Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  28 Rabi' I 1438 Na: 16073
M.  Jumanne, 27 Disemba 2016

Waacheni Huru Watetezi wa Khilafah:

Haki inadai Kuachiliwa Huru Mara Moja kwa Wale Wanaolingania Khilafah kwa Njia ya Utume.

 (Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 24 Disemba 2016, Jaji Mkuu Mteule wa Mahakama ya Upeo, Mian Saqib Nisar, alisema, “Ninaahidi hakutakuwa na shinikizo kwa idara ya mahakama na hakuna anayeweza kuthubutu kuhoji uwazi wetu. Siwezi kuutoa muhanga uhai wangu kesho Akhera kwa manufaa yoyote ya kidunia.” Hakika hakimu aliyeongoka ni yule anayehukumu kwa Uislamu ili apate Jannah. Na ole wake yule anayehukumu kwa yasiokuwa Uislamu! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«الْقُضَاةُ ثَلَاثَةٌ: وَاحِدٌ فِي الْجَنَّةِ، وَاثْنَانِ فِي النَّارِ، فَأَمَّا الَّذِي فِي الْجَنَّةِ فَرَجُلٌ عَرَفَ الْحَقَّ فَقَضَى بِهِ، وَرَجُلٌ عَرَفَ الْحَقَّ فَجَارَ فِي الْحُكْمِ، فَهُوَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ قَضَى لِلنَّاسِ عَلَى جَهْلٍ فَهُوَ فِي النَّارِ»

“Makadhi ni aina tatu: mmoja yuko Peponi, na wawili wako Motoni, ama yule aliye Peponi ni mtu aliyeijua haki na akahukumu kwayo, na mtu aliyeijua haki kisha akaivuka hukmu hiyo, huyo yuko Motoni, na mtu aliyewahukumu watu kwa ujinga, huyo yuko Motoni.” [Abu Dawud].

Cha kusikitisha ni kwamba, katika nchi iliyoasisiwa kwa jina la Uislamu ambayo watu wake watukufu wanatamani kujitolea mhanga kwa ajili ya akhera, Waislamu kwa jumla, na hasa watetezi wa Khilafah wamekumbwa na dhulma kubwa. Waislamu wengi wanaopigania Uislamu wamepata mateso makali, ikiwemo kunyimwa usingizi, kupigwa bila huruma, kulazimishwa kutumia dawa za kubadili akili na kupigwa shoti ya umeme. Baadhi ya watetezi wa Khilafah wamefungwa kwa muda mrefu bila kuhukumiwa, wakiwemo wale waliokamatwa tarehe 5 Disemba 2014, zaidi ya miaka miwili iliyopita. Na wengine wametekwa nyara, akiwemo Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, ambaye ametoweka kwa zaidi ya miaka minne na nusu, tangu kutekwa nyara kwake tarehe 11 Mei 2012 na asasi za serikali. Kwa hiyo, inatarajiwa kwamba Jaji Mkuu mteule na mahakimu wengine wawe wakweli kwa nia zao njema na wawakomboe Waislamu wote wanaopigania Uislamu, bila ya kusita, wasimwogope yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt).

Dhulma kubwa dhidi ya Waislamu wanaopigania ubwana wa Uislamu inafanyika ingawa utabikishaji wa Uislamu ni Wajibu, kwani Mwenyezi Mungu (swt) amesema.

 [وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Maida 5:45]. Udhalimu huu unafanyika ijapokuwa utetezi wa Khilafah ni harakati tukufu, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alibashiri kurudi kwake, kuwa ndio sababu ya kukomesha dhulma.

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“Kisha itakuwepo utawala wa kiimla, utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (Mtume) (saw) akanyamaza.” [Ahmed].

Na dhulma hii kubwa inafanyika huku wahalifu wa kweli wakiwa huru, yaani, watawala wa sasa wanaotawala kwa ukafiri na kushirikiana na wakoloni, kupora na kufuja mbele ya macho ya wazi, na kuifanyia mahakama. Watawala hawa wafisadi wanategemea kusalia kwao shinikizo kwa taasisi zote za Pakistan kutoka kwa mabwana zao huko Washington, ambao wanatafuta kuwafurahisha mchana na usiku, licha ya maafa yote yanayoikumba Pakistan kama matokeo. Hakika, ni shinikizo hili hili ndilo linalohakikisha kwamba wale wanaofanya kazi ya kusimamisha tena Uislamu kama dola, ambayo Washington inaihofia zaidi ya chochote chengine, wanatekwa nyara au kufungwa.

Enyi Mahakimu Wanyofu wa Mahakama! Ni wazi kutokana na uingiliaji kati wa Jenerali Raheel ili kukimbia kutokana haki ya Jenerali Musharraf mnamo Machi 2016, kwamba uwezo wa kupunguza shinikizo kwa mahakama upo mikononi mwa taasisi yenye nguvu zaidi ya Pakistan, vikosi vya jeshi. Zaidi ya hayo, ikiwa mahakama itaendelea na mfumo wa sasa, chini ya watawala wa sasa, haiwezi kamwe kutarajiwa kusimamisha haki kwa mujibu wa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Hivyo basi, ni juu yenu nyote kutumia ushawishi wenu mkubwa kuwataka maafisa wanyofu wa majeshi yetu kuipa Nussrah (Msaada wa Nyenzo) Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kuregesha mara moja Khilafah kwa Njia ya Utume. Hapo ndipo tutakapoona uadilifu wa kweli ambao sote tunautamani kama Waislamu. Hatimaye, tutaona mahakama iliyoongoka ipasavyo ambayo itawahukumu watawala wa sasa kwa ajili ya ukiukaji wao mwingi wa Uislamu, ambao kwao adhabu kali inawangoja mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[ وَلاَ تَحْسَبَنَّ ٱللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ ٱلظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ ٱلأَبْصَارُ * مُهْطِعِينَ مُقْنِعِى رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَآءٌ]

Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.* Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu.” [Ibrahim: 42-43]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu