Jumatano, 14 Muharram 1447 | 2025/07/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  8 Muharram 1447 Na: 1447 H / 002
M.  Alhamisi, 03 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto Wanakufa kwa Njaa... Huku Watawala Wakiendelea na Uzembe wao!
(Imetafsiriwa)

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Palestina mjini Gaza, Dkt. Munir Al-Barsh, alifichua kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaokufa kwa njaa, na kuthibitisha kwamba uvamizi "unafurahi kuwaua," huku kukiwa na mzingiro unaoendelea, kufungwa kwa vivuko, na kupuuza mfumo wa kimataifa. Katika mahojiano katika Chaneli ya Al Jazeera, Al-Barsh alisema kuwa idadi ya watoto waliouawa shahidi kutokana na utapiamlo uliokithiri imefikia 66 hadi sasa, kati yao wa hivi punde ni mtoto mchanga wa miezi mitatu Jouri Al-Masri, akibainisha kuwa makundi yaliyo hatarini zaidi, hasa miongoni mwao ni watoto, wamekuwa wahanga wakuu.

Maafa ya njaa katika Ukanda wa Gaza yamezidi kuwa mabaya kutokana na kuendelea kuzingirwa na umbile la Kiyahudi na kupungua kwa mahitaji muhimu. Afisi ya Habari ya Serikali mjini Gaza ilisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba uvamizi huo unaendelea kufunga vivuko na kuzuia kuingizwa kwa maziwa ya watoto wachanga na virutubishi vya lishe vilivyotengwa kwa ajili ya makundi dhaifu na yaliyo hatarini, haswa watoto wachanga na wagonjwa, ambayo imesababisha vifo vya watu 244 kutokana na njaa na ukosefu wa dawa, kati yao watoto 66, huku kukiwa na hofu ya kuongezeka kwa idadi hiyo chini uzembe na ushiriki wa kimataifa.

Asilimia 90 ya watoto wenye umri kati ya miezi 6 na 23, pamoja na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, wanakabiliwa na umaskini mkubwa wa chakula. Watoto wanakufa kwa njaa kulingana na ripoti ya hivi punde ya Global Nutrition Cluster, na kuna si chini ya 90% ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano walioambukizwa na ugonjwa mmoja au zaidi ya kuambukiza. Shirika la Afya Duniani pia lilitangaza kuwa karibu watoto 112 wanalazwa kila siku katika hospitali za Ukanda wa Gaza kwa matibabu kutokana na utapiamlo tangu mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na kizuizi kinachowanyonga.

Dkt. Al-Barsh aliieleza Al Jazeera kwamba ripoti za Shirika la Mpango wa Chakula Duniani zinathibitisha kuwa takriban Wapalestina milioni 1.2 mjini Gaza wanakabiliwa na uhaba wa chakula, kati yao watoto 785,000 wakinyimwa chakula bora, huku takriban watoto 70,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali. Alidokeza kuwa tangu kufungwa kwa vivuko hivyo, visa 8,923 vya utapiamlo miongoni mwa watoto vimerekodiwa, wakiwemo zaidi ya elfu moja wanaokabiliwa na utapiamlo unaotishia maisha. Ameona ipo fursa ya kweli ya kuwaokoa watoto walioathiriwa na utapiamlo, mradi tu vivuko vifunguliwe na kuletwa maziwa ya tiba na vifaa vya matibabu, huku akisisitiza kuwa wahudumu wa afya wa Gaza wana uwezo wa kutoa matibabu, lakini wananyimwa vitendea kazi. Alieleza masikitiko yake akisema: “Maziwa haya yasipoingia, hatima ni kifo,” akishikilia kuwa uvamizi huo unawajibika kwa vifo hivyo, hasa kwa kuwa unawanyima maziwa kwa makusudi kama njia ya kuwaua polepole. Alifahamisha kuwa uvamizi huo hautosheki na kuzuia chakula, bali pia unawalenga raia wanaojaribu kupata misaada, akitoa mfano wa mauaji ya daktari mmoja wakati alipokuwa akijaribu kuwaletea chakula watoto wake. Alionya kwamba Ukanda wa Gaza umeingia katika hatua ya kuwa "zaidi ya janga," ambapo watu wanazurura mitaani bila makazi, wakati watoto wanakufa mfululizo mikononi mwa mama zao, huku kukiwa na ukosefu usio wa kweli wa uwezo wa kimataifa.

Mkurugenzi wa Kituo cha Misaada ya Dharura ya Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Emory alisema kwamba picha zinazotoka Gaza zinaonyesha aina kali zaidi za utapiamlo, ikiwa ni pamoja na "kupoteza," ambayo inahusu kupungua kwa uzito kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na urefu, kutokana na kushuka kwa kasi kwa kalori kwa muda mfupi. Aliongeza kuwa ikiwa utapiamlo utarefushwa, itasababisha matokeo ya muda mrefu kama vile kudumaa kwa ukuaji, kupungua kwa uwezo wa kujifunza, kudhoofika kwa kinga ya mwili, na pia ukuaji wa utambuzi kwa watoto.

Wamagharibi, uvamizi, na vibaraka wao miongoni mwa tawala, watawala, taasisi, mashirika ya kimataifa, na jumuiya wanajaribu kuwaangamiza watu wa Gaza, kuwahamisha, na kuwanyenyekesha kwa mbinu na njia zote, ikiwemo baa hili la njaa ambalo wamelibuni wao na wale wanaoshirikiana nao katika nchi za Kiislamu na kwa hakika dunia nzima. Njaa hii haitokani na uhaba wa kimaumbile wa rasilimali, bali ni udhalili na usaliti wa watawala ambao waliweka utajiri wote wa Ummah mikononi mwa maadui zake ili kuudhibiti, bila kuwaruhusu hata kuwaruzuku watoto wa Gaza wenye njaa na kile ambacho kingewamudu. Wanawaacha wafe kwa njaa mbele ya macho yao bila kuhisi au kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakitekeleza amri za mabwana zao kuhifadhi viti vyao vya utawala, ambavyo vitaangamia hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Uokoaji wa watoto wa Gaza, wanawake wake, na watu wake, na ukombozi wa Palestina na ardhi nyengine za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu, utakuwa tu kwa kuwang’oa watawala hao waovu, wasaliti, wazembe, walaghai, na kumpa utawala Imam mwenye kujali ambaye atazikomboa ardhi na kuwaokoa waja kutokana na dhulma zao na kutokana na udhibiti wa Magharibi juu ya mali na rasilimali za Ummah. Hayo yatakuwa kwa kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu.

[إِن يَنصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aal-i-Imran:160]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizbuttahrir.today

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu