Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
| H. 24 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 18 |
| M. Jumatatu, 15 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Bangladesh Lazima Likatae Kuwa Rafiki wa Wakoloni kwa Jina la kile kinachoitwa Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa na Kurudisha Hatima Yake kama Walinzi wa Ummah
(Imetafsiriwa)
Jeshi la Bangladesh linathibitisha shambulizi baya la droni kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Abyei nchini Sudan mnamo 13 Disemba 2025. Shambulizi hili liliwaua walinda amani sita wa Bangladesh na kuwajeruhi wengine wanane. Wakati huu wa kuhuzunisha moyo hauhitaji maombolezo tu, bali pia tathmini mpya muhimu ya misheni ambayo kwayo walitoa maisha yao.
Mzozo waliotumwa kuusimamia si mgogoro tu wa kindani. Ni matokeo ya moja kwa moja na yaliyokusudiwa ya ‘mpango wa karne wa kikoloni wa Kimagharibi’ wa kugawanya, kudhoofisha, na kupora ulimwengu wa Kiislamu. Mipaka nchini Sudan - kama ile ya Afrika na Mashariki ya Kati - ilichorwa jijini London na Brussels ili kumnasa ndugu dhidi ya ndugu, na kuchochea ushindani usokwisha juu ya ardhi na rasilimali kama vile mafuta yaliyo chini ya eneo la Abyei.
Leo, mradi huu wa kikoloni unaendelea chini ya jina jipya: “Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa.” Misheni kama UNISFA si juhudi za kibinadamu zisizoegemea upande wowote. Ni walinzi wenye silaha wa mfumo wa kilimwengu wa ukandamizaji wa Magharibi uliofeli. Kusudi lao si kutatua migogoro kwa haki, bali ni ‘kuisimamia na kuifunga”, kuhakikisha dola za Magharibi, hasa Marekani, zinadhibiti ardhi za kimkakati, rasilimali, na matokeo ya kisiasa. Wanahalalisha mipaka ile ile iliyosababisha vurugu na kulinda serikali fisadi, za kisekula, zilizowekwa na Magharibi nchini Sudan zinazotawala bila ya Uislamu. Ajenda ya Marekani iko wazi kabisa. Ilitumia John Garang na miongo kadhaa ya uasi kuichana Sudan Kusini kutoka kwa mwili wa Ummah wa Kiislamu. Sasa inatumia wawakilishi kama vile Vikosi vya Msaada wa Haraka ili kuigawanya Darfur, ikitaka kuigawanya ardhi ya kimkakati ya Waislamu kuwa dol dhaifu, zinazoweza kudhibitiwa.
Lazima tujiulize: Jeshi la Waislamu la Bangladesh linawezaje kuwa chombo katika njama hii ya ukoloni mamboleo? Majeshi ya Waislamu yanaundwa ili kuwa watetezi wa Uislamu, sio mamluki kwa maslahi ya Makafiri wa vita. Kushiriki katika misheni hizi kunatufanya kuwa washirika katika mfumo unaopora utajiri wa Waislamu na kugawanya Ummah wetu. Pia, unafiki wa serikali yetu uko dhahiri. Haiwezi kulinda mipaka yetu au uhuru wetu kutokana na uvamizi wa adui India, lakini inawatuma maafisa wetu wa kijeshi kwa urahisi kusherehekea gwaride la mshindi nchini India, kama ilivyoripotiwa na The Business Standard mnamo 8 Disemba 2025, huku ikiwapa wanajeshi wetu jukumu la kufa wakilinda mipaka ya wakoloni nchini Sudan.
Mipango ya adui haitasimama. Usalama wa kweli kwa Ummah utakuja tu kwa kushughulikia chanzo kikuu: kukosekana kwa uongozi wa Kiislamu ulioungana chini ya Sharia ambao utavunja mfumo wa dola ya kitaifa wa Magharibi. Suluhisho la msingi ni kusimamishwa tena kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo pekee inaweza kulinda ardhi za Waislamu, kubatilisha mipaka ya wakoloni, na kusimamia haki. Hebu damu ya mashahidi wetu na ituamshe. Hebu na ikomeshe dori yetu katika mfumo wa kilimwengu uliofilisika na kuchochea kurudi kwetu kwenye wajibu wa kuunganisha na kutetea Ummah wa Kiislamu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |



