Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  11 Ramadan 1444 Na: 1444 / 16
M.  Jumapili, 02 Aprili 2023

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza
(Imetafsiriwa)

مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ

وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً﴿

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]

Kwa kuamini Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu na watu wa Jordan kwa jumla na kwa mashababu wa Hizb ut Tahrir hasa, mmoja wa mashababu wake waaminifu, wenye subira na matumaini, ndugu mwanachuoni mkubwa:

Dkt. Abdul Halim Muhammad Al-Ramahi (Abu Imad)

ambaye alikwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu (swt) alfajiri ya siku hii ya Jumapili tarehe 11 ya Ramadhan 1444 H, sawia na tarehe 2 Aprili 2023 M, akiwa na umri wa miaka 84, alioutumia kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na akifanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, hakukatishwa tamaa na hilo kutokana na yale aliyokumbana nao ya dhulma na matusi kutoka kwa madhalimu, wala yale aliyoyapata kutokana na maradhi ya muda mrefu, na alikabiliana na hayo yote huku akimuamini Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi, na akiwa na yakini ya ushindi wake, mwenye subira, mkakamavu na mwenye kutaraji malipo mema, bila ya kumlainishia njia au kudhoofisha azma yake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ammiminie rehma pana ndugu yetu Abu Imad na ajaalie makaazi yake kuwa Pepo ya juu kabisa pamoja na Mitume, wakweli, mashahidi, wema na hao ndio marafiki wema kama tunavyomuomba Yeye (swt) kwetu sisi na jamaa zake subira, faraja, na rambirambi njema, na hatusemi ila yale tu aliyotuamrisha Mwenyezi Mungu (swt):

 [الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. [Surah Al-Baqarah 2:156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Jordan

- Kalima ya Ustadh Muhammad al-Fuqaha wakati wa mazishi ya Sheikh Dkt. Abdul Halim Muhammad al-Ramahi (Abu Imad), Mwenyezi Mungu amrehemu -

- Kalima ya Ustadh Marwan Obeid katika kikao cha tanzia ya Dkt. Abdul Halim Muhammad al-Ramahi (Abu Imad), Mwenyezi Mungu amrehemu -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu