Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 29 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 092 |
| M. Jumatatu, 15 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Moto Mijini: Jinsi Ubepari Unavyowasha Moto katika Miji ya Waislamu yenye Wakaazi Wengi
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatatu, tarehe 1 Juni 2026, vyombo vya habari viliripoti kuhusu moto mkubwa ulioharibu eneo la makaazi lenye watu wengi huko Kebon Kosong, Kemayoran, Jakarta ya Kati, Indonesia. Takwimu rasmi kutoka kwa Wakala wa Kupunguza Maafa wa DKI Jakarta (BPBD) na uthibitishaji wa uwanjani zinaonyesha takriban familia 354—takriban watu 620—waliachwa bila makao. Takriban watoto 160 wenye umri wa kwenda shule waliathiriwa moja kwa moja.
Kitongoji hicho ni kitongoji duni kinachojulikana chenye nyumba za mbao, plywood, na mabati vya kudumu zipatazo 250–304. Mamia ya wakaazi hawa maskini wa mijini hawana vyeti vya umiliki wa ardhi (SHM); wanamiliki tu rekodi za vitambulisho vya kiidara pekee (KTP na kadi za familia) zilizosajiliwa katika eneo la kelurahan. Sio kutia chumvi kusema mamia ghafla wamekuwa bila makao usiku kucha. Wameishi kwa miongo kadhaa kama wakaazi wasio rasmi katika ardhi ya serikali inayosimamiwa na PPK Kemayoran, bila hati miliki halali.
Wako mbali na ustawi, wengi walihamia pamoja na familia zao na watoto wao hadi mji mkuu, lakini wakakwama katika kuzimu ya mijini—wakiishi kama wafanyikazi maskini wasio rasmi katika makaazi duni yanayokabiliwa na moto. Kwa mtazamo mpana zaidi, ni waathiriwa wa maendeleo mamboleo ya kiliberali ya mijini tangu miaka ya 1980: mtindo wa "globopolis" unaohusisha miji kuwatumikia kipote cha tabaka la juu wakibadilika kuwa kama injini ya ukuaji wa kiuchumi. Huku Jakarta ikifurika hadi kufikia watu milioni 11, imekuwa mji mkuu unaonyonya rasilimali unao kusanya mamilioni ya wahamiaji wa ndani. Kupungua kwa ardhi ya mijini—kuchukuliwa kwa ajili ya afisi, maduka makubwa, nyumba za kifahari, na viwanda—kumeongeza bei za ardhi na kusababisha jambo la "Kizazi cha Milenia cha Watu Wasio na Makaazi", ambapo vijana hawawezi kumudu nyumba.
Moto huu ni janga la kimfumo, matokeo ya mfumo wa kiuchumi uliofeli na mkakati wa maendeleo ya mijini uliofeli ambao unanyanyua pesa na riba juu ya mwongozo wa Quran. Upangaji uliovurugika wa mazingira, maendeleo ya vijijini na mijini yasiyo na usawa, na ukuaji wa miji usiozuilika umezidisha tatizo.
Maadamu miji ya Kiislamu itachukua mifumo ya maendeleo ya kiliberali ya kibepari ya kisekula, mamilioni jijini Jakarta, wakiwemo watoto wengi, wataendelea kuteseka katika kuzimu hii ya mijini—wakiathiriwa maradufu na umaskini wa vijijini na unyonyaji wa kiuchumi wa mijini unaosababishwa na kupuuza sheria za Mwenyezi Mungu katika mipango ya miji. Ni kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, dola ya usimamizi wa raia wake, inayotabikisha sheria za Kiislamu kwa ukamilifu wake, na kutawaliwa na Khalifa anayeelewa wajibu wake wa Kiislamu wa kutoa kiwango kizuri cha makaazi na maisha kwa watu wake na kuwalinda kutokana na aina zote za madhara na unyonyaji, ndipo watu wa Indonesia na kwengineko katika ardhi za Waislamu watakapoondolewa katika hali yao mbaya. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللّهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]
“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’idah: 50].
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizbuttahrir.today |



