Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  4 Jumada II 1445 Na: 1445 H / 018
M.  Jumapili, 17 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhalifu wa Kikatili na Mauaji ya Uwanjani, Hivi Wako Wapi Ndugu wa Dini na Walinzi?!
(Imetafsiriwa)

Uchunguzi wa Haki za Binadamu wa Euro-Mediterranean ulinakili ugunduzi wa miili takriban 15 iliyooza katika Shule ya Serikali ya Shadia Abu Ghazaleh katika eneo la al-Fallujah, magharibi mwa kambi ya Jabalia. Uchunguzi wa awali ulifichua kwamba waliuwawa uwanjani wakati wa kuhojiwa na jeshi la umbile halifu la Kiyahudi. Uchunguzi huo uliongezea kuwa miili ya mashahidi hao ilipatikana baada ya magari kijeshi ya jeshi la uvamizi kuondoka kutoka ndani na pambizoni mwa shule hiyo iliyotajwa baada ya kuweko hapo kwa siku kadhaa na kuwanyanyasa watu wasio na makao ambao walikuwa wamekimbilia huko. Kulingana na walio shuhudia, kati ya mashahidi hao walikuwa wanawake, watoto, na wazee.

Sera ya wauwaji ya uwanja iliyotekelezwa na askari wa uvamizi dhidi ya raia katika majumba, hospitali na vichochoro ambazo zilisemekana kuwa salama inadhihirisha ukatili na uhalifu wa umbile hili halifu na oga, ambalo huelekeza hasira yake kwa raia wasio na ulinzi, wanawake na watoto ambao wawekuwa ni benki kwa malengo yake. Je! Raia hawa waliuawa kwa dhambi gani?! Je! Wanawake, watoto na wazee wanaleta hatari gani kwa umbile hili halifu?!

Maadili na miito yote bandia ya kibinadamu yameanguka na ukweli wa wale walioyabeba katika vita hivi vya kikatili umedhihirika. Uhalisia wa taasisi na mashirika ya kibinadamu pia umedhihirika na kwamba ni ala mikononi mwa dola za kikoloni, na kwamba hunyanyua kauli mbiu ya haki na ubinadamu pindi hilo linapotumikia maslahi ya mabwana zao. Walakini, linapokuja suala la Waislamu, wao ni viziwi, mabubu, na vipofu. Badala yake, ni washirika katika uhalifu wa kikatili unaofanywa dhidi ya watu wa Gaza. Uhalisia wa taasisi za utetezi wa wanawake ambazo zilikuwa zikifanya kazi kwa bidii huko Gaza kabla ya vita kueneza ufisadi, kufisidi familia ya Kiislamu na kuwafanya wanawake haswa kuasi dhidi ya hukmu za sharia pia umedhihirika, lakini leo wako kimya kuhusu uhalifu wa kikatili wa umbile la Kiyahudi dhidi ya wanawake na watoto.

Umbile hili halifu halingefanya uhalifu huu wa kikatili mbele ya ulimwengu, unaonakiliwa kwa sauti na video, kama isingekuwa msaada wa dola za kikoloni, zikiongozwa na Marekani, kiongozi wa uovu na uhalifu, ambayo ililipa idhini na kulisambazia pesa na silaha kufanya mauaji dhidi ya watu wa Gaza, na kama isingekuwa kwa njama na usaliti wa watawala wa Kiarabu na Waislamu na ulinzi wao, umbile hili lisingekuwa salama, kwani watawala hawa wameufunga Ummah na majeshi yake ili wasisonge kuling’oa na kuwanusuru watu wa Gaza.

Enyi Waislamu: Wasaidieni watu wa Palestina, wasaidie watu wa Gaza, na muwafikie kabla ya umbile hili halifu kuwaangamiza. Na muwakane watawala wenu wasaliti, na muwashike mkono watoto wenu ndani ya majeshi ili waweze kusonga kuwanusuru ndugu zenu huko Gaza na Palestina yote.

Enyi Askari na maafisa katika Majeshi ya Waislamu: Je! Unasubiri nini karibu kutokea ili uchukue hatua ?! Je! Ni lini mutagundua kuwa hakuna utiifu kwa kiumbe ikiwa anamuasi Muumba, na kwamba watawala hawa na mabwana zao watakukana Siku ya Kiyama ikiwa mutaendelea kuwatii na kushindwa kuwanusuru ndugu zenu. Basi je! Mutakuwa miongoni mwa waliohasirika hapa ulimwengu huu na Akhera?! Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[إِذْ تَبَرَّأَ ٱلَّذِينَ ٱتُّبِعُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ وَرَأَوُاْ ٱلْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ ٱلْأَسْبَابُ]

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao.” [Al-Baqarah 2:166]. Basi kuweni upande wa Umma wenu na muyaandike majina yenu kwenye sajili za utukufu hapa duniani na Akhera.

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu