Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  26 Jumada II 1437 Na: PR16018
M.  Jumatatu, 04 Aprili 2016

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Komesha Utesaji wa Hizb ut Tahrir

Mwacheni Huru Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah, Aliyetekwa Nyara mnamo 11 Mei 2012, kwa Ajili ya Kupaza Sauti Yake dhidi ya Madhalimu

(Imetafsiriwa)

Kama sehemu ya mfululizo unaoangazia watu wa Hizb ut Tahrir wanaoteswa na serikali, tunawasilisha kesi ya Naveed Butt.

Naveed Butt sasa ana umri wa miaka 47, ni mhandisi na ameoa na ana watoto wanne. Alitekwa nyara mnamo tarehe 11 Mei 2012 na vyombo vya usalama na anaendelea kutekwa nyara karibu miaka minne baadaye.

Naveed Butt anatoka katika familia maarufu na inayoheshimika sana ya Kashmir inayoishi huko Islamabad. Alijishindia nafasi katika Chuo Kikuu cha Uhandisi cha kifahari huko Lahore na kutokana na maendeleo yake bora aliweza kuhamia Chuo Kikuu cha Illinois huko Chicago, Marekani ili kuhitimu. Alifanya kazi Motorola kama mhandisi anayelipwa vizuri kabla ya kuamua kuregea Pakistan kufuatilia kazi ya kuregesha Khilafah katika ardhi za Waislamu.

Naveed Butt ni Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir. Ameandika mamia ya taarifa kwa vyombo vya habari zilizofichua utumwa wa watawala kwa Amerika na khiana zao kwa Uislamu na Waislamu. Amesafiri kwa urefu na upana wa Pakistan akiwahutubia watu kuhusiana na Khilafah na wajibu wake kutoka kwa Uislamu na muundo wake wa kina.

Naveed Butt alitekwa nyara kwa sababu alikuwa mmoja wa wakosoaji mashuhuri wa utawala wa Pakistan. Kutekwa nyara kwake kulifuatia kampeni ya nguvu ya uwajibikaji dhidi ya utawala wa Pakistan kwa utiifu wake kwa Amerika, baada ya kuachiliwa kwa jasusi wa Marekani, Raymond Davis, na shambulizi la Abbottabad na vikosi vya kijeshi vya Marekani. Naveed aliongoza kampeni ya Hizb ut Tahrir akiwa mbele, akikosoa vikali ushirikiano wa wasaliti katika uongozi wa kiraia na kijeshi wa Pakistan na Amerika.

Wakati ambapo watawala wa sasa wa Pakistan wanafuata nyayo za madhalimu wa Kiquraish kwa kutawala kwa mabavu na hofu, watetezi wa Khilafah kama Naveed Butt ni chanzo cha msukumo kwa Waislamu wanaoamini maneno ya Mtume wao:

«أَفْضَلَ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ»

"Jihad bora ni neno la haki mbele ya kiongozi jeuri.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu