Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 7 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: 1446/35 |
M. Jumanne, 03 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuna Uungwana kutoka Ng'ambo ya Bahari... Uko wapi Uungwana wa Jeshi la Misri?!
(Imetafsiriwa)
Katika wakati ambapo mauaji dhidi ya watu wa Gaza yamezidi, na ardhi kuungua chini ya miguu ya wanyonge, vyombo vya habari vya Marekani vimeandika kichwa cha kikuu habari kuhusu kijana Muislamu kutoka Misri aitwaye Mohammed Sabry Soliman, ambaye alituhumiwa kwa kurusha vinywaji vya Molotov kwenye maandamano ya kuunga mkono umbile la Kiyahudi nchini Amerika, akiimba "Uhuru kwa Palestina." Wakati vyombo vya habari vinajadili tukio hili, kiini cha tukio hili hakiwezi kupuuzwa: kijana Muislamu, aliyehama kutoka ng'ambo ya bahari, akisukumwa na maumivu ya moyo wake na maumivu ya Ummah wake, kueleza kukataa kwake kimya cha kimataifa na kufeli kwa Waarabu kushughulikia hali inayoendelea mjini Gaza.
Tukio hili si tu kitendo cha mtu binafsi; ni kilio cha uungwana, kinachofichua hali ya Umma ambayo haijampata yeyote miongoni mwa majeshi na watawala wake kuchukua hatua ya kuwanusuru wanaodhulumiwa. Alichokifanya kijana huyu kinawakilisha hasira huru kutoka moyoni mwa Muislamu ambaye itikadi na utu wake vinakataa kuwaona watu wake wakiangamizwa huku yeye akiwa amesimama kimya.
Wakati huo huo, misimamo ya tawala za Kiarabu, zinazoongozwa na utawala wa Misri, inafichuliwa. Wanaendelea kushindwa, wakishiriki katika kuzingirwa kwa Gaza kwa kufunga vivuko na kuzuia usambazaji mahitaji, na hata kusukuma gesi kwa Mayahudi na kuratibu pamoja nao katika masuala ya usalama na kisiasa. Usaliti huo umevuka nyanja ya kisiasa na kujumuisha uhamasishaji wa kidini na vyombo vya habari, kwani wanazuoni wa serikali wamehamasishwa kuhalalisha kimya hiki na kupotosha ufahamu wa watu, katika jaribio la kugeuza mzozo huo kuwa suala la "kibinadamu" lisilohusiana na ukombozi na jihad.
Hapa swali la msingi linaibuka: Jeshi la Misri liko wapi? Wako wapi wale wanaoimba kuhusu utukufu wa Oktoba na kujivunia historia yao ya ushujaa? Je, hakuna mwanamume mwenye hisia miongoni mwao anayeweza kuona watoto na wanawake wa Gaza wakichinjwa na maeneo yake matakatifu yakipigwa mabomu? Je, hawaoni jinai za kila siku zinazofanywa na Mayahudi wahalifu? Au wameuliwa hisia zao na amri za kisiasa, na wakawa walinzi wa mipaka ya wakoloni badala ya walinzi wa Ummah?
Utawala wa Misri ni mlinzi wa usalama wa Kiyahudi, unaowanyima misaada watu wa Gaza, kuwafungia vivuko, kuendesha vita vya vyombo vya habari na vya kisiasa ili kuwapotosha wanaowatetea, na kuwatuhumu wapiganaji wa upinzani kwa ugaidi!
Hata wanavyuoni wanaodaiwa kuwa warithi wa mitume walipotea katikati ya uoga na ulafi. Wengine walikaa kimya, huku wengine wakiegemea upande wa mtawala, wakihalalisha udhalilifu wao kwa uhalisia na kuulaza Ummah kwa kisingizio cha “faqhi ya maslahi” na “busara,” na kusahau kwamba jihad ni faradhi na kwamba kusema ukweli kwa dhalimu ni jukumu lisiloweza kuakhirishwa.
Enyi watu wa Misri (Kinanah), Enyi wana wa Salahuddin na Qutuz, je, haujafika wakati wenu kuukataa uhalisia huu?! Je, si wakati wenu wa kusema imetosha kwa utawala unaosaliti Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa jina lenu? Je, si jambo la aibu kwamba historia inaandika kwamba Misri ilikuwa kwenye mipaka ya Gaza na haikusonga kwa ajili ya nusrah (msaada) yake?!
Alichofanya Mohammed Sabry Soliman kinaonyesha kwamba bado kuna wale ndani ya Umma ambao hisia zao ziko hai. Hata hivyo, hatari halisi iko katika ukweli kwamba uungwana wa Ummah unabakia kwa watu binafsi, wakati Ummah na majeshi yake yakikaa kimya, utashi wao unapooza. Hili ndilo linalorefusha uvamizi na kuendeleza udhalilifu wa Ummah.
Maafisa na askari katika Jeshi la Kinana: Nyinyi ndio watoaji uamuzi halisi. Vivuko viko mikononi mwenu, mipaka iko chini ya miguu yenu, na vilio vya Gaza vinakufikieni. Mna udhuru gani wa kukaa kimya? Msidanganywe na amri za kisiasa, na msidanganywe na maneno ya vyombo vya habari. Mnawajibika kwa Mwenyezi Mungu, sio kwa viongozi wenu. Je, hamuogopi kwamba mtaulizwa Siku ya Kiyama kuhusu damu ya watoto? Kuhusu kuzingirwa kwa kina mama? Kuhusu misikiti kupigwa mabomu mukiwa jirani?
Hatuitishi ghasia au uasi wa kiupofu. Bali sisi tunakuiteni kwenye yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu (swt): kuwa maanswari wa Dini yake, kusimama pamoja na Ummah wenu, sio dhidi yake, kutumia silaha zenu kuwasaidia wanaodhulumiwa, na sio kuwalinda wasaliti, na kufanya kama walivyofanya Answar pamoja kwa Mtume (saw) walipomwambia: "Lau utatuvusha bahari, tutavuka pamoja nawe."
Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, ndio suluhisho msingi. Itaunganisha nguvu za Ummah, itaelekeza uungwana wake kwenye mradi wa ukombozi, itavunja nguvu ya uvamizi, itamaliza ulaji njama na maadui wa Ummah, na kuuregesha kuwa umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu.
Ewe Mwenyezi Mungu, kuna watu wenye ikhlasi katika jeshi la Kinana. Kwa hiyo, zisukume nyoyo zao, ukomboe utashi wao, wape heshima ya ushindi, na uwaegemeze na wale ambao hawadhuriki na usaliti wa wasaliti.
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na Watoto” [An-Nisa: 75]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |