Hakuna Wokovu kwa Watu wetu nchini Sudan Wala Amani au Usalama isipokuwa chini ya Mfumo wa Uislamu
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika yote historia, wingi wa makabila nchini Sudan kamwe haukuwa sababu ya mizozo na vita. Bali, kilichosababisha haya ni mapambano makali ya kisiasa na kijeshi baina ya dola za kikoloni na vibaraka wao, ambayo yaliharibu mazao na vizazi, hasa baada ya wao kuigawanya nchi na kupanda mbegu za fitina na mapigano ya kikabila na kimapendeleo, sawa kabisa na yale yanayotokea leo na kwa usahihi kabisa kama ilivyotokea katika siku za mwanzo za Ujahiliya.



