Katika wakati ambapo sura za mauaji yanayofanywa na Mayahudi mjini Gaza zikiongezeka, na chakula, dawa, na maji vikizuiliwa kwa watoto, wanawake na wanaume, Al-Azhar ilitoa tamko la kulaani "jinai ya kuweka njaa" inayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi. Taarifa hiyo ilifutwa baadaye! Basi je, inajuzu kilio dhidi ya dhalimu kifutwe?! Na je, sauti ya wanazuoni inaweza kukaa kimya dhidi ya mauaji?! Taarifa hiyo ilikuja ikiwa imejaa misamiati ya kibinadamu, yenye kuwavutia watu wenye dhamiri hai, jumuiya ya kimataifa, na dola zenye ushawishi, na kutoa wito wa kufunguliwa kwa vivuko na utoaji wa misaada. Umbile la Kiyahudi lilielezewa kuwa linafanya uhalifu wa njaa, likituhumiwa kwa mauaji ya halaiki na kuzuia misaada, na ilitoa wito kwa mashirika ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kusonga mbele kufungua vivuko, pamoja na kuwaombea dua watu wa Gaza kwamba Mwenyezi Mungu awanusuru na alipize kisasi kwa ajili yao.