Jumanne, 13 Shawwal 1447 | 2026/03/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  7 Shawwal 1447 Na: 1447/34
M.  Jumatano, 25 Machi 2026

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kati ya Magereza ya Wahubiri na Bandari za Silaha…Je, ni Upi Msingi wa Hukumu wa Utawala Huu?

(Imetafsiriwa)

Huku magereza na vituo vya uzuizini vikiwa wazi kwa wabebaji wa Dawah wanaotaka utabikishwaji wa Uislamu, na huku wakiteswa kwa ajili ya riziki zao, wakinyamazishwa, na fikra zao zikikandamizwa—si kwa uhalifu wowote walioufanya, wala uchokozi wowote walioufanya, bali kwa sababu tu wanasema kwamba Uislamu lazima utabikishwe maishani, na kwamba Ummah lazima utawaliwe na sheria ya Mola wake Mlezi—wakati huo huo, bandari zinafunguliwa, barabara zinarahisishwa, na huduma zote zinatolewa kwa kila kitu kinachowatumikia maadui wa Ummah na kuimarisha nguvu zao!

Ni aina gani ya kitendawili hiki kinachofanya ulinganizi wa Uislamu kuwa uhalifu, huku kuwezesha kile kinachowafikia maadui wake kuwa kitendo kinachokubalika au hata kinachovumiliwa?! Na ni aina gani ya kipimo hiki kinachofanya neno la haki kuwa kosa la jinai, huku kikifumbia macho vitendo vinavyopelekea kuwaimarisha wale wanaowaua Waislamu na kuikalia kimabavu ardhi yao!?

Kukamatwa, kuteswa, na unyanyasaji unaowakabili wabebaji wa Dawah wanaolingania Uislamu si matukio ya kipekee, bali ni mbinu thabiti inayoakisi asili ya serikali iliyopo. Serikali hii inauona Uislamu kama mfumo wa utawala kama tishio na inatafuta kuutokomeza. Kinyume chake, serikali hii haina wasiwasi wowote kuhusu kufanya kazi kama chombo ndani ya mfumo wa kimataifa unaotumia rasilimali kuhudumia umbile la Kiyahudi kupitia uratibu wa kisiasa, ushirikiano wa usalama, na hata uwezeshaji wa kilojistiki, ikiwemo kupitisha nyenzo zinazotumika katika sekta zake za kijeshi.

Kisa cha meli ya MSC DANIT kinatumika kama kielelezo dhahiri cha uhalisia huu wa aibu. Meli hiyo, inayoripotiwa kubeba shehena za chuma zinazopelekwa kwa makampuni ya kijeshi katika umbile la Kiyahudi, ni sehemu ya silsila ya usambazaji inayotumika katika utengenezaji wa zana za kivita na silaha. Hii ina maana kwamba kurahisisha kupita kwake au kuipokea inajumuisha usaidizi kwa silsila hizi na sekta hii, ambayo huachilia moto wake kwenye vifua vya Waislamu nchini Palestina, Lebanon, Syria, na Iran. Hii inaonyesha kwamba jambo hilo si shehena ya kibiashara tu, bali ni kazi inayofanywa na serikali ili kulinda hali halisi iliyowekwa na umbile la Kiyahudi.

Enyi Watu wa Misri – Kinanah: Nyinyi ambao mliobeba Uislamu kwa karne nyingi, na mumekuwa ngome na nusra yake, kinachotokea sio msururu wa matukio ya kipekee, bali ni uhalisia kamili unaohitaji uelewa wa kina. Tatizo haliko katika uamuzi hapa au utaratibu pale, bali katika mfumo unaokutawaleni, na katika msingi ambao unaegemea. Mabadiliko ya kweli hayatakuja kupitia kutia viraka mambo, wala kupitia hasira tu, bali kupitia kutambua kwamba Uislamu sio matambiko tu, bali ni mfumo kamili wa maisha ambao lazima utabikishwe na kuwa msingi pekee wa utawala, siasa, uchumi, na nyanja zengine zote za maisha. Fahamuni ukweli huu, na musidanganyike na kaulimbiu za uongo za serikali. Jueni kwamba kuelewa ukweli huu ni hatua ya kwanza kuelekea mabadiliko ya kweli.

Enyi Askari wa Misri – Kinanah: Nyinyi ni watu wenye nguvu na ulinzi, na Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu nguvu hizi: zilitumikaje, na zilielekezwa dhidi ya nani? Wajibu wenu si kulinda uhalisia unaogongana na imani yenu, wala kulinda maslahi ya wale wanaouchukia Umma wenu, bali ni kuinusuru Dini yenu, kusimama na Umma wenu, na kuzuia dhulma isiupate.

Tunachoshuhudia leo, ikiwemo tukio la meli hii, ni uthibitisho zaidi kwamba uhalisia huu hauwezi kurekebishwa kutoka ndani. Inahitaji mabadiliko makubwa ambayo yataregesha utulivu na kuuweka Uislamu kama dola inayotawala, chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’idah: 50]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu