Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 5 Rabi' II 1446 | Na: H 1446 / 033 |
M. Jumanne, 08 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chafanya kwa Mafanikio Kongamano la Kimataifa la Wanawake Mtandaoni
“Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”
(Imetafsiriwa)
Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni, kilifanya kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni lenye mafanikio kwenye jukwaa la Zoom kwa kichwa “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema” mnamo siku ya Jumamosi, Oktoba 5, 2024. Mamia ya wanawake wanaozungumza Kiarabu kutoka kote duniani walihudhuria kongamano hilo, katika ukumbi wa mikutano na kwenye kurasa za Facebook za Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Wazungumzaji kutoka Palestina, Tunisia, Syria, Lebanon, Indonesia na Amerika walishiriki katika kongamano hilo.
Kongamano hilo lilianza kwa usomaji mzuri wa aya za Qur'an Tukufu, na kufuatiwa na hotuba ya mwendesha kongamano ambaye alielezea mtazamo wa hali ya sasa ya Gaza na Palestina baada ya mwaka wa vita vya mauaji ya halaiki vinavyotekelezwa na umbile la Kiyahudi na miungano yake, kwa kula njama na kutochukua hatua kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu.
Wakati wa mjadala huo, washiriki walifafanua vikwazo vinavyozuia kukombolewa kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kutokana na ulaji njama wa watawala kwa manufaa ya umbile la Kiyahudi na Magharibi, bila kusahau utaifa na ukabila uliosambaratisha Umma. Pia waliangazia dori ya taasisi za kimataifa na mikataba yao, pamoja na vyombo vya habari vinavyofadhiliwa vinavyo husika na tawala zinazolenga kupotosha watu kwa kugeuza dira mbali na mwelekeo sahihi.
Kisha wakazungumza kuhusu dori ya Umma wa Kiislamu katika kutatua kadhia ya Palestina kwa njia ya kimsingi, ambayo lazima itoke kwenye Aqidah (itikadi) sahihi za Kiislamu na sio kutoka Magharibi au masuluhisho na mipango yake. Suluhisho litakuja tu kwa kufanya kazi ya kuinua neno la Mwenyezi Mungu na jihad, kwa kuwaondoa watawala wasaliti na kuyakusanya majeshi ili kuwakomboa na kuliondosha umbile la Kiyahudi na wafuasi wake. Licha ya pengo ambalo tawala za sasa zimetengeneza kati ya majeshi haya na Ummah, bado ipo kheri katika majeshi haya. Wanahitaji mtu wa kuwahamasisha kutekeleza wajibu wao, ili waweze kuulinda Ummah, na kuwashinda maadui zake.
Washiriki hao pia walizungumzia kuhusu dori ya wanawake na wanachama wengine wa Umma hususan wanazuoni na maimamu katika kukomesha uvamizi na mauaji ya kinyama, iwe ndani au nje ya Palestina.
Wazungumzaji walikuwa na shauku kubwa ya kueneza matumaini na kusisitiza bishara njema licha ya misiba yote, mauaji na hali duni ya Ummah, kwani baraka zinatokana na matatizo na nuru itang'aa licha ya giza. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume Wake (saw) na ni lazima sote tuifanye kazi ili tupate kheri ya maisha haya ya dunia na Akhera.
Wakati wa kongamano hilo, majibu yalitolewa kwa maswali mengi yaliyoulizwa katika ukumbi wa kongamano na kwenye kurasa za Facebook kupitia upeperushaji wa moja kwa moja.
Kongamano hilo lijumuisha uonyeshaji video kadhaa zilizotolewa na Kitengo cha Wanawake, ambazo zilionyesha kiwango cha uhalifu na ukatili unaofanywa na umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa Palestina, hasa Gaza. Vile vile zilifichua uhaini wa watawala wa nchi za Waislamu, na kwamba wote ni vibaraka na wasaidizi wa maadui wa Ummah, wanaofunga pingu mikono ya watu na kuwaruhusu maadui kudhibiti nchi, watu wao, na mali yao. Video hizi ziliwasilisha nguvu na uwezo wa majeshi, na ni silaha ngapi na vifaa vilivyomo kwenye kambi na maghala ambazo kwazo jeshi moja tu linaweza kuliondoa umbile la Kiyahudi, vipi basi ikiwa wote wangeunganishwa katika jeshi moja likiongozwa na Imam mmoja!
Wanawake wa Kiislamu walitoa wito kwa majeshi ya nchi za Kiislamu kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, pengine sauti na maneno yao yatagusa nyoyo za fahamu ndani ya majeshi haya, pengine tutamuona mtu kama Al-Mu'tasim.
Vile vile walisisitiza kheri ya Umma wa Kiislamu, na kwamba unahitaji tu mtu wa kuuongoza kwenye mwelekeo sahihi, mwenye silaha ya imani na uaminifu katika ushindi (nusrah) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na watu wa Gaza ni mfano hai wa hilo, vile vile dori ya wanazuoni na maimamu katika kuangaza njia ya Umma, kusema ukweli mbele ya watawala, na kuyahimiza majeshi kuwanusuru watu wa Palestina na Gaza.
Kongamano lilihitimishwa kwa dua yenye kugusa moyo, ambayo tunamuomba Mwenyezi Mungu aijibu.
Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kilikuwa kimetuma barua mbili za wazi kupitia tovuti za Afisi Kuu ya Habari; moja kwa watu wenye nguvu na uwezo katika majeshi ya Kiislamu ili kuwahimiza kuchukua hatua kuelekea kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na nyengine kwa kina mama, wake, mabinti na dada wa watu binafsi katika majeshi hayo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu zifikie masikio yenye fahamu na nyoyo zenye utambuzi.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |