Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  10 Safar 1445 Na: H.T.L 1445 / 01
M.  Jumamosi, 26 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sauti Zinazounga Mkono Ushoga Zisingeongezeka Lau si kwa Ufisadi wa Mamlaka na Kutokuwepo kwake hata katika Utabikishaji wa Sheria Walizoanzisha!
(Imetafsiriwa)

Mamlaka ya kisiasa imetoweka, nguvu yake imefifia, na, pamoja na wabunge wake, walipuuza hata vifungu vya katiba walivyovipitisha, ambavyo vinakemea waziwazi na uchafu na ufuska. Waliwaacha watu kwenye hatima yao mbaya, hata katika kupata huduma msingi kama maji na umeme. Hata wale ambao walijitaja kama mawakala wa mabadiliko walijishughulisha na mambo madogo, wakitia saini rufaa ambayo inaonyesha uchafu, ufuska, na ukiukaji wa maumbile ya mwanadamu. Wengine walipatikana wakifuatilia filamu ya kipuuzi, wakidai kuwa hii ndio sura ya Lebanon wanayoitamani, badala ya dola yenye maadili mazuri au hata kwa chache, iliyo mbali na uzinzi.

Katika dhurufu hizi zisizo na uwajibikaji, haishangazi kwamba sehemu ya wafanyikazi wa vyombo vya habari na chaneli nchini Lebanon imeibuka kutetea ushoga, ujinsia, na utetezi wa wanawake, kwa uwongo wakidai kuwa mambo kama haya ni ya kimaumbile! Bila hisia yoyote ya aibu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

[قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَى كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَى“Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliye kipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa.” [Ta-Ha: 50] au mbele ya Waislamu wanaomuamini Yeye Subhanahu, na kukubali sheria zake na kufuata uongofu wake, kwa mujibu wa suluki zao njema.

Tumeonywa na Mwenyezi Mungu dhidi ya matendo ya kihadaifu ya Shetani na njia zake, ambapo ameeleza:

[لَّعَنَهُ اللَّهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا]

“Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako.” [An-Nisa: 118]. Mtume Muhammad (saw), pia amesema:

«إذا لم تستحْيِ فاصنَعْ ما شئتَ» “Ikiwa huoni haya, fanya unavyotaka.”

Kundi hili la wanahabari na wamiliki wa chaneli limethibitisha kuwa watu wasioaminika katika kutoa habari na kufichua ukweli kwa watu. Wamekuwa wapigiaji debe wa ufisadi, ni ufisadi ulioje huu! Upotosha wa kijinsia na kufungua milango ya uchafu katika aina zake mbaya zaidi, hata duni kuliko tabia ya wanyama. Hatuna maneno kwao isipokuwa maneno ya Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa yote ya Waja Wake:

[أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّهُ عَلَى عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَى سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَى بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّهِ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ]

“Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?” [Al-Jathiya: 23]. Na maneno yake (swt):

[أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا]

“Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia.” [Al-Furqan: 44].

Inajulikana sana kuwa fikra hizi zinaenezwa na mashirika ya kimataifa na viongozi wao, wanaoshikamana na mfumo fisadi wa kibepari ambao hushusha ubinadamu kwa kiwango chini ya wanyama, na kusababisha migogoro ndani ya jamii zao, kuvunjika kwa familia, kupungua viwango vya uzazi, na kuongezeka kwa kujiua, ubakaji, msongo wa mawazo, na watoto wa mahusiano haramu.

Inaonekana kana kwamba mashirika haya ya kimataifa na mabwana zao yamekuwa na wasiwasi juu ya umoja na mshikamano wa Waislamu na familia zao, pamoja na viwango vyao vya juu vya uzazi. Kwa miongo kadhaa, wamejaribu kusafirisha migogoro yao kwetu, wakidai wokovu katika mfano wao, ilhali sio chochote bali sumu na uharibifu.

Mashirika haya ya kimataifa na viongozi wao walipata mazingira mwanana ndani ya nchi yetu, sio miongoni mwa watu, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, bali miongoni mwa watawala vibaraka mafisadi na wanasiasa, haswa wale wa nchini Lebanon, ambao walifungua milango kwa taasisi hizi na vyama fisadi, zinazolenga kupenya katika akili za vijana wetu bila kizuizi.

Lakini, ni ishara nzuri kwamba watu wengi wanakataa fikra potovu na fahamu zenye sumu kama vile ujinsia, utetezi wa wanawake, na kadhalika. Waislamu wengine wamenyanyuka kukabiliana na shambulizi hili kwa kufichua uongo wake na kulaani vitendo vyake. Kwa watu hawa, tunapongeza juhudi zao na tunawashajiisha kufanya kazi zaidi katika kuzuia uenezaji wa mambo kama haya.

Ama kwa wale ambao wameinua vichwa vyao kuunga mkono ushoga kwa kukosekana kwa mamlaka, tunasema: mnapaswa kuwa na wasiwasi zaidi juu ya maswala yanayowakabili watu wa Lebanon, ambayo ni mazito na yanastahili umakini wenu, badala ya kufanya ushoga na utetezi wake kuwa ndio njia yenu! Kana kwamba watu wa Lebanon wamekosa maswala ya kuwashirikisha!

Sisi katika Hizb ut Tahrir, tunafanya kazi bila kuchoka kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya uongozi na tamkini Ardhini. Tunatangaza kwa wote kuwa tuko kwenye ukingo wa mfumo wa ulimwengu wa kiwahyi, mabadiliko kutoka kwa mfumo wa sasa fisadi. Chini ya Khilafah kwa njia ya Utume, Waislamu wataungana, ardhi zao zitaungana, Sharia (sheria ya Kiislamu) itasimamishwa, na ujumbe wa Uislamu utafikishwa kwa ulimwengu. Italinda rasilimali zao, kuwafurusha wavamizi na wakoloni, na kushughulikia matatizo tofauti tofauti ya watu. Wengine wanaweza kuliona hili kuwa liko mbali, lakini tulinaona kuwa karibu. Na hilo ni nini kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu.

[فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفاً فِطْرَتَ اللهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللهِ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru.” [Ar-Rum:30]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah L ebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu