Jumamosi, 04 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/05/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: H.T.L 1446 / 16
M.  Jumapili, 25 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kudumu kwa Mashirika ya Kifeministi na Mashoga hadi kufikia Hatua ya Kueneza Uchafu miongoni mwa Waumini ni Shambulizi la Dhahiri kwa Heshima ya Waislamu

(Imetafsiriwa)

Baada ya wasagaji wawili wanachama wa chama chenye uhusiano na Chuo Kikuu cha Marekani cha Beirut (AUBMC), chini ya kivuli na jina "Programu Oanishi ya Afya ya Jimai ya Wanawake (WISH) katika AUBMC," kutembelea shule ya upili ya wasichana jijini Tripoli, kwa uratibu wa Wizara ya Elimu; kisha kwa mbwembwe na bila aibu kuendekeza mambo machafu na kuonyesha picha na maudhui machafu kwa wanafunzi, wazazi wakasukumwa kuripoti tukio hilo kwa uongozi wa shule, ambao nao ulieleza kuwa wawili hao walikuja shuleni kwa amri ya Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu!

Bila ya maelezo zaidi wala kuzungumzia mambo mengi waliyoyafanya watu hawa katika suala la uchafu, na hata baada ya jitihada za pande zinazohusika katika suala hilo kukwepa na kutoa visingizio ambavyo ni vibaya zaidi kuliko uhalifu, tunazitaka pande zinazohusika zichukue hatua kali, nzito na za hadharani kuhusiana na jambo hilo, na pande hizi ni:

- Waziri Mkuu Nawaf Salam ambaye nafasi yake ya urais na serikali yake ni pamoja na Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu ikiwakilishwa na Waziri Rima Karami, alitakwa asimamishwe majukumu yake na aitwe kwa ajili ya uhakiki na uwajibikaji, hata kufikia hatua ya kufutwa kazi, endapo itathibitika kuna uhusiano wowote na wizara hiyo.

- Wizara ya Mambo ya Ndani ya Lebanon inapaswa kusimamisha shughuli za chama hiki na kuuita usimamizi wake na wafanyikazi wawili waliofanya kazi ya kueneza uasherati miongoni mwa wasichana wetu, bila aibu na bila hofu ya kuhisabiwa, kana kwamba walikuwa wamejificha nyuma ya kifuniko cha kisheria katika msingi wa chama hiki. Ni lazima, bali ni wajibu, kuwahisabu wale wanaotumia njia na mbinu za kueneza ufisadi.

- Idara ya Elimu ya Tripoli na Lebanon Kaskazini, ambako ndiko iliko shule hiyo husika, inaombwa kuchunguza tukio hilo, kupinga kitendo hiki kiovu, na kufafanua ni kwa haki gani mtu yeyote ana haki ya kuwa peke yake na wanafunzi. Kitendo chenyewe cha kuomba kuwa peke yake na wanafunzi kinaleta tashwishi na shaka.

- Chuo Kikuu cha Kimarekani cha Beirut, ambacho lazima kiite mamlaka husika inayosimamia vyama hivi kwa Idara ya Masuala ya Chuo Kikuu cha Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu, na kuchukua hatua zinazohitajika ikiwa uhusika wake katika suala hilo utathibitishwa.

- Dar Al-Fatwa kwa ujumla, na hasa Dar Al-Fatwa ya Tripoli, kuhakiki rasmi kilichotokea na kufungua madai ya kisheria pale inapobidi, kwa jina la kueneza uchafu na kutumia njia na mbinu zisizofaa.

- Hata kama jambo hili litafichuliwa katika shule husika, nani anajua kitakachofuata? Wengine wanaweza kuificha, iwe kwa nia njema au mbaya. Kwa hiyo, ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe ili kutokomeza vitendo hivi kabla havijatokea, badala ya kukwepa tu jambo hili baada ya kutokea na kujaribu kurekebisha kwa kuhofia uwajibikaji na hasira za wale walio na ghera na dini na heshima zao.

Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon, tunatahadharisha vikali dhidi ya matokeo ya kupuuza jambo hili. Tunatoa wito kwa familia, masheikh, walimu, na wale wote wanaopigana na watetezi wa LGBTQ na ufeministi kuchukua hatua madhubuti na kali. Hii isiwe tu kauli za ufafanuzi na kuomba radhi, bali hatua za utekelezaji wa umma dhidi ya vyama hivi na kuendelea kwake kufanya kazi na kuwepo. Baada ya tawala za awali za Marekani kusafirisha vyama hivi hadi nchi yetu, utawala wa sasa ulivitenga na kuanza kuzuia shughuli zao. Hata hivyo, bidhaa za kifisadi walizouza nje zinaendelea kuenea kama saratani mbaya katika nchi yetu. Kwa hiyo, mamlaka husika hazina budi kuchukua hatua kali dhidi ya waliofanya kitendo hiki kiovu na dhidi ya waanzilishi wa vyama hivyo viovu.

[قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَاناً وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ]

Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua. [Al-A’raf 7:33]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu