Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
| H. 24 Rabi' II 1447 | Na: 1447 / 10 |
| M. Alhamisi, 16 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Licha ya Serikali ya Jordan Kuwaangusha Watu wa Gaza na Kujisalimisha Kwake kwa Mpango wa Trump, Vyombo Vyake vya Usalama Vyamkamata Mmoja wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)
Serikali ya Jordan inaendelea kwa kiburi katika dhambi na uvamizi, licha ya kuwaangusha watu wa Gaza, na kwa hakika ushirikiano wake na umbile la Kiyahudi katika vita vya mauaji ya halaiki ambavyo imepigana katika Ukanda wa Gaza, kwa kulipatia njia za uwezeshaji na uhai. Haikusita kumbariki Trump mhalifu katika kuifilisi kadhia ya Palestina kwa kuhudhuria kile kinachoitwa “Baraza la Amani” ili kuwa shahidi wa uongo wa mpango wa Trump wa udhibiti juu ya ardhi za Waislamu na kwa kupotea kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina.
Badala ya kuficha usaliti na kufeli kwake, vyombo vyake vya usalama mnamo 8 Oktoba 2025 vilimkamata kikatili Ustadh Khalid Al-Ashqar (Abu Al-Mu'tazz), mmoja wa wanachama wa Hizb ut Tahrir, kutoka mlangoni mwa msikiti alipokuwa akitoka kwenye swala (pamoja na kumkamata shemeji yake wakati huo huo kutoka sehemu nyengine); kwa ajili tu ya kuzungumza na imamu wa msikiti mapema kuhusu hali ya Gaza na wajibu wa kuinusuru, na kile ambacho Ummah unalazimishwa kufanya na Shariah ili kuinusuru—hivyo kuzuia neno la haki ambalo Mashababu wa Hizb ut Tahrir wanalizungumza, wakitimiza wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu—wakati ambapo miji kote ulimwenguni inachemka juu ya mauaji ya halaiki yanayofanywa na Mayahudi huko Gaza.
Kuongezeka kwa kampeni ya ukandamizaji ya utawala dhidi ya neno la haki linalosemwa katika kufichua uzembe wake na kuegemea kwake kwa umbile la Kiyahudi na Amerika, na kufeli kwake kutekeleza wajibu wake wa kuwanusuru watu wa Gaza kwa kuhamasisha majeshi, kunaonyesha msisitizo wake wa kuendelea katika unyenyekevu wake kwa Wakoloni makafiri wa Magharibi na dhulma yake kwa watu wa Jordan na Palestina, na kuendelea kwake kushirikiana na maadui wa Ummah na kuwaegemea, wakati neno la haki linapoitikisa mbele ya udhalimu wake.
Na kama mnavyoijua Hizb ut Tahrir, haitachoka wala kukatishwa tamaa na kukamatwa huku na ukandamizaji unaofanywa na serikali dhidi ya wanachama wake, wala kwa kutoangaziwa na vyombo vya habari. Haitakatishwa tamaa kufafanua misimamo yake na lengo lake ambalo inalifanyia kazi kupitia mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa, ambayo ni kuregeshwa kwa mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume — dola ambayo itahamasisha majeshi kuangamiza umbile la Kiyahudi na mikono ya Amerika na mipango yake kwa eneo hilo, na itaregesha heshima na hadhi ya Ummah.
[الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ]
“Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa.” [Aal-i Imrān: 173]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |



