Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  2 Rabi' II 1446 Na: 05 / 1446 H
M.  Jumamosi, 05 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vilio vya Kuficha Mauaji ya Halaiki

(Imetafsiriwa)

Wanaotetea mauaji ya halaiki na wawezeshaji wao wasio na haya katika vyombo vya habari na siasa wamezusha raundi nyingine ya msukosuko wa kimakusudi unaozunguka mkutano uliopendekezwa huko Lakemba, ukiangazia kampeni ya mwaka mzima ya mauaji ya halaiki nchini Palestina.

Hizb ut Tahrir/Australia ingependa kueleza hadharani kwamba dhana na uongo unaoenezwa na wafuasi wa Kizayuni kuhusiana na waandaaji wa mkutano huo, bora zaidi, wamepewa taarifa potofu na baya zaidi , ni kwa nia mbaya. Inashangaza kwamba wanasiasa daima wanatoa wito wa kuwepo kwa uwiano wa kijamii lakini hawana kusita katika kukubali simulizi za uongo - kueneza habari potofu katika mchakato huo na hatimaye kuhujumu “mshikamano wa kijamii” wanaoupigia debe.

Ulimwengu unatazamiwa kuamini kwamba hatari kubwa zaidi hailetwi na wale wanaotekeleza mauaji ya halaiki, bali wale wanaoyavutia. Tunaulizwa kuamini kuwa ni kutojali kukusanyika siku fulani, lakini sio kupiga mabomu, kuua siku hiyo hiyo.

Kampeni hii ya hivi punde ya propaganda inazidi kuchochea moto wa chuki dhidi ya Uislamu—sio kuridhika na kuwadhalilisha Wapalestina wote, lakini pia kuwalenga wale wanaokusanyika kutafakari maumivu yao wakati wa mauaji ya halaiki.

Je, ni kwa jinsi gani madai na maonyo kuhusu kusambaratisha mshikamano wa kijamii yanaweza kuchukuliwa kwa uzito kutoka kwa wale wanaohalalisha, kwa kila njia, kuichana miili ya wanadamu?

Madai haya hayana msingi, yamepotoka, ya uongo. Lakini ulimwengu tayari unajua hilo.

Ni wakati sasa wa serikali ya Australia kukiri hilo pia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu