Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  4 Sha'aban 1444 Na: H.T.L 1444 / 07
M.  Ijumaa, 24 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utekaji Nyara wa Sheikh Ahmed Shuaib Al-Rifai
(Imetafsiriwa)

Siku tano zimepita na mpaka sasa mtekaji nyara hajajulikana! Pamoja na vyombo vyote vya usalama vinavyodai kuwa na uwezo unaowawezesha kutokomeza tukio hilo kabla halijatokea! Jana, baadhi ya watu walio na nia na wafuasi wa kesi hiyo walisema kuwa chombo cha usalama kilimkamata, na ni Chombo Kikuu Usalama tu ndicho kilichokanusha tuhma hiyo kwa niaba yake chenyewe, na kuwatishia wale wanaokituhumu kuwafungulia mashtaka.

Kuhusiana na suala hili, tunasema yafuatayo:

- Inajulikana kuwa vyombo vya juu zaidi vya usalama na afisa wa juu kabisa, hawezi kuchukua hatua isipokuwa iwe na kifiniko cha kisiasa kinachowezesha kufanya hivyo, au wakati wanasiasa wanapotaka kufanya mambo kwa nia za kisiasa, na kwa hivyo washukiwa wa kwanza ni wanasiasa wanaosimama nyuma vyombo hivyo na kuvifadhili na kuvihifadhi na idara na maafisa wake kutokana na kuhesabiwa. Kutokana na hayo, lazima ifichuliwe ni nani anayefanya maamuzi katika kiwango hiki na huduma za usalama zinazotekeleza maamuzi haya.

- Ikiwa mtekaji nyara alikuwa genge, chama, au ubalozi, basi msiba ni mkubwa, kwa kuwa wanafanya ufisadi bila kuzuiwa au kusita.

- Inafahamika kwamba jukumu la kimaadili kwa kila uhalifu ni la vyombo vinavyosimamia usalama wa watu, na nyuma yao kuna mawaziri wenye jukumu la kufuatilia vyombo hivi; Kwa hiyo, mawaziri hawa lazima watoke nje mara moja kueleza dhurufu zote.

- Haikubaliki kwa vyombo vya dola kuamiliana na watu kwa njia ya vitisho, na kuwashtaki wale wanaolia kutokana na maumivu yao. Bali ni wajibu wao kueleza undani wa kazi yao, ili watu wapate kufarijiwa na nafsi zao zitulie.

- Inajulikana vyema kuwa munaichukulia Tripoli kuwa ni eneo la usalama, ambalo mipango ya usalama inaandaliwa, na watu wanakamatwa huko, haswa Waislamu, na sehemu zingine, kwa sababu ya tuhuma tu, na wanafungwa bila mashtaka, na suala la wafungwa wa Kiislamu bado ni ushahidi hai, huku mukiwaachilia kutoka magerezani wale wanaotoka nje ya nchi huku mukitazama nchi anayobeba utaifa wake, haya yote, na uhalifu wa wazi kama huu tuliomo ndani na karibu yake, na bado mungali kimya! Hivi ni mwanasiasa, au wanasiasa, au chama cha kisiasa kipi kinachofinika suala hili, ni nani?!

- Ikiwa vyombo vyote hivi vitashindwa kutekeleza wajibu wao, basi ni lazima kuzingatia jukumu la wanaoviongoza na kustahiki kwao wajibu huu mkubwa, wao na wanasiasa walio nyuma yao.

- Haikubaliki kwa upande wowote kufanya utekaji nyara, wala utekaji nyara kufanywa dhidi ya upande wowote, bila kujali dini au dhehebu.

- Haikubaliki kuligeuza suala hili kuwa ni suala la kimadhehebu na uchochezi wa kimadhehebu, au kuingizwa nyuma ya wale wanaotaka kuifanya Tripoli kuwa sehemu isiyo salama, ambayo watu wanajilinda, hivyo machafuko kutawala, na kuwa mlango wa kuingia mikono ya vyumba nyeusi na kile kinachojulikana kama mipango ya usalama.

Enyi Waislamu wa Lebanon: Nyinyi ndio watu wa nchi hii, na wengine waliishi pamoja nanyi kwa mamia ya miaka, na mlikuwa katika kiwango cha Shariah ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo kwayo mliyotawala, lakini leo mataifa yamepigana dhidi yenu, na bila ya hukmu ya Mwenyezi Mungu mumekuwa povu kama povu la mto!

Suala hili leo si chochote ila ni uthibitisho wa kile ambacho ni hakika, ambacho ni kufeli kwa serikali ya Lebanon kama ilivyo.

Wajibu wenu kuhusiana na suala hili na kuhusiana na kesi zote za dhulma zinazokusibuni ni kuwakana wale wanasiasa wanaodai kuwawakilisha, baada ya kushindwa kufikia mahitaji ya chini kabisa ya ulinzi na usalama, na kutoingizwa kuwa watetezi wa uchochezi na fitna, ambapo mutakuwa ndio kichocheo, na wale wachochezi watabaki kwenye makasri yao, watoto wao na fedha zao, wakisubiri uwekezaji unaokusibuni.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu