Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 26 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: H 1446 / 46 |
M. Jumamosi, 24 Mei 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Muda Inatengwa na Wananchi kwa sababu ya Utiifu wao kwa Amerika; kwa upande mwingine, Msimamo wa Jeshi letu katika Kupendelea Ubwana wa Nchi kwenye Masuala ya 'Mkondo' na 'Bandari' ni Dhihirisho la Matarajio ya Watu
(Imetafsiriwa)
Huku serikali ya mpito, ikiwapuuza Waislamu wa Rohingya na ubwana wa nchi hiyo, inatamani sana kupeana 'mkondo' kwa maslahi ya kisiasa ya kijiografia ya Amerika na kukabidhi shughuli za 'New Mooring Container Terminal' kwa kampuni yenye ushawishi wa Marekani "DP World", msimamo mkali wa jeshi letu kuunga mkono ubwana wa nchi umesifiwa na watu wengi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
«كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Kila mmoja wenu ni mchungaji. Na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya walio chini yake. Kwa mfano Imam (mtawala) wa watu mchungaji wao, na yeye ataulizwa juu yao” (Sahih al-Bukhari).
Ni wazi kutokana na Hadith hii kwamba jukumu alilokabidhiwa kila mtu mwenye cheo ni amana na ni wajibu (fardh) kwake kuilinda amana hii. Kwa upande mwingine, kutoilinda amana hii ni khiyana kwa watu, ambayo itamlazimu kuwajibika hapa duniani na adhabu kali inamngoja kesho Akhera. Kwa kupuuza kulaani na hasira za wananchi, ahadi ya serikali ya mpito ya kutekeleza miradi hiyo ya kikoloni ya Marekani, imezua shaka miongoni mwa wananchi kuhusu shughuli zao na wanatambuliwa na wananchi kuwa ni watiifu kwa Wamarekani. Matokeo yake, serikali ya mpito inatengwa na wananchi na inakabiliwa na mgogoro uliopo. Serikali iliyoanguka ya Hasina, tiifu kwa Uingereza, iliruhusu meli za kivita za junta ya Myanmar inayoungwa mkono na Uingereza kuendesha operesheni katika maeneo ya bahari ya St. Martin na Teknaf ili kuwezesha mapambano dhidi ya Jeshi la Arakan. Jeshi la Mabudha linaloungwa mkono na Marekani pia linahusika na uhamisho, mateso na mauaji ya halaiki ya Waislamu wa Rohingya, kama serikali ya kivita ya Myanmar ilivyofanya. Kwa hivyo, msaada wa serikali ya mpito kwa Jeshi la Arakan ni usaliti kwa Waislamu wa Rohingya, na mfano usio na aibu wa utiifu kwa Marekani ambao wanahusika katika mauaji ya halaiki ya Waislamu duniani kote, ikiwemo Palestina-Iraq-Afghanistan-Syria-Yemen.
Kwa upande mwingine, barakoa za makundi ya kisiasa na wasomi yanayoiunga mkono Marekani pia zimepomoka nyusoni mwa watu. Wanaunga mkono kwa upofu mradi wa ukoloni wa Marekani na wanajaribu kuligawanya jeshi letu kwa maslahi ya Marekani, kama vile Hasina alivyojaribu kudhoofisha jeshi letu kwa kutekeleza njama ya Pilkhana kwa maslahi ya India. Kwa hakika, kulinda maslahi ya wananchi inapaswa kuwa moja ya misingi ya siasa, ambayo kwayo wananchi watakuwa wamoja. Hata hivyo, makundi haya ya kisiasa ya kipumbavu yanatii kwa upofu Magharibi ili kubaki madarakani au kuingia madarakani, na kutengwa na watu. Na wanapotengwa na watu, nchi za Magharibi huwatupa kama karatasi na kujaribu kuwabadilisha na vibaraka wengine, ambapo tayari tumeshuhudia mifano mingi.
Enyi Maafisa Wanyoofu katika Jeshi! Hakuna mtu, aliyechaguliwa au ambaye hajachaguliwa, ana haki ya kuchukua maamuzi dhidi ya ubwana wa nchi hii. Ni ukweli uliothibitishwa kwamba hakuna tabaka tawala linaloitii Magharibi huwawakilisha watu wa nchi hii milele. Lazima muwe mumetambua kwamba kwa sababu ya msimamo wenu sahihi kwa niaba ya watu, mumepata sifa kutoka kwa watu, na utiifu wenu kwa Mwenyezi Mungu (swt) umeonekana, jambo ambalo limekutukuzeni.
Mtume wetu kipenzi Muhammad (saw) amesema,
«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifah) ni ngao ambayo nyuma yake mnapigana na kujikinga nayo” [Sahih Muslim]. Hivyo basi, ni lazima mrudishe uongozi wa kweli wa Umma wa Kiislamu, Khilafah, kwa njia ya Utume, ambao chini yake mtaweza kutekeleza ipasavyo wajibu wenu katika kuulinda Uislamu, maslahi ya watu, na ubwana wa nchi. Kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu wa Rohingya, eneo la Waislamu linalokaliwa kwa mabavu la Arakan linaweza kukombolewa na kuregeshwa chini ya Khilafah. Kwa hiyo, sisi katika Hizb ut Tahrir tunakuombeni kwa ikhlasi kutoa nusrah (kukabidhi mamlaka) kwa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha uongozi wa kweli wa Khilafah kwa njia ya Utume.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfal: 24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |