Afisi ya Habari
Kenya
H. 17 Jumada II 1446 | Na: H 1446/05 |
M. Alhamisi, 19 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Chini ya Urasilimali Utunzaji wa Afya huwa kama Fadhila tu wala Hauchukuliwi kuwa ni Haki Msingi
(Imetafsiriwa)
Serikali imeanzisha Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) ili kusimamia bima ya afya ya jamii nchini. SHA ina hazina tatu za kifedha: Hazina ya Huduma ya Afya ya Msingi, Hazina ya Bima ya Afya ya Jamii na ile ya hali ya Dharura na Ugonjwa hatari. Watoa huduma za afya nchini Kenya wanaweza kuingia katika kandarasi na mamlaka ya SHA ili kutoa huduma za afya kwa walengwa.
Sisi katika Hizb ut Tahrir /Kenya tungependa kueleza yafuatayo:-
Mfumo wa SHA, unaotajwa kuwa unanuia kubadilisha sera ya fedha za afya nchini, unatajwa na serikali kama mfumo ulio bora zaidi kimanufaa kuliko ule wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) uliogubikwa na visa vya rushwa. Hata hivyo, muungano wa mashirika ya Safaricom, Apeiro na Konvergenz Network Solutions Ltd ulishindwa kuwa na mfumo mzuri wa sera za kiutendakazi kuhusiana na SHA. Gharama ya mpango huu wa haraka kama kawaida huanguka kwenye mabega ya walipa kodi ambao tayari wamelemewa na ushuru unaotozwa na utawala usioonyesha huruma.
Katika Mfumo wa Kirasimali, faida ndio kichocheo kikuu cha huduma zozote za sera za kifedha. Kwa msingi huu, kuhama kutoka NHIF hadi SHA kuko mbali kabisa na suala la kuboresha kiwango cha afya cha raia wa kawaida. Hii ni kwa kuwa msukumo mkubwa ni faida ambayo tawala za kibepari zimetanguliza juu ya majukumu yote ya kijamii. Uhalisia huu sio kwa Kenya tu bali ni duniani kote, mfano mzuri ukiwa ni dola kuu leo ya Marekani ambapo wagonjwa wanaohitajia gharama kubwa kwa serikali wamekuwa wakipuuzwa na kuhatarishwa afya zao kwa sababu tu ya uchu wa kampuni za bima ya afya hali inayosababisha vurugu miongoni mwa jamii. Kisa cha karibuni ambacho ni ukweli usiopingika ni kuuwawa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa United Healthcare, Brian Thompson.
Tunasema kwamba maslahi yoyote ya umma ni lazima yatekelezwe na serikali kwani huingia kwenye majukumu yake na hili ni kulingana na maneno ya Bwana Mtume (saw): «الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam/ Kiongozi ni mchungaji na ataulizwa juu ya watu anawaochunga”
Kwa muktadha huu, Uislamu umefanya huduma ya afya kuwa ni jukumu la msingi la Serikali na sio fadhila kwa raia; kwa maana hiyo, ndio Uislamu ukawajibisha kwamba usimamizi wa afya unaangukia serikali pekee. Huduma ya afya ya serikali lazima iwe bila malipo kwa raia wote wa Khilafah, Waislamu na wasio Waislamu. Huduma ya afya lazima iwepo, thabiti na ya viwango vya juu kwa wote.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |