Afisi ya Habari
Kenya
H. 29 Rabi' II 1446 | Na: H 1446/04 |
M. Ijumaa, 01 Novemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Uzinduzi wa Kampeni ya Kijamii ya Hizb ut Tahrir / Kenya chini ya Kauli Mbiu:
Uislamu Suluhisho Bora la Migogoro ya Kinyumbani
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir/Kenya imezindua rasmi kampeni ya kushughulikia masuala ya kijamii ambayo itaendeshwa kwa muda wa mwezi mmoja. Kampeni hii ya mwezi mmoja itaanza tarehe 1 Novemba 2024 na kumalizika tarehe 1 Disemba 2024.
Lengo la kampeni hii ni kuangazia uhalisia wa mfumo wa kijamii wa kibepari na jinsi ulivyosababisha maovu kadhaa ya kijamii katika mujtamaa, ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa ndoa, migogoro ya ardhi, mizozo ya kinyumbani na kiwango kikubwa cha talaka.
Wakati wa kampeni hii Hizb ut Tahrir itawasilisha mtazamo wa wazi wa Mfumo wa Kiislamu juu ya masuala yanayohusiana na familia pamoja na kuukumbusha Umma wa Kiislamu katika kushikilia Shakhsiya ya Kiislamu. Tunaamini kwa uthabiti kuwa kukosekana kwa utekelezaji wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha kumesababisha kuzorota sio tu muundo wa kijamii bali kisiasa na kiuchumi pia. Ni Uislamu ambao ulipotekelezwa kwa karne 13 na Khilafah ulitatua changamoto zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Pia tunaamini kwamba mara tu Khilafah itakaposimamishwa kwa Njia ya Utume matatizo yote yatatatuliwa.
Amali za kampeni zitajumuisha darsa, mazungumzo ya mitaani, semina na wasomi miongoni mwa nyengine.
Tunatoa wito kwa umma kwa jumla na hasa Umma wa Kiislamu kuungana nasi katika kampeni hii tukufu ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Tunamuomba (swt) aifanikishe kampeni hii na kuifanikisha kwa Ummah mzima wa Kiislamu.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |