Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  25 Rabi' I 1446 Na: 04 / 1446 H
M.  Jumamosi, 28 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hawajaridhika na Uharibifu wa Gaza, Wazayuni Sasa Wanaendeleza Uhalifu Wao hadi Lebanon

(Imetafsiriwa)

Baada ya mwaka mmoja wa kampeni ya wazi ya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina, iliyofanywa mchana kweupe kwa ushirikiano wa dola za kimataifa na watawala wa Waislamu wanaowazunguka, Wazayuni hivi sasa wameendeleza jinai zao hadi Lebanon kwa kulipua mabomu kiholela katika makaazi yenye wakaazi wengi, na kuua maelfu ya watu tayari, kwa matumaini wanaweza kurekebisha sura yao iliyoshindwa baada ya kampeni yake angamivu mjini Gaza.

Wakishajiishwa na kifiniko cha kisiasa na kijeshi cha dola za Magharibi, ikiwemo Australia, na uungaji mkono wa khiyana wa kuokoa maisha wanaopata kutoka kwa watawala wa Waislamu wanaowazunguka, Wazayuni hivi sasa wanataka kubadilisha kampeni yao angamivu huko Gaza kuwa ushindi wa kivita kama vile vita vya 1967 na 1973, ambapo nguvu ya mvamizi hutiwa chuku na kutochukua hatua kwa makusudi kwa watawala wa Waislamu.

Wazayuni wamesubutu tu kufungua eneo jipya wakijua kuwa watawala wa Waislamu ndio walinzi wake wa kwanza na wa mwisho, ambao huzuia majeshi yao, huwafunga pingu watu wake, huimarisha mipaka yake, na huogopa kukabiliana na uvamizi bila kutoa chochote isipokuwa maneno matupu. Watawala wa Waislamu hawashiriki tu katika jinai za Wazayuni dhidi ya watu, bali ni wawezeshaji wake.

Magharibi, ikiwemo Australia, imetoa kila kifiniko cha kisiasa, kijeshi na kiuchumi kwa uhalifu wa Wazayuni dhidi ya watu wetu. Kama vile ilivyowezesha uhalifu wa kuasisi umbile haramu la Kiyahudi hapo awali, nchi za Magharibi zina furaha sana kuwezesha kuendelea kwa uhalifu wake leo. Hakujawa na umuhimu wowote wa kuzingatia maadili, sheria au ubinadamu. Uvamizi huu ulijengwa juu ya mafuvu ya wenyeji wake, na uendelevu wake unapanuliwa juu ya mafuvu ya watu wa leo. Ombi kwa taasisi za kimataifa, na ombi kwa sheria ya kimataifa, sio mzaha tu, bali ni uhalifu.

Ngurumo za simba wa uwongo zimewekwa wazi ili watu wote waone. Majigambo yote ya watawala wa Waislamu, bila kuwabagua, yamethibitishwa kuwa si chochote ila ni uongo. Wote wamewatelekeza Waislamu wa Palestina, na sasa Waislamu wa Lebanon, na kabla ya hapo Waislamu wa Iraq, Afghanistan na Yemen, na hakika kila mahali Waislamu wanakandamizwa. Hata vibaraka wa tawala za Kiislamu, ambao kwa miongo kadhaa wametumikia mabwana zao kwa uhalifu, sasa wanatupwa kwenye jukwaa la manufaa ya kisiasa.

Iwapo mataifa ya Magharibi yanatumai sasa ni wakati mwafaka wa kuunda upya eneo la Mashariki ya Kati, ambapo uhalalishaji mahusiano na umbile linalokalia kimabavu uko katikati yake, basi historia iwe ukumbusho wa kujitolea kusikoyumba kwa Waislamu ya kujikwamua na uvamizi wote. Wakati watawala wa Waislamu daima wamekuwa imara katika mfukoni mwa mabwana zao wa Magharibi, pengo kati ya Waislamu na watawala wao halijawahi kuwa pana zaidi kuliko sasa.

Mazingira ya kisiasa yamebadilika sana katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita hivi kwamba nafasi ya watawala hawa haijawahi kuwa dhaifu, dhamira ya Waislamu haijawahi kuwa na nguvu zaidi, na minong'ono kutoka kwa umma kwa jumla imefikia majeshi ya kitaalamu kwa sauti kubwa sana. Ni suala la muda tu kabla ya wana wa Ummah wanyoofu kujinasua kutoka kwa minyororo waliofungwa kwao, kuregesha utashi wao wa kujitegemea wa kisiasa, na umbile hilo haramu litalazimika kukabiliana na jeshi ambalo kwa hakika limejitolea kuwalinda wasio na ulinzi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu