Jumamosi, 30 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  28 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 16
M.  Jumatano, 19 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hukumu ya Kifo kwa Hasina:
Udhalimu wa Kisekula Uliomuunda Hasina Ungalipo

(Imetafsiriwa)

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa hukumu ya kifo ya kihistoria dhidi ya mtawala wa Bangladesh aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina. Kwa watu waliokandamizwa wa Bangladesh, uamuzi huu unatoa uthibitisho wa kiishara uliochelewa kwa muda mrefu na unasimama kama shtaka lenye nguvu kwa utawala uliokanyaga ubinadamu wa kimsingi. Lakini uamuzi huu unahitaji tafakari ya kina, sio sherehe tu. Haki ya kweli inahitaji mabadiliko ya kimfumo, sio adhabu ya mtawala dhalimu tu. Chanzo kikuu ni mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, ambao unahubiri demokrasia huku ukitekeleza ‘mantiki ya siasa za kijiografia’. Dola za Kimagharibi huweka kipaumbele mara kwa mara ‘utulivu’ na maslahi ya siasa za kijiografia na kiuchumi kuliko haki za binadamu, na kuhalalisha ukandamizaji wa kimabavu katika mataifa kama Bangladesh, Pakistan, na Misri kwa jina la maendeleo. Dikteta anayeunga mkono Magharibi daima hupendelewa kuliko demokrasia isiyotabirika. Hii inaonyesha unafiki wa msingi wa mfumo wa kidemokrasia wa kisekula: “demokrasia ya maneno, lakini udikteta wa vitendo.” Muungano wao pamoja na madikteta sio kufeli kwa mfumo - ni mfumo wenyewe.

Hukumu dhidi ya Sheikh Hasina, ingawa ni muhimu, sio pekee inayohakikisha ukombozi wa kweli. Kwa hivyo, mapambano yetu lazima yabadilike: kutoka kuwaondoa madikteta binafsi hadi kubomoa usanifu wa kinafiki wa siasa za kijiografia unaowazalisha. Mzunguko huu wa kuunda na kisha kuwaondoa madikteta ni matokeo ya moja kwa moja ya ombwe la madaraka lililoachwa kwa kuanguka kwa Khilafah ya Uthmani mnamo 1924, ambalo lilijazwa na mfumo uliobuniwa na Magharibi unaoweka kipaumbele udhibiti juu ya haki na dhamiri halisi.

Tangu kuvunjwa kwa Khilafah, Magharibi adui ilibuni simulizi ili kukashifu kurudi kwake (Khilafah) kwa kuielezea kwa uongo kama mnara mkuu wa ukandamizaji wa miaka 1400. Simulizi hii ya Maorientalisti inaangazia kwa ubaguzi watu fulani kama Hajjaj ibn Yusuf au masultani wachache wa Mamluk, huku ikipuuza mifumo imara ya kisheria na kimaadili iliyozuia utawala wa kidikteta. Khilafah ya Uthmani iliendeshwa kwa kanuni ya “Mzunguko wa Haki” (Daire-i Adliye), ikiunganisha waziwazi nguvu ya dola na ustawi wa umma. Sultan Suleiman alipata lakabu yake ya “Al Qanuni (Mpeanaji Sheria)” kupitia upangiliaji wa vifungu vya sheria, sio utawala wa kiholela. Zaidi ya hayo, baada ya kufunguliwa Konstantinopoli na Sultan Mehmed II (“Mfunguzi”), Mfumo wa Uthmani wa Millet wa katikati ya karne ya 15 ulizipa dini za walio wachache uhuru mkubwa wa kujiendesha wenyewe, huku wasomi huru (ulama) na Sharia zikitumika kama udhibiti wa kudumu wa mamlaka ya Khalifa. Kanuni ya uwajibikaji inaonyeshwa waziwazi na Sheria za Mahakama za za kesi za Udhalimu za Kihistoria (Mahkamat al-Madhalim), ambazo ziliwaruhusu raia kutafuta fidia ya kisheria dhidi ya maafisa wenye nguvu wa serikali. Ingawa Khilafah Rashida ndio muundo wetu, Khilafah za baadaye hazikuwa udhalimu mithili ya tawala za kidhalimu za utamaduni wa Magharibi. Zilikuwa mifumo imara yenye vyombo vya asili vya haki kwa dini na rangi zote.

Enyi watu, lazima muelekeze wakati huu zaidi ya kuanguka kwa dhalimu mmoja na kuelekea ukombozi kutoka kwa mfumo unaowazalisha. Mabadiliko ya kweli na ya kudumu hayako katika kubadilisha nyuso bali katika kutabikisha utawala wa kiwahyi chini ya utawala wa Khilafah. Mfumo huu, uliobuniwa na Azza wa Jal Mwenye Kujua Yote, umeandaliwa kipekee kuondoa utawala wa kidikteta katika mzizi wake, ukiweka vidhibiti visivyobadilika juu ya madaraka na kuweka kipaumbele cha haki kwa wote. Mapambano sasa ni kwa ajili ya mabadiliko haya makubwa — kubadilisha miundo yenye dosari, kandamizi ya mwanadamu kwa mfumo adilifu na mtakatifu wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Azza wa Jal asema katika Quran:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfal:24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu