Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 10 Dhu al-Hijjah 1444 | Na: 1444 H / 043 |
M. Jumatano, 28 Juni 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamia ya Wanawake na Watoto Wanazama kwenye Vifo vyao katika Ulimwengu wa Kibepari na Kizalendo Uliovuliwa Ubinadamu wake
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 18 Juni, 2023, BBC iliripoti juu ya kuzama kwa mashua iliyokuwa imebeba wahamiaji zaidi ya 500 kutoka pwani ya Ugiriki. Picha za mashua hiyo iliyochukuliwa na walinzi wa pwani kabla ya kuzama zinaonyesha mamia ya wanaume wakiwa wamejazana kwenye sehemu ya juu. Mashua hiyo ilitengenezwa kubeba sehemu ndogo tu ya idadi hiyo ya watu. Kati ya watu 104 waliookolewa bado mamia hawajulikani walipo. Kumekuwa na maelezo ya kutisha ambayo yameibuka kutoka kwa ushuhuda wa walionusurika. Watu waliokuwa kwenye mashua hiyo waliripoti kwamba "ilikuwa inakunywa maji ya bahari kwa angalau siku mbili" kabla ya kuzama.
Msemaji wa afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Jeremy Laurence amenukuliwa akisema: "Idadi kubwa ya wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waliopotea katika 'mkasa huo wa kutisha'". Baadaye ilifahamika kuwa watoto 100 walikuwa wamefichwa eneo la chini la mashua, ambayo ilizama chini ya bahari.
Uzembe na kutelekezwa kwa makusudi kwa watu wasio na hatia waliokuwa wabeabiri chombo hicho ilianakiliwa na waandishi wa habari walioripoti mkasa huo. Mwanzoni, walinzi wa pwani walisema walikuwa wameweka "masafa ya tahadhari" kutoka kwa mashua hiyo. Lakini gazeti la Ugiriki la Kathimerini lilinukuu chanzo kimoja kikisema walinzi wa pwani walikuwa wamefunga kamba kwenye mashua hiyo ili wafanyikazi wake waangalie hali yake, na wale waliokuwemo ndani waliifungua ili kuendelea kuelekea nchini Italia. Msemaji wa serikali Ilias Siakantaris alithibitisha mnamo siku ya Ijumaa kwamba walinzi wa pwani "walitumia kamba kujiimarisha, kukaribia, kuona kama walitaka msaada wowote." Lakini akasisitiza: “Hakukuwepo na kamba ya kufunga,” akiashiria kuwa hakukuwa na jaribio lolote la kuivuta mashua hiyo au kuifungasha kwa muda wote. Wengi wa abiria walikuwa ni Wamisri, Wasyria, Wapakistani, Waafghan na Wapalestina.
La hawla wala Quwatta Illah Billah! Je, ni unyama wa aina gani unaoandaa ulimwengu kwa mamia ya wanawake na watoto kuachwa kuzama baharini? Uko wapi uwajibikaji wa watawala wetu ambao wamenyamazia kimya mateso ya wanawake na watoto wetu? Tunaishi chini ya mfumo wa kiulimwengu wa kibepari ambao unawasukuma mbali watu waliokata tamaa na walio hatarini zaidi kutoka fukwe zao kwa sababu ya maslahi ya kitaifa na kiuchumi. Ni mfumo wa kiulimwengu usio na maadili ya kiakhlaqi na ya kibinadamu.
Hakuwezi kuwa udhuru wowote kwa upuuzaji huu wa kimakusudi wa mambo yetu na kuwatelekeza ndugu na dada zetu hadi kufa kwao. Ukiukaji wa kulinda uhai wa Waislamu ni kitendo kinachomkasirisha Mwenyezi Mungu Al-Malik Al-Jabbar. Sisi, kama Waislamu, hatuwezi kushuhudia maelfu ya ndugu na dada zetu ambao wameachwa kuzama na hawana msaada kwa hili. Watu hao tunaowaona wakifa kwenye vyombo vya habari ni sehemu ya idadi ya vifo vya kweli, kwani wahamiaji wengi hawaangaziwi na hupoteza maisha katika njia ya kutisha zaidi. Je! Watoto wa kesho katika mikono ya Mwenyezi Mungu watasema nini kuhusu kusalitiwa uaminifu wao wanapoitwa kutoa ushahidi wa haki zao zilizokiukwa?
Enyi Waislamu! Hakuna ucheleweshaji unaoweza kuwa hoja katika kazi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume kuchunga masuala ya maisha yaliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Lazima muharakishe kuisimamisha haraka iwezekanavyo ambayo kamwe haitaruhusu kutelekezwa na kupuuzwa kwenu. Bali itafungua ardhi yake kwa waliodhulumiwa na kuwapa ulinzi, hifadhi ya heshima, na kushughulikia mambo yao, bila kujali utaifa, rangi au dini yao - kwa kuwa hii ndio alama ya dola iliyostaarabika, yenye utu inayoongozwa na Sheria za Muumba Al-Aziz Al-Kareem.
[إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ]
“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbiya: 106]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |