuwa wakati wa hotuba hii, alitaka kuonyesha vita kama mapigano kati ya wema na uovu, kati ya ustaarabu na ushenzi.
Hakika, vita ni baina ya kheri na shari, kheri iliyomo ndani ya Uislamu na Waislamu kama alivyoshuhudia Mola Mlezi wa walimwengu dhidi ya ghilba na uongo wa wauaji na waungaji mkono wao. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْراً لَهُمْ مِنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ]
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” [Quran 3:110]. Kama Ummah usingetiishwa na watawala wateja ambao ni vibaraka wa nchi za Magharibi, wakiongozwa na Marekani, ungewaonyesha wanadamu uadilifu na rehma ya kweli kwa kuzingatia mafundisho ya Mwenyezi Mungu ya Uislamu, hata kwa wauaji hawa, ambao Khilafah uliwakinga na mateso ya Makruseda wa Ulaya.
Hotuba ya kiburi ya muuaji wa Gaza katikati ya ulimwengu wa Magharibi, akijigamba kwa ushindi wake dhidi ya Waislamu—kutokana na kutokuwepo kwa Farooq wa Umma huu—inadhihirisha kwamba wafanyaji maamuzi nchini Marekani wamekamilisha mauaji huko Gaza kupitia kijeshi, kiuchumi, kisiasa na msaada wa vyombo vya habari. Dola haramu ya Kizayuni katika ardhi ya Waislamu ni chombo tu cha kuwakandamiza Waislamu kwa niaba ya mabwana wake katika dola ya Marekani na kwa hakika si chochote ila ni kambi ya kijeshi iliyo katikati ya ulimwengu wa Kiislamu, inayomshambulia yeyote anayepiga toka nje ya nyumba ya utumwa na ukoloni wake. Ni kama “paka anayejifurisha na kuonekana kama simba.”
Kwa upande mwingine, umma jumla wa Marekani bado haujui uungaji mkono kamili wa watawala wao kwa muuaji wa Gaza. Hii ni kwa sababu watawala wao, wakikiri kuwa mauaji ya watu wasio na hatia ni kitendo cha kuchukiza kinachochukiwa na roho za watu na kulaaniwa na watu wa kawaida, wanashikilia fimbo kutoka katikati. Wanapeleka zana zote za kuua kwa muuaji wao waliyemuajiri, wakati huo huo wakimlaumu ikiwa atashindwa katika misheni yake au wakati vitendo vyao vya kishenzi vinapofichuliwa. Zaidi ya hayo, umma kwa jumla hautambui kwamba Uislamu - ambao watawala wao wanauelezea kama “ugaidi” - ni dini ya Mungu na mfumo kamili wa maisha ambayo Mungu ameichagua kwa viumbe vyake.
Hivyo basi, ni lazima tuuwasilishe Uislamu katika nuru yake ya kweli katika nchi za Magharibi, kama hadhara badali ya hadhara ya kidhalimu iliyopandikizwa juu ya ulimwengu—si kupitia kujihusisha na mfumo dhalimu kwa kushiriki katika chaguzi zake. Kwa njia hii, tunatimiza amana ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametukabidhi, tukifikisha ujumbe jinsi Mwenyezi Mungu (swt) anavyopenda na anavyoridhia, na tuwe nguvu chanya katika jamii ya Marekani, tukiipendelea kheri yote – Uislamu kama mfumo kamili wa maisha na njia ya kuishi kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyokusudia kwa ajili yetu na wao – na kutopenda vitendo vya uhalifu wa watawala wake au kuunga mkono kwao kwa wahalifu kwa jina lake.
[ادْعُ إِلَى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ]
“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.” [Quran 16:125].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |