Jumatatu, 21 Dhu al-Qi'dah 1446 | 2025/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  15 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: H 1446 / 43
M.  Jumanne, 13 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwisho wa Enzi ya Awami League, Chama Kinara cha Siasa za Kisekula - ni Onyo la Kihistoria kwa Vyama Vilivyopo vya Kisiasa na Nyuso Mpya za Kisiasa

(Imetafsiriwa)

Kwa kuanguka kwa dhalimu Hasina na tangazo rasmi la kupigwa marufuku kwa shughuli zote za chama kiovu cha Awami League, enzi ya giza ya siasa za chama kikuu cha kisekula -Awami League imekamilika. Kuangamia huku kwa Awami League, mrithi wa 'All India Muslim League' iliyoanzishwa mwaka wa 1906, hakutokani na mlingano wa kisiasa wa mamlaka ya kundi lolote la kisiasa, bali ni ukweli wa kihistoria na usioepukika. Hamu ya Waislamu wa India ni kuishi chini ya utawala wa Kiislamu-Khilafah. Ili kuihadaa hamu hii, kwa jina la kulinda maslahi ya Waislamu, 'All India Muslim League' iliendeshwa chini ya uongozi wa Mohammad Ali Jinnah, kibaraka wa Waingereza Wakoloni. Kwa kauli mbiu ya ‘Yapi makusudio ya Pakistan, La ilaha illallah’, kibaraka huyu wa Uingereza Jinnah aliwagawanya Waislamu wa eneo hili na kuanzisha Pakistan mwaka 1947 kwa msingi wa utaifa wa Kiislamu na kuanzisha mfumo wa kisekula wa ubepari kwa Waislamu, na kuwageuza kuwa koloni mamboleo ya Uingereza. Baadaye, kibaraka mwengine wa Uingereza Sheikh Mujibur Rahman alianzisha ‘Awami League’ kwa msingi wa utaifa wa Kibengali na akajishughulisha tena na siasa za njama za kuwagawanya Waislamu kwa uungwaji mkono wa India.

Kwa kuwa ‘Awami League’ haikuficha kitambulisho chake cha kisekula, Awami League ilishindwa kupata imani na uungwaji mkono wa watu wanaopenda Uislamu wa nchi hii. Matokeo yake, Hasina na Awami League walikataliwa na watu wapenda Uislamu wa nchi hii na kuchukua msimamo wa wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ili kukwamia madarakani, uongozi wa Awami ulijiimarisha kama 'mkruseda wa kidemokrasia' katika 'vita dhidi ya Uislamu' kwa jina la 'vita dhidi ya ugaidi' ili kupata uungwaji mkono wa nchi za Magharibi, hasa Wamarekani, na kuendelea na majaribio yake yote maovu ya kudhoofisha jeshi la nchi hiyo ili kuitiisha ardhi hii chini ya India, mshirika wa kikanda wa Marekani. Kuanzia kwenye mauaji ya Pilkhana, ukandamizaji na mateso yanayoendelea ya wanasiasa wakweli na wenye ikhlasi na wale wanaobeba ujumbe wa Uislamu, ni mifano ya hao. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ * فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ * فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ]

Ambao walifanya jeuri katika nchi. Wakakithirisha humo ufisadi. Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. [Surah al-Fajr: 11-13]. Kwa njia hii, mtawala huyo dhalimu alianguka duniani kote na adhabu ya Mwenyezi Mungu iliwasibu wafuasi wake vipofu. Uhalisia huu usioepukika ni onyo la kihistoria kwa vyama vya kisiasa vilivyopo na nyuso mpya za kisiasa nchini. Yeyote katika ardhi hii iliyo na wakaazi wengi Waislamu ambaye atajiunga katika vita vya Wamagharibi dhidi ya Uislamu na kujaribu kulazimisha maslahi ya kikoloni ya mabwana zao wa kigeni kwa watu, atatupwa kwenye takataka za historia na watu kama Awami League iliyoanguka.

Swali la serikali ya mpito lililo akilini mwa watu ni, pindi serikali dhalimu ya Hasina ilipokipiga marufuku chama cha kisiasa chenye ikhlasi cha Hizb ut Tahrir kwa kuchukua msimamo mkali kwa ajili ya Uislamu, Waislamu na ubwana wa nchi na kwa kutolegeza msimamo, na kufanya dhulma na mateso ya kikatili kwa wanaharakati wake, basi kwa nini marufuku haramu kwa Hizb ut Tahrir bado haijaondolewa baada ya kuondoka kwa dhalimu huyo? Swali kwa viongozi wa vuguvugu la kupinga ubaguzi ni, mnapiga kelele kuhusu kupigwa marufuku kwa Awami League, lakini kwa nini mnanyamaza kimya kuhusu marufuku ya kidhalimu ya serikali ya Awami dhidi ya Hizb ut Tahrir? Vivyo hivyo kauli mbiu zenu "Aposh na Sangram - Sangram, Sangram (Legeza msimamo au Pambana - Pambana, Pambana)" "Dalali na Rajpath - Rajpath, Rajpath (Siasa za Njama au Kulaani - Kulaani, Kulaani)" ni za kweli, au maneno matupu? Lazima mujue kwamba Hizb ut Tahrir ni chama kikuu cha kisiasa kinachojumuisha vijana kutoka taasisi maarufu za elimu za nchi, hivyo lazima muelewe mapigo ya vijana. Mkichagua njia ya ‘kulegeza msimamo na utiifu’ (Vijana wa Kituruki), kizazi cha vijana kitakukataeni kwa chuki. Wakati kizazi cha vijana kinabeba "bendera ya Shahada", ikiwa mutachukua nafasi ya uongozi wa kisekula wa 'Awami League' iliyoanguka, basi mnaweza kutambua ni matokeo gani yanayokusubirini?

[وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ]

Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. [Surah Adh-Dhariyat: 55]

Enyi Viongozi Wanyoofu wa Kisiasa, Wasomi na Maafisa wanaohudumu katika Jeshi, ‘Supu ikiwa na chumvi, kubadilisha kijiko haitasaidia’ – methali hii ya Kiarabu ina maana kwamba masuluhisho ya juu juu au ya muda bila kujua chanzo cha tatizo hayafai na hayana maana yoyote. Ubepari wa kisekula ni mfumo uliofeli ulimwenguni kote, ambao sasa unatiliwa shaka mahali ulipozaliwa, ulimwengu wa Magharibi wenyewe. Kwa hiyo, kwa kubadilisha tu nyuso hakujakuweko na mabadiliko katika mfumo huu kwa miongo kadhaa iliyopita, vile vile hakutakuwa na mabadiliko ya kweli katika siku zijazo pia. Mtume (saw) amesema, «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»“...kisha kutakuwa na mwisho wa udhalimu, kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume” (Hadith: Musnad Ahmad). Lazima mjue kwamba watu wapenda Uislamu wa ngazi zote za nchi wanasubiri kuanzishwa kwa Khilafah kwa ajili ya ukombozi wa Umma wa Kiislamu. Kwa hiyo, tunakulinganieni: badala ya kuingia katika mtego wa siasa za mifarakano na kutimiza matarajio ya watu, shirikianeni na Hizb ut Tahrir na mujitokeze kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu