Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 9 Jumada II 1445 | Na: 1445 H / 019 |
M. Ijumaa, 22 Disemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Je, Palestina Tutaikomboa Vipi?”
Kongamano la Kimataifa la Wanawake Mtandaoni juu ya Palestina Lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa Ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni
(Imetafsiriwa)
Huku mauaji ya halaiki na mzingiro wa kikatili juu ya Gaza yakiendelea, na ugaidi, kukamatwa kwa watu wengi na mauaji ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi yakipamba moto mikononi mwa umbile katili uaji la Kizayuni, miito imepazwa kote ulimwenguni, kutoka kwa Waislamu na vilevile wasiokuwa Waislamu, ya ‘Ukombozi wa Palestina’. Hata hivyo, ufafanuzi unahitajika wa ‘Ukombozi wa Palestina’ inajumuisha nini kiuhalisia na jinsi ukombozi wa Palestina unaweza kupatikana kivitendo. Baadhi wanaendelea kuunga mkono lile linaloitwa suluhisho la dola mbili kumaliza umwagaji damu, huku wengine wakipigia debe uanzishwaji wa dola moja kwa msingi wa kanuni za kisekula za kidemokrasia ambapo Waislamu, Mayahudi na Wakristo watagawanya mamlaka ya kisiasa.
Pia kumekuwa na miito ya kulisusia umbile la Kizayuni na kampuni zinazoliunga mkono, na pia kukoleza shinikizo kwa serikali kuulazimisha uvamizi wa mauaji ya halaiki kukomesha mauaji yake ya watu wengi na kukubali kusitisha mapigano. Pamoja na hayo, kumekuwa na wito wenye nguvu unaotoka kwa Waislamu kote ulimwenguni wa ukombozi wa Ardhi nzima Iliyobarikiwa ya Palestina kwa kuhamasisha majeshi ya Waislamu kupitia usimamishaji wa uongozi wa mfumo na dola ya Kiislamu - Khilafah kwa njia ya Utume. Hivyo ni ipi njia na mbinu ya kweli ya ‘Ukombozi wa Palestina’?
Mnamo Jumamosi Disemba 30, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Wanawake wa Hizb ut Tahrir ulimwenguni kitaandaa Kongamano la Kimataifa la Wanawake la Mtandaoni juu ya Palestina kujibu swali hili kwa undani. Amali hii itajumuisha wanapaneli wa kike kutoka Palestina, Uturuki, Tunisia, Indonesia, Amerika na Uingereza.
Kongamano hili litachunguza kwa undani mapendekezo na masuluhisho mbali mbali yanazowasilishwa kukomesha mauaji ya halaiki ya Gaza na kuleta haki na ulinzi kwa Waislamu wa Palestina. Litahoji dori na umuhimu wa Umoja wa Mataifa na Mfumo wa Kilimwengu wa Kimataifa katika kuzuia mauwaji wa kimbari ya Wapalestina kutoka ardhi yao. Litashughulikia vizuizi vikuu vyenye kuzuia ukombozi wa Palestina na ambavyo vinawezesha uendeleaji wa uhalifu wa umbile la Kizayuni. Na litauliza ni kwa nini serikali za ardhi za Waislamu zimeshindwa kutumia nguvu na ushawishi wa kiuchumi, kisiasa, kimkakati na kijeshi kuwalinda Waislamu wa Palestina kutokana na uvamizi huu wa kikatili na kusaidia ukombozi wa Ardhi hii Iliyobarikiwa. La muhimu, kongamano hili litashughulikia suluhisho la Kiislamu, la kivitendo na la kudumu kwa ukaliwaji kimabavu wa Palestina, na dori ya Ummah wa Kiislamu, watu wao wenye ushawishi, wanazuoni na majeshi yao katika kukomesha umwagaji damu huu. Pia litahoji iwapo uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu kuikomboa Ardhi nzima ya Palestina kutokana na ukaliwaji kimabavu wa Wazayuni ni lengo la kihakika, na ikiwa ni hivyo - vipi linaweza kupatikana. Kwa kuongezea, amali hii itajadili jinsi amani na usalama kwa Waislamu, Wakristo, Mayahudi na wale wa imani zote inaweza kupatikana tu eneo hilo kupitia kurudi kwa utawala wa Kiislamu wa dola ya Khilafah ambayo inafurahia urithi wa kihistoria wenye kuhakikisha haki za watu wa imani zote, jamii na makabila chini ya mfumo wake zilihakikishwa na kulindwa. Wanapaneli pia watatoa ufahamu juu ya fikra, mhemko na wito wa umma, watu wenye ushawishi na majeshi ndani ya eneo lao dhidi ya uvamizi wa Palestina.
Tunatumai Bi idhnillah kwamba kongamano hili litafafanua njia wazi ya ukombozi wa Palestina ili kukomesha kiwango kisichoelezeka cha mateso, maumivu, dhulma na udhalilishaji wanaopitia ndugu na dada zetu kwa zaidi ya miongo saba ya giza. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfaal 8:72]?
Kongamano hili ni HAFLA YA WANAWAKE PEKEE na litakuwa kwa Kiingereza. Litafanyika 12:30pm GMT (3:30pm Saa za Madina). Kwa maelezo zaidi au ili kuhudhuria kongamano hili, tafadhali wasiliana na anwani ifuatayo:
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |