Nidhamu ya Uislamu
- Imepeperushwa katika Vitabu
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kitabu cha Nidhamu ya Uislamu
Kitabu cha Nidhamu ya Uislamu
Mnamo 18 Julai, katika mji wa St.Petersburg, mwanamke wa Kiislamu Jannat Bespalova (Alla Bespalova) alipatikana na hatia kwa kushiriki shughuli za Hizb ut Tahrir kutokana na kukiri kwa Bespalova juu ya mashataka hayo dhidi yake na kunyimwa haki ya kupinga uamuzi huo na mahakama haikuutilia maanani ushahidi wake na badala yake kumfunga kifungo cha miaka mitano gerezani.
Katika ugandamizaji wao wa nguvu kwa ulinganizi wa kisiasa wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, watawala wa Pakistan wametupilia mbali hadhi kuu ambayo Uislamu umeipatia heshima ya mwanamke wa Kiislamu.
Saa za mapema mnamo 30 Julai 2018 wafanyikazi kutoka idara ya ujasusi ilimteka nyara Dada Romana Hussain, mwalimu wa Kiislamu mwenye kuheshimika na mama wa watoto wanne.
Tunisia hivi sasa imo katika kipindi kigumu baada ya wale tuliowafikiria kuwa ni watawala kuyatelekeza majukumu yao msingi na kuziwachia dola za msalaba za kikoloni na wafanyikazi wake ndani ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa kuamua sera za kiuchumi, kifedha na kijamii mpaka nchi ikadhibiti usambaratikaji wa kiuchumi licha ya kwamba kulikuwa na madeni makubwa.
Tawala za ukandamizaji na udhalimu hususan utawala wa kihalifu na ukandamizaji wa Ash-Sham, umekuwa ukiwapokonya Ummah maamuzi yao, ukiyakosea heshima matukufu yao, na kuwafuatilia kinyama kupitia taasisi za ujasusi ili kuwatia hofu kiasi kwamba watu wameshindwa mpaka kuzungumza na ndugu zao kuhusu masuala ya ummah.
Ni wazi kwa kila muangalizi asiye na mapendeleo kuwa mvutano pekee wa kimfumo unao endelea kwa sasa katika ngazi ya kiulimwengu ni baina ya Uislamu na Urasilimali na itikadi yake ya kisekula.
Kutokana na maafa yanayo tekelezwa na serikali ya kihalifu ya Urusi dhidi ya Waislamu wa Urusi, leo, mamia ya Waislamu wanafungwa katika magereza ya Urusi kwa sababu ya kushiriki kwao katika kazi ya Hizb ut Tahrir. Walituhumiwa “ugaidi” kirongo kwa kutegemea uamuzi wa kufedhehesha wa Mahakama ya Upeo wa kuiorodhesha Hizb ut Tahrir kama shirika la kigaidi. Kwa mujibu wa uamuzi huu wa kiajabu, Chama hiki cha Kisiasa cha Kiislamu, kikawa chama cha “kigaidi”.
Watawala waovu wa Pakistan wanaendelea kuwalazimisha vibaraka wa Amerika nchini Pakistan na kuwalazimisha juu ya shingo za Waislamu, hususan wanachama na wafuasi wa Hizb ut Tahrir, sasa imechukua hatua kakamavu zaidi katika mbinu zao ovu kuteka nyara wanawake!
Pamoja na masomo juu ya zana za vita, mikakati na mbinu, utafutaji wa shahada ulitizamwa kama msingi wa fahamu za masomo, uelewaji na ujengaji wa nafsiyya. Utafutaji wa shahada ndio uliotia nishati majeshi ya Kiislamu katika vita, ukiwawezesha kufikia yale ambayo wengine walishindwa kuyafikia na wasingejaribu kuyafikia.