Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 22 Rabi' I 1446 | Na: H 1446 / 030 |
M. Jumatano, 25 Septemba 2024 |
Kongamano la Kimataifa la Wanawake la Mtandaoni Lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa Uratibu na Wanawake wa Hizb ut Tahrir Ulimwenguni
(Imetafsiriwa)
Mwaka mzima umepita tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vikali vilivyofuata huko Gaza. Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, watu wa Gaza wamevumilia mitihani mikubwa, wakiishi katika machungu, mateso, na majanga yasiyohesabika: kuhamishwa, mauaji, njaa... mabaki yaliyotawanyika ya watoto na wanawake yaliyokusanywa kwenye mifuko, na mashahidi walionaswa chini ya vifusi, wasiowezekani kutolewa, na kuongeza katika maumivu na huzuni kutokana na kushindwa kuwaheshimu na kuwazika. Mauaji ya kikatili ya halaiki yanafanywa na umbile halifu kwa mtazamo kamili wa ulimwengu ambao unashiriki na kupuuza. Hata hivyo, licha ya mikasa na majonzi ya vita hivi, vimejaa mafunzo na tafakari zinazotolewa na kundi aminifu, vumilivu na thabiti linalosimama kidete dhidi ya njama za maadui na khiyana za watawala na wale wanaodai kuwa marafiki. Kundi hili dogo, bila kukatishwa tamaa na wale waliowatelekeza, linabaki stahimilivu, bila kupoteza kamwe tumaini la ushindi wa Mola wa mbingu na ardhi. Licha ya vilio, maombi, na wito wa kuomba msaada kutoka kwa watu wa Gaza, majibu yamefichua na kudhihirisha usaliti wa watawala wa Waislamu ambao wamekaa kwenye viti vyao vya utawala, viziwi, mabubu na vipofu kwa uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile hilo halifu dhidi ya watu wa Gaza na Palestina kwa jumla. Watawala hawa wamejitolea kuonyesha uaminifu na utiifu kwake, kuhalalisha mahusiano nalo, na kuimarisha uwepo wake.
Vita hivyo pia vimewafichua sura za wanazuoni wengi, na kuwafichua wakweli kutoka kwa wadanganyifu. Vimefunua pazia machoni, vikionyesha ukweli wa kile kinachotokea. Asili ya halisi ya mzozo wa Palestina imekuwa wazi: mapambano kati ya haki na batili, kati ya Waislamu wa Palestina na umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, nyakuzi, la kikafiri. Ndiyo, watu wa Palestina kwa jumla, na hasa Gaza, wameuita Ummah. Hivyo, je jibu lilikuwaje? Lilikuwa dhaifu, likidhihirika katika maandamano machache, au kususia baadhi ya taasisi na maduka yanayounga mkono umbile hilo, au kutuma chakula na nguo kama msaada! Licha ya umbile hilo vamizi kuendelea kutekeleza uhalifu wa kivita mmoja baada ya mwingine, na licha ya maombi yote hayo yanayokaririwa, vilio vya kuomba msaada, na matukio ya kuhuzunisha, kimya cha dunia nzima, usaliti wa serikali, kimya cha Umma wa Kiislamu na majeshi yake, na ukosefu wao wa kuchukua hatua yamekuwa, na bado yangali, kama majibu yao!
Haya yote yanazua maswali kuhusu sababu za kuzuia kumalizika kwa mauaji haya ya halaiki na ukombozi wa Palestina! Je, ni suluhisho gani la msingi ambalo kwalo kadhia hii inaweza kutatuliwa milele? Maswali haya na mengine yatashughulikiwa na kujibiwa mnamo Jumamosi, Oktoba 5, 2024, wakati wa kongamano la kimataifa la wanawake la mtandaoni lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote duniani, chini ya kichwa: “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema” Kongamano hili litaainisha njia sahihi ya kutatua kadhia hii na mambo mengine yanayohusu Umma wa Kiislamu. Litaangazia nukta muhimu za kadhia ya Palestina na kutoa suluhu zinazohitajika ili kukomesha mateso ya watu wa Palestina na Waislamu kwa jumla, kwa kuzingatia kuwa ni kadhia ya Ummah mzima na sio kadhia ya kitaifa inayofungamana na mipaka bandia iliyoundwa na dola za kikoloni. Wazungumzaji kutoka Palestina, Tunisia, Syria, Lebanon, Indonesia, na Amerika watashiriki. Kongamano hili litawafichua wale wanaozuia kumalizika kwa mauaji hayo ya halaiki, kufafanua sababu za kuzuia kukombolewa Palestina kutoka kwa Mayahudi, na kujadili dori ya taasisi za kimataifa na maamuzi yao katika kula jama dhidi ya kadhia ya Palestina. Zaidi ya hayo, litazungumzia dori ovu ya vyombo vya habari katika kupotosha na kuficha ukweli, na kuionyesha kama ni kadhia ya kitaifa au ya kikabila, ili kuwapotosha Waislamu kutoka kwenye njia sahihi ambayo wanapaswa kufuata ili kuitatua kimsingi.
Kongamano hili pia litazungumzia dori ya Umma wa Kiislamu katika kufikia suluhisho hili la kimsingi, ambalo lazima litoke kwenye Aqida (itikadi yake). Litaangazia kwamba masuluhisho yaliyopandikizwa na maadui na wakoloni ni silaha tu zinazotumiwa kuupiga vita Ummah, kuupotosha kutoka kwenye njia sahihi. Masuluhisho ya kivipande na ya muda yanayopendekezwa si chochote zaidi ya njia ya kuutia ganzi Ummah, kuuzuia kuchukua dori ambayo lazima uicheze. Kongamano hilo pia litaelezea vikwazo vinavyowazuia watu kutabanni ruwaza ya Kisharia kwa ajili ya ukombozi wa Palestina, na litafafanua kwa nini majeshi yanasalia katika kambi zao, kutoitikia wito wa mara kwa mara wa kuchukua hatua.
Zaidi ya hayo, kongamano hilo litafichua juhudi zinazolenga kupanua mwanya kati ya Ummah na majeshi yake kwa kuyaonyesha majeshi hayo kuwa hayana nguvu, tiifu kwa tawala, na hayana uwezo wa kutoa nusra au ushindi. Madai na tuhma hizi zitakanushwa kwa kutoa mifano ya watu wenye ikhlasi ndani ya jeshi waliojitolea mhanga kwa ajili ya dini yao na ushindi wake, na kubainisha dori ya ufahamu na rai jumla katika kuwahamasisha watu wengi wenye ikhlasi katika majeshi kuchukua hatua.
Aidha, kongamano hilo litafichua sababu msingi zilizo nyuma ya kuweka mzigo wa kukomboa ardhi takatifu kwa watu wa Palestina pekee, huku zikificha mjadala kuhusu dori ya Umma na majeshi yake, ambayo yana vifaa vya kutosha na yako tayari.
Kongamano hilo pia litaangazia dori ya kila Muislamu katika kutatua kadhia hii, kwa kuzingatia makhsusi wanawake wa Kiislamu na hatua wanazopaswa kuchukua ili kuchangia kukomesha mauaji ya halaiki na uchinjaji unaofanywa dhidi ya watu wetu wa Gaza na Palestina kwa jumla. Litasisitiza wajibu wao wa kufanya kazi pamoja na wengine wanaopigania ukombozi wake. Kongamano hilo litasisitiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi na tamkini, na kutukumbusha kwamba faraja huja baada ya dhiki, na kwamba ushindi hufuata mitihani. Litasisitiza tena utukufu wa Ummah huu, wenye uwezo wa kupata ushindi Inshallah.
Tunaomba kwamba kongamano hili litaangaza njia sahihi ambayo Ummah unapaswa kuchukua ili kuregesha tena mamlaka yake, uongozi, na kufikia ukombozi wa Palestina kutoka mikononi mwa maadui na makafari. Kama anavyosema Mwenyezi Mungu:
[وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ] “Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj:40].
Jiungeni nasi, kina dada, katika kongamano hili la kimataifa kupitia link ya Zoom:
https://us06web.zoom.us/j/81685047416
Kongamano hili litakuwa kwa lugha ya Kiarabu.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |