Jumatano, 05 Safar 1447 | 2025/07/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  28 Muharram 1447 Na: 1447 / 03
M.  Jumatano, 23 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vyombo vya Ukandamizaji vya Serikali ya Jordan Vyamkamata Sheikh Saeed Radwan kutoka Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo watu wa Jordan kutoka kaskazini hadi kusini na kutoka matabaka yote ya maisha wanaongeza hasira na uungaji mkono kwa Gaza, ambayo inaangamizwa, watu wake wanakabiliwa na njaa ya kikatili inayolazimishwa na umbile halifu la Kiyahudi kwa njama za fedheha kutoka kwa serikali ya Jordan, na huku vyombo vya ukandamizaji vya serikali hii vikisimama kupinga uasi huu kupitia ukandamizaji na ukamataji wa wana na watu waheshimiwa wa Umma huu...

Majeshi haya ya kikandamizaji yamemkamata mbebaji Da’wah, Sheikh Saeed Radwan (Abu Imad), mtu mwenye fikra na siasa kutoka miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir, kutoka nyumbani kwake licha ya ukongwe wake, kwa sababu tu alishikamana na amri za Mwenyezi Mungu na akabakia juu yake, akitangaza haki na bila kuogopa lawama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kulingania nusra ya watu wa Gaza kwa misiba mikali wanayokabiliwa na mbele ya kufeli kwa watu dunia kuwanusuru.

Ni fedheha na aibu iliyoje! Je, hamuogopi ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, enyi mnaozuia njia yake na kutetea batili ya watawala wenu, walinzi wa umbile la waliolaaniwa, mkinyamazisha midomo yenye kusema ukweli dhidi ya maadui wa Umma na Uislamu?! Basi mcheni Mwenyezi Mungu na mumjali Yeye, kwani hakika ushindi wa Mwenyezi Mungu unakuja kwa idhini yake, na umbile la Kiyahudi litatoweka bila ya shaka, na itatimia bishara njema ya Mtume Wake (swt) kuhusu kuregea kwa Khilafah Rashida. Basi jiokoeni, acheni ukandamizaji wenu, na jiungeni na Ummah wenu, na chukueni msimamo wa heshima unaomridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini.

Hizb ut Tahrir imejitolea katika kufanya kazi kwa ajili ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Jueni kwamba ukamataji wenu utaongeza dhamira na azma yake ya kufanya kazi kuelekea kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hizb ut Tahrir itabaki kuwa kiongozi muaminifu asiyesaliti watu wake.

[وَاتَّقُوا يَوْماً لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئاً وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ]

“Na iogopeni Siku ambayo mtu hatomfaa mtu kwa lolote, wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake; wala hawatanusuriwa.” [Surat Al-Baqara: 48]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu