Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  18 Rabi' I 1436 Na: PR15002
M.  Ijumaa, 09 Januari 2015

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kampeni Mwacheni Huru Naveed Butt
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan Yatoa Makala ya Naveed Butt:
"Jinsi Amerika Ilivyofanikiwa Kuwasha Moto katika Pembe Tofauti Tofauti za Pakistan"

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan imetoa makala yaliyoandikwa na msemaji wake nchini Pakistan, Naveed Butt, yenye kichwa, "Jinsi Amerika Ilivyofanikiwa Kuwasha Moto Katika Pembe Tofauti Tofauti za Pakistan". Utawala wa Raheel-Nawaz unatumia mauaji ya Peshawar ili kuondoa fahamu ya Jihad kutoka Pakistan, ili kuthibitisha vita hivi vya Marekani ni vita vyetu, kuwatangaza watu hao kama magaidi wanaopigana nchini Afghanistan dhidi ya majeshi vamizi ya Marekani, na kumuimarisha Raj wa Kiamerika nchini Pakistan. Kuanzia wakati wasaliti katika uongozi wa kisiasa na kijeshi walipoanza kubaini kwamba vita hivi vya Marekani ni vita vya Pakistan, ulinzi wetu nyeti na mitambo ya kiraia imekuwa shabaha ya mabomu na mashambulizi. Katika makala haya, Naveed Butt anathibitisha kwa ushahidi wa kina kwamba kwa hakika sababu kuu ya kuyumba kwa Pakistan na ukosefu wa usalama ni uwepo wa Marekani na C.I.A. na wahudumu wa BlackWater, wanaopanga milipuko na mashambulizi ya mabomu. Mashirika haya ya Marekani yameruhusiwa na wasaliti katika uongozi wa kisiasa na kijeshi kuzunguka kwa uhuru kote nchini ili kupeleleza, kupata makao, kupanga mashambulizi mabaya na kuajiri watu kutekeleza mashambulizi haya.

Makala haya yanaondoa mkanganyiko katika fikra za watu na kujibu kwa kuridhisha swali la je, vita hivi ni vya Marekani au ni vyetu? Yanafichua mipango ya Marekani dhidi ya Pakistan na vibaraka wa Marekani waliopo katika uongozi wa kisiasa na kijeshi. Makala haya yanaangazia kwa nini Marekani, baada ya kukamilisha kuikalia kimabavu Afghanistan, ilianza kudai hatua za kijeshi katika maeneo ya makabila ya Pakistan. Pia inapambana na kisingizio cha woga na kilemavu cha kipote cha watawala kwamba waliingia katika vita hivi vya Amerika kwa sababu bila ya usaidizi wa Amerika uchumi wetu hauwezi kuhimili na hatuwezi kuifukuza Amerika kutoka eneo hili. Yanamalizia kwa kutoa wito kwa Waislamu wa makabila na vikosi vya jeshi kuwafurusha wasaliti kutoka kwa safu zao na kuungana ili kuifurusha Amerika kutoka eneo hili, kazi ambayo sio ngumu, ikizingatiwa kuwa tayari wameshafanya hivyo kwa mithili ya USSR, dola kuu ya wakati wake.

Kumbuka: Naveed Butt aliandika makala haya kabla ya kutekwa nyara. Mnamo tarehe 11 Mei 2012, alitekwa nyara na mashirika ya serikali alipofika tu nyumbani na watoto wake kutoka shuleni kwao. Hadi leo, hajaachiliwa wala kufikishwa mbele ya mahakama yoyote. Kosa lake pekee ni kwamba alibeba kwa bidii mvutano wa kifikra na kisiasa dhidi ya Raj wa Kiamerika na kwa ajili ya kusimamisha Khilafah nchini Pakistan.

Makala haya yanaweza kutazamwa na kupakuliwa kutoka link hii: http://pk.tl/1i3z

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu