Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 13 Shawwal 1442 | Na: 1442 / 77 |
M. Jumanne, 25 Mei 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa Kuifungulia Anga na Bahari Amerika, Serikali ya Bajwa-Imran Yatekeleza Dori ya Mwajiriwa wa Kati na Kati wa Kusahilisha Maslahi ya Amerika Nchini Afghanistan
(Imetafsiriwa)
Waislamu wa Pakistan na vikosi vyao vya kijeshi wanapinga dori ya serikali ya Bajwa-Imran ya kuwa mwajiriwa mwenye kusahilishia jeshi la Amerika nchini Afghanistan, pamoja na idhini yake kuifungulia Amerika anga na bahari ili kuweza kusaidia uwepo wake wa kimsalaba nchini Afghanistan. Usaliti wa utawala wa Bajwa-Imran unakinzana na msimamo msingi wa wapiganaji wa kikabila wa Afghanistan, ambao walikizika kiburi cha jeshi la Amerika chini ya milima, kupitia nguvu zao za kiroho, ambazo zilifidia uchache wa nguvu zao za kimada. Kwa kushindwa kumaliza upinzani wa Waislamu kwa askari wake waoga, Amerika sasa inatumia mawakala wake katika uongozi wa jeshi la Pakistan kudhibiti Afghanistan. Amerika inahitaji sana msaada kwa kambi za kijeshi katika nchi za eneo hilo, vituo vikubwa vya kijasusi vinavyojifanya kama balozi jijini Kabul na Islamabad na kunaswa kwa upinzani wa Afghanistan ndani ya sokomoko la mradi wa kisekula wa kidemokrasia kupitia mikataba ya kugawanya mamlaka. Kwa njia hii, utekelezaji kamili wa Shariah utabaki kuwa ndoto tu, huku utawala wa kieneo wa Amerika utaendelea. Hivyo basi, Amerika inawategemea wasaliti ndani ya uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan kutenda kama wawezeshaji walioajiriwa kwa mkoloni wa Amerika Raj katika eneo hilo. Kauli ya Waziri wa Kigeni wa Pakistani juu ya "Ushirikiano Mpana wa Kimkakati" na mkutano wa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Pakistan pamoja na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Amerika zote ni viungo katika silisili hiyo hiyo mmoja ya utumwa kwa Amerika.
Ruwaza ya Uislamu ya kieneo yako wazi. Vizazi vya Abdali na Ghauri ndani ya Jeshi la Pakistan lazima waunge mkono upinzani wa Afghanistan dhidi ya Waamarika wanaokimbia. Lazima wautokomeze Msitari wa Durand uliochorwa na Waingereza ili kuziunganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati kupitia ruwaza ya kisiasa ya Khilafah. Ruwaza hii ya kivitendo itakidhi mahitaji ya usalama wa chakula ya eneo zima kupitia uwezo wa uzalishaji wa kilimo wa Pakistan, na pia mahitaji ya nishati ya eneo hili kupitia akiba ya hydrocarbon ya Bahari ya Caspian ya Asia ya Kati. Uislamu pekee ndio unaotoa ruwaza ya kimkakati ya kijiografia ya kiuchumi ambayo italeta uhuru wa kweli wa eneo hili kutoka kwa Mkoloni Magharibi. Khilafah ndiyo ambayo itauzinganisha kwa haraka nchi zingine zote za Kiislamu, kwa hivyo Khilafah itakuwa ndio dola inayoongoza ulimwenguni kama ilivyokuwa kwa karne nyingi nyuma.
Enyi Wanajeshi ya Pakistan! Ni wazi kabisa kwamba uongozi wenu wa sasa umepuuza heshima ya Mtume (saw), ukiuwa upande wa makruseda makafiri. Haikuinua hata kidole kukomesha shambulizi la aibu la Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na Waislamu wa Palestina, wakati mulikuwa mnatamani ukombozi wa Qibla cha Kwanza, mukiwa tayari kujitolea mhanga kila kitu kwa ajili yake. Ni uongozi wa sasa ndio ambao umewatelekeza kaka na dada zenu huko Kashmir mbele ya mnyanyasaji wa Kibaniani, ilhali muna uwezo wa kuwashinda Mabaniani hao waoga, mukhtasari ambao mumeuonyesha mnamo Februari 27, 2019. Sasa ni uongozi huu ndio unaoiwezesha Amerika kubakia kama nyoka kwenye nyasi, licha ya kuwa muna uwezo wa kuhakikisha kuwa inalikimbia eneo hili. Ung'oeni uongozi ambao unasimama na maadui wa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na Ummah. Toeni Nusra kwa Hizb ut Tahrir ili murudishe tena mwendo ya ufunguzi ambao ulikatika kwa kuvunjwa Khilafah Uthmani. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
]فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ]
“Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea” [Surah Aali-Imran 3: 159].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/pakistan/1606.html#sigProId261285174e
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |