Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 20 Safar 1446 | Na: 1446 / 08 |
M. Jumapili, 25 Agosti 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Komesheni Kupigania Vyeo na Marupurupu katika Jeshi la Pakistan. Badala yake, Maafisa wa Jeshi Waislamu Lazima Watoe Nusrah kwa ajili ya Kusimamisha Khilafah Rashida
(Imetafsiriwa)
Katikati ya utakaso wa sasa na kuwekwa kando maafisa ambao wanampinga mkuu wa sasa wa jeshi la Pakistan, ilijiri kutajwa kwa Hizb ut Tahrir. Gazeti maarufu la Kiurdu la “Daily Jang,” liliripoti mnamo tarehe 13 Agosti 2024, katika toleo lake kwa jiji la jeshi la Rawalpindi kwamba, “(2011) Brigedia Ali Khan alifikishwa mahakama ya kijeshi kwa kuwa na uhusiano na shirika lenye itikadi kali la Hizb ut Tahrir. Pia alituhumiwa kwa kueneza uasi ndani ya Jeshi la Pakistan.”
Hizb ut Tahrir inasisitiza kwamba kupigania madaraka kwa utaratibu na mfumo wa sasa hakuna thamani yoyote kwa Waislamu. Haileti mabadiliko ya kweli. Kwa kweli, ni chanzo cha madhara. Katika miaka ya hivi karibuni, Jeshi la Pakistan, jeshi lenye nguvu zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu, limekuwa likikumbwa na upiganaji wa ndani kwa ndani katika vyeo vyake vya juu. Hata hivyo, kikundi chochote kitakachofanikiwa hatimaye, mshindi halisi ni bwana wa mfumo na utaratibu wa sasa, Marekani. Ni Marekani ndiyo inayoamua sera zote kuu ndani ya Pakistan, ikiwemo zile zinazohusiana na uchumi na jeshi. Marekani ndiyo inayotumia vibaraka wake katika uongozi wa jeshi kufanya kazi ya kuwa mlinzi na mdhamini wa mfumo huu fisadi.
Pakistan imeona mabadiliko ya vipodozi mara nyingi katika historia yake. Nyuso zinabadilika, lakini ukoloni wa kiharibifu unabaki. Kibaraka mmoja wa ukoloni anachukua nafasi ya mwengine. Kwa hivyo, Pakistan ni sawa na dola nyengine katika Ulimwengu wa Kiislamu, ambapo mabadiliko ya nyuso yanapangwa, ili kuhakikisha kuwa mfumo uliopo unabaki. Mapinduzi ya Kiarabu yalileta mifano mingi ya ukweli huu wa kusikitisha, kama ilivyo kwa mabadiliko ya hivi majuzi nchini Bangladesh, licha ya kujitolea mhanga na misimamo ya ushujaa ya Waislamu.
Kwa kweli, uongozi wa kisiasa na kijeshi nchini Pakistan, na makundi yao yote, wananyakua mamlaka ya watu. Hakuna uongozi unaotawala kwa mujibu wa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Hakuna ufikiaji utawala kupitia Ba’yah ya Kisheria ambayo Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na Waumini wameridhia. Hakuna kufikia uongozi kwa utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini. Hakuna usimamizi unaoongozwa na muongozo wa Uislamu, wenye kufuata hukmu za Shariah, hata kama kuna aliyehifadhi Quran miongoni mwa makundi yanayoshindana. Misimamo ya kisiasa na maamuzi ya kijeshi yanachukuliwa tu kwa manufaa ya kibinafsi. Hakuna kundi hata moja lililokuja kwa matakwa ya watu na uchaguzi wao huru na wa haki.
Uongozi wa kijeshi pamoja na wa kisiasa, na mirengo yao yote, hutegemea uwepo kwao kwa dola za kikoloni za Magharibi. Badali yake serikali za Magharibi zinawapa uhuru walafi hawa, kupora na kufuja watu, na kudhoofisha nchi. Huku wakifanya kazi hii chafu, wanapigania vyeo na maslahi ya mali, mithili ya mazimwi ya porini wanavyopigania mawindo. Lau kungekuwa na ikhlasi yoyote kwa Uislamu, au kujali nchi, katika kundi lolote lile, kundi hilo lingetoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir na mradi wake wa mabadiliko ya kweli, kupitia kusimamishwa tena kwa Khilafah Rashida.
Hizb ut Tahrir inatetea mabadiliko kupitia watu wenye nguvu, lakini kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume. Lengo la mabadiliko si vyeo na manufaa ndani ya dola za sasa zilizofeli, ambazo zinatawala kwa sheria zinazoamuliwa na akili finyo za wanadamu. Lengo la mabadiliko katika Uislamu ni kusimamisha hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ili kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikutana na watu wa vita, moto na chuma, na akataka kutoka kwao Nusrah kwa ajili ya Dini. Yeye (saw) alitafuta uwezo wa kimada wenye nguvu na utambuzi wa kina, akiuliza, «فَهَلْ عِنْدَ قَوْمِكَ مِنْ مَنَعَةٍ؟» “Je, watu wako wana nguvu?” Hivyo alikutana na makabila mengi yakiwemo; Banu Kalb, Banu Hanifah, Banu Amr bin Sa’asah, Banu Kinda na Banu Shaiban. Yeye (saw) aliendelea na mbinu hii kwa subira mpaka Mwenyezi Mungu (swt) alipofanikisha. Answari (ra) walitoa Nusrah, na Dola ya Kiislamu ya Madinah ikaanzishwa.
Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan!
Vibaraka wa Marekani katika uongozi wenu ni wale waliomuasi Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Hao ndio wanaofanya uhaini wa wazi, wakiwatelekeza Waislamu wa Kashmir na Gaza, huku wakichochea vita kati ya Waislamu. Vipi bado mnawatii? Imepokewa katika Ibn Majah na Ahmad kwa riwaya sahih kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «مَنْ أَمَرَكُمْ مِنْهُمْ بِمَعْصِيَةِ اللَّهِ فَلَا تُطِيعُوهُ» “Yeyote miongoni mwao atakayekuamrisheni kumuasi Mwenyezi Mungu msimtii.”
Tembeeni njia ya Answar (ra), watu wa vita ambao walitoa usaidizi wao wa kimada (Nusrah), ili kutawala kwa Uislamu kuanze. Walifanya biashara kwa nafsi zao na mali zao ili waingie Jannah. Ni Answari (ra) waliomuuliza Mtume (saw): “فَإِنّا نَأْخُذُهُ عَلَى مُصِيبَةِ الْأَمْوَالِ وَقَتْلِ الْأَشْرَافِ ْ نَحْنُ وَفّيْنَا” “Tunamchukua Mtume (saw) licha ya mitihani yote inayohusu maisha na mali zetu. na kuua waheshimiwa wetu. Basi tutapata nini, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ikiwa tutashikamana na ahadi zetu?” Ilikuwa kwa Answari (ra) kwamba Mtume (saw) aliwajibu kwa urahisi, «الْجَنّةُ» “Jannah.”
Ilikuwa ni Answar (ra) ambao walimpa Nusrah Mtume (saw) pindi aliposema, «أُبَايِعُكُمْ عَلَى أَنْ تَمْنَعُونِي مِمّا تَمْنَعُونَ مِنْهُ نِسَاءَكُمْ وَأَبْنَاءَكُمْ» “Naomba bay’ah yenu kwamba mtanilinda kama mnavyowalinda wake zenu na watoto wenu.” Basi mnangoja nini, enyi Wana wa Muhammad bin Qasim? Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir sasa, ili tupate kuhukumiwa tena kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt).
Afisi wa Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |