Majanga na Maafa ni Matokeo ya Kimaumbile ya Kukosekana Dola yenye Kujali
- Imepeperushwa katika Iraq
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika msururu wa ajali za mara kwa mara na moto wa kutisha-hasa ule moto wa ukumbi wa harusi wa mwaka 2023 huko Ninawi, ambao uligharimu maisha ya zaidi ya watu 120 na kujeruhi 200; moto wa mwaka 2021 katika Hospitali ya Al-Hussein huko Dhi Qar, ambao uliua zaidi ya watu 92; na moto wa mwaka 2021 wa kituo cha utengaji wagonjwa wa COVID-19 katika Hospitali ya Ibn Al-Khatib jijini Baghdad, ambao ulisababisha vifo vya watu 82-unakuja msiba mwengine tena wa kutisha. Moto mkubwa ulizuka katika soko kuu la Kut jioni ya Jumatano, 16 Julai 2025. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ilithibitisha kuwa moto huo, ambao ulizuka ndani ya jengo la biashara la ghorofa tano katikati mwa mji wa Kut, uliwaua watu 61, ikiwa ni pamoja na miili 14 iliyoungua ambayo bado haijatambuliwa. Waathiriwa wengi walikufa kutokana na kuvuta moshi. Wizara hiyo iliongeza kuwa jengo hilo ambalo lilikuwa na mkahawa na kituo cha biashara, lilikuwa limefunguliwa kwa siku saba pekee.