Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  16 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: H.T.L 1443 / 16
M.  Jumatano, 15 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Na kwa Amos Hochstein Zinakuja Habari Halisi!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumanne, Juni 14, 2022, Gazeti la Al Joumhouria lilichapisha habari kwenye tovuti yake yenye kichwa "Hockstein atangaza: Jibu la Lebanon lasukuma mazungumzo mbele," ambacho ni dondoo ya mahojiano ya kipekee na mpatanishi wa Marekani katika faili ya kuweka mipaka ya mafuta ya baharini kati ya Lebanon na umbile la Kiyahudi, Amos Hochstein, na Chaneli ya Al-Hurra. Mahojiano hayo yanahusu suala nyeti linalohusiana na uondoaji wa gesi kutoka kwenye uwanja wa Karish, na umbile la Kiyahudi myakuzi wa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. Dondoo zilizochapishwa zinatosha kujua msimamo wa mamlaka fisadi na pande zake nchini Lebanon. Inajulikana kuwa Hochstein alitoa mapendekezo ya hapo awali katika ziara yake ya kwanza mnamo Machi 2022, ingawa mapendekezo haya hayakutangazwa wazi, lakini maneno ya Hochstein katika mahojiano haya yanaonyesha mapendekezo haya yalikuwa nini, na mamlaka ilikaa kimya kuyahusu kwa muda wote huu pamoja na umuhimu wa suala hili kutokana na uchaguzi.

Hochstein alibainisha, "Habari njema ni kwamba nimepata maafikiano zaidi juu ya ujumbe huo ... kwa hivyo nadhani ilikuwa ni jaribio kubwa la kuangalia machaguo tukisonga mbele, bila ya kupoteza uoni wa wazo ambalo tunapaswa kuridhiana na kufikiria kwa njia yenye manufaa."

Hochstein anazungumzia juu ya makubaliano gani?! Ikiwa Mstari wa 29 ni haki kwa Lebanon, je kuna yeyote nchini Lebanon aliye na hata haki ya kuiacha?! Na kama Mstari wa 29 sio haki kwa Lebanon, kama wanasiasa wafisadi wa Lebanon walivyoamua kwa pamoja sio kawaida! Lakini si chochote zaidi ya mstari wa mazungumzo, na barua iliyotumwa kwa Umoja wa Mataifa miaka 11 iliyopita inasema kwamba Lebanon ina haki ya 23, sio ya 29, kwa hiyo ni makubaliano gani mapya yaliyofanywa na Lebanon?! Je, ni katika Kitalu cha 8 kwa kubadilishana ahadi, udanganyifu na kauli mbiu katika uwanja wa Qana ambao haujathibitishwa kitaalamu kuwa na gesi mpaka sasa?! Hii ni ikiwa tutakubali kwa ajili ya hoja ambazo mistari hii, pamoja na idadi yake yote, inawakilisha ukweli uliothibitishwa, na sio zao la maslahi ya Marekani na umbile nyakuzi la Kiyahudi.

Alipoulizwa kama Lebanon ilijadili Mstari wa 29 naye, hasa kwa vile timu ya kiufundi na usambazaji ya jeshi la Lebanon ilisema kwamba ilikuwa ikitayarisha faili thabiti kuhusu Mstari wa 29, alisema: "Faili zenye nguvu zaidi ambazo upande wa Lebanon unapaswa kuandaa ni zile zinazoweza kufanikiwa, na suluhisho la mafanikio linahitaji kuachana na kufikiri. Je, nina kesi bora zaidi ya kisheria, je niko katika nafasi nzuri zaidi, je, nataka kuwa sahihi kwa sababu wakati mwingine unapokuwa sahihi, huwezi kuthibitisha hilo?” Aliendelea, "Kuna pande mbili hapa na katika pande zote mbili. Badala ya kuzingatia ipi ni haki yangu dhidi ya upande mwingine ambao anaona ni haki yake, ufikiriaji lazima uzingatie nishati ambayo inapaswa kutumika katika kufikiria, ni mawazo gani ya ubunifu ambayo tunaweza kukubaliana sote. Huenda nisipate kila kitu nilichotaka, lakini nimepata mengi zaidi ya niliyo nayo sasa, na kwa upande wa Lebanon, si chochote."

Ndiyo, ninyi watu wa Lebanon, kwa sababu mumefilisika - kulingana na huyu Hochstein – kuachana na kufikiria kuwa mstari wa 29 ni haki yenu. Suala si kwamba muko sahihi na munatetea haki yenu, bali munakaa kimya licha ya mbinu na tafiti zote zinazothibitisha kwamba mstari wa 29 ni upanuzi wa kimaumbile wa Lebanon! Na munapaswa kujua kama munavyosema: Hii ni haki yenu, kwani upande wa pili unaiona kama haki yake! Je, mumemsahau, Hochstein, yule ambaye kwamba kwa kweli munahusishwa naye ni adui mvamizi, anayenyakua? Ndio,  ndivyo alivyo, na ikiwa atakwamia kwa Marekani, Ulaya na dunia nzima, atabaki kuwa mnyakuzi, mvamizi katika nchi za Kiislamu zisizo na mipaka, isipokuwa ile iliyobuniwa na nyinyi na wale waliokutangulieni kutoka miongoni mwa wakoloni, au mvamizi mnayelitumikia jeshi lake, na anajaribu kulazimisha uwepo wake!

Labda ukweli pekee ambao Hochstein aliukusudia ni pale alipoulizwa kuhusu msimamo wake kuhusu wazo lililotolewa na mkuu wa Harakati Huru ya Kizalendo, Gebran Bassil, katika suala la kulazimisha kanuni ya "Karesh dhidi ya Qana", ambapo alisema: "... Sidhani kwamba jambo hilo limefungika na kauli mbiu tu," na akamalizia kwa kusema: "...najua ni vigumu kwa sababu watu wanapenda kauli mbiu, na hakuna shaka kwamba mambo ni magumu zaidi kuliko hayo!"

Katika hili, mnastahili kusikia maneno haya: Umesema ukweli lakini wewe ni muongo. Tabaka hili fisadi la kisiasa na pande zake halikuwa, na kamwe halitamiliki, isipokuwa kauli mbiu tupu na kiburi, lakini wakati wa ukweli, watauza na kukubali kushindwa kwa badali ya kukaa kwenye viti vibovu vya mamlaka yao, au kudumisha silaha ambayo ilitumiwa - Katika nyakati ngumu - dhidi ya watu wa Lebanon na Syria, lakini wakabakia kimya na hawatasema lolote kuhusu ubwana, mipaka na utajiri wa nchi na watu wake.

Enyi mamlaka fisadi, nyinyi mnaodai kutetea ardhi na ubwana: Karish, kama tulivyotaja hapo juu, amedondosha jani la mtini kutoka kwa kauli mbiu zenu zote, au zile zilizobakia, na mnaendelea kwa haraka katika mradi wa Marekani wa kupanga hali ya gesi ya eneo hilo na kukaza mshiko wake juu yake iwe ni silaha yenye kutumikia maslahi yake katika kanda hii na duniani, hasa katika mgogoro wa sasa wa gesi duniani, na huyu hapa mzee wenu Biden akikimbilia eneo hilo kupanga jambo hilo na harakati za utajiri huu mkubwa, kama walivyofanya watangulizi wake hapo awali.

Lakini tunawaambia nyinyi na mabwana zenu walio nyuma yenu: Choreni na mupange na leteni majukwaa na wachimbaji kutoka kila upande, kwani kwa kipindi kidogo tu mtakuwa na majuto, siku ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu atawapa ushindi wanaofanya kazi, hivyo wataiondoa mipaka ya udanganyifu mliyoipanda, na kuziunganisha nchi na waja chini ya kivuli cha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume itakayochukua fursa ya njama mlizopanga. Pia itachukua fursa ya mali ya Waislamu kama ilivyoamrishwa na Mola wake Mlezi, Mwenye nguvu na Mtukufu, Aliyeuweka utajiri huu katika ardhi na akawateua kama makhalifa ndani yake.

 (عَسَى رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ)

“Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi.” [Al-A’raf:129]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu