Risasi Zimechukua Maisha ya Watu … Na Serikali Zinacheza Densi Juu ya Majeraha!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa mujibu wa mashirika ya habari; mtoto wa miezi 8 Laila Al-Ghandour alifariki mnamo Jumanne asubuhi eneo la Mashariki mwa Gaza baada ya kuvuta gesi. Tukio hili linaongeza idadi ya mashuhadaa wa “Msafara wa Mkubwa wa Maregeo” na kufikia idadi ya 61, wakiwemo watoto 7 na majeruhi 2,800, wengi wao wakiwa ni kutokana na risasi na wengine wakiwa ni kutokana na vipande vya mabomu na gesi ya sumu wakati wa uzimaji msafara na majeshi ya umbile la Kiyahudi iliyoanza maeneo tofauti Mashariki mwa ukanda wa Gaza katika kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba, na ambayo ilipinga na kukataa kuhamishwa kwa ubalozi wa Amerika jijini Al-Quds (Jerusalem).



