Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 3 Dhu al-Hijjah 1444 | Na: 1444 H / 040 |
M. Jumatano, 21 Juni 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Duara Ovu la Ulanguzi wa Binadamu ni la Milele Ndani ya Ubepari
(Imetafsiriwa)
Takriban wakaazi 15 wa Ende Regency, Nusa Tenggara Mashariki (NTT) - jimbo la visiwa mashariki mwa Indonesia - walikuwa wahasiriwa wa uhalifu wa usafirishaji haramu wa binadamu (ulioripotiwa mnamo tarehe 5 Juni 2023). Walitumwa kinyume cha sheria kufanya kazi katika kampuni moja ya Malaysia huko Pekanbaru mnamo Oktoba 2022, lakini waathiriwa hawakupewa mshahara hadi mwezi wao wa tano wa kazi. (Detik.com). Tukio hili ni hadithi moja tu kati ya hadithi nyingine nyingi za kusikitisha kutoka NTT. Hapo awali kulikuwa na Meriance Kabu, mwanamke ambaye alifanya kazi kama mfanyikazi wa ndani asiye na utaratibu mwaka wa 2014 nchini Malaysia. Wakati wa miezi minane ya kazi yake nchini Malaysia, Meriance alikabiliwa na "mateso yenye kusababisha majeraha". Kwa bahati nzuri, bado aliweza kurudi nyumbani akiwa hai. Kuanzia 2014 hadi 2022, zaidi ya wafanyikazi 700 wahamiaji wa Indonesia kutoka NTT wamerudi nyumbani wakiwa ndani ya majeneza. (Habari za BBC)
Mkoa wa NTT ni mojawapo ya mifuko mikubwa ya biashara ya ulanguzi wa binadamu nchini Indonesia. Labda kwa sababu hii, NTT ilichaguliwa kama eneo la Mkutano wa 42 wa ASEAN Mei uliopita. Suala la usafirishaji haramu wa binadamu likawa moja ya masuala makuu yaliyoangaziwa, na kupelekea tamko la kutokomeza biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu, haswa katika suala la matumizi mabaya ya teknolojia, kwa sababu njia nyingi za uhalifu hufanyika mtandaoni ambazo zimeenea zaidi tangu janga la Covid-19. Indonesia ndiyo nchi kubwa zaidi katika ASEAN ambayo ina wahanga wengi zaidi wa biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu. Hivi sasa kuna wafanyikazi wahamiaji milioni 4.4 wa Indonesia wasio na hati nje ya nchi, wengi wao wakiwa wanawake. Mkuu wa BP2MI (Wakala wa Ulinzi wa Wafanyikazi Wahamiaji wa Indonesia) Benny Rhamdani alisema hakika ulanguzi wa binadamu umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu sana, ni kana kwamba makundi na mafia wanaopata faida kubwa kutokana na biashara hii chafu hawajagunduliwa. Pia aliongeza kuwa hasa kwa msaada wa teknolojia, sasa waathirika zaidi na zaidi wanatoka kwa watu waliosoma.
Katika mfumo huu fisadi wa kibepari, udhalilishaji wa binadamu unakuwa rahisi kutokana na nafasi dhaifu ya serikali, umaskini, udhibiti wa polepole na unaosababishwa na maisha ya anasa na mizigo mikubwa ya kiuchumi ya watu binafsi. Teknolojia pia husaidia kuwezesha mtandao wa mashirika ya ulanguzi wa binadamu kuwa na mpangilio zaidi. Kinaya ni kwamba, ingawa mfumo wa utumwa ulikomeshwa zamani na kauli mbiu za kisasa za haki za binadamu mara nyingi zinasisitizwa, desturi ya ulanguzi wa binadamu inaongezeka, na tunahisi kana kwamba tumerudi katika zama za katikati. Ulanguzi wa binadamu kwa hakika ni mtindo mpya wa utumwa. Ingawa vitendo na mbinu ni tofauti, dhati yake ni inakaribiana na utumwa wa zamani, yaani wanadamu wanachukuliwa kuwa ni bidhaa zinazoweza kutumiwa na kudhulumiwa kwa hiari na kunyimwa haki zote. Uwepo wa Mkutano wa ASEAN huko Labuan Bajo NTT mwezi uliopita haukuwa chochote zaidi ya sherehe na uthibitisho kwamba kiwango cha udhibiti sio cha haraka kama kiwango cha uhalifu wa ulanguzi wa binadamu. Nchi ya Kiislamu kama Indonesia imekabiliwa na suala la wafanyikazi wahamiaji kwa karibu miongo 4 ikiwa na mabadiliko mbalimbali ya sheria na kanuni. Hata hivyo, janga hili halijakoma na halitakoma kamwe, kwa sababu makundi ya magendo ya ulanguzi wa binadamu ni duara ovu ambalo daima litakuwa ni mwindaji, mwenye kuwinda mzunguko wa umaskini na ukosefu wa ajira kutokana na utabikishwaji wa mfumo mbovu wa kiuchumi wa Kibepari. Makundi haya yameongezeka chini ya mfumo wa kibepari ambao umekuza fikra za ulafi wa kupenda mali, na kutengeneza mazingira muafaka ya biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu.
Wakati huo huo, Uislamu unatoa ruwaza ya ukombozi wa mwanadamu ambayo inataka kukomesha tabia ya utumwa, ikiahidi malipo makubwa kesho Akhera kwa wale wanaomkomboa mtumwa. Mafundisho ya Kiislamu yanatoa maadili matukufu ya kibinadamu kwa sababu yanawaweka wanadamu kuwa wa thamani zaidi kuliko vitu vya kimada na pesa. Hii ni pamoja na utabikishaji wa mfumo wa kupambana na riba, usawa, kodi ya chini na ugavi adilifu wa mali – mfumo wa kiuchumi ili dola iwe huru na umaskini na mitego ya ukandamizaji wa kiuchumi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[...وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ * فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ * وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ * فَكُّ رَقَبَةٍ...]
“…Na tukambainishia zote njia mbili? Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? Kumkomboa mtumwa …” [Al Balad: 10-13].
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |