Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  28 Rabi' I 1446 Na: 1446 / 10
M.  Jumanne, 01 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

India Inafanya Kazi Kutishia Ugavi Wetu wa Maji, Huku Watawala wa Pakistan Wakifanya Kazi Kusawazisha Mahusiano na Mchokozi

(Imetafsiriwa)

Licha ya kupita siku nyingi, watawala wa Pakistan bado hawajajibu ipasavyo hatua hatari ya India kuhusiana na Mkataba wa Maji wa Indus (IWT), makubaliano ya kugawanya maji yaliyosimamiwa na Benki ya Dunia mnamo 1960. Mnamo 18 Septemba 2024, India ilituma notisi rasmi kwa Pakistan, ikitaja masuala mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya idadi ya watu, changamoto za kimazingira, na mambo mengine, ikiomba kutathminiwa upya kwa mkataba huo. India imeripotiwa kutuma barua nne tangu Januari 2023, ikitaka uhakiki.

Hii si mara ya kwanza kwa uongozi wa India kuzalisha mzozo na Pakistan kuhusu maji. Mnamo tarehe 1 Aprili, 1948, India ilizuia mtiririko wa maji kwenye mikondo muhimu katika Mstari wa Radcliffe. Mara kwa mara, India inatishia usambazaji wa maji wa Pakistan. Kando na uadui dhidi ya Pakistan, uchokozi wa maji wa India dhidi ya Waislamu wa Bangladesh unajulikana vyema. Mnamo Agosti 2024, India ilizindua uchokozi wa maji ambao haujawahi kutokea dhidi ya Bangladesh ili kuunda shinikizo la kisiasa. India ilifungua ghafla milango ya Bwawa la Dumboor bila onyo, na kusababisha mafuriko na kupoteza maisha.

Mtetezi wa kikanda wa Amerika, India, inalenga kudhoofisha nguvu za jeshi lenye nguvu zaidi la Umma wa Kiislamu, Pakistan. Mipango hii ya India inafurahia uungwaji mkono kamili wa Marekani kwani Washington inataka kukomesha vizuizi vyovyote kwa utawala wa India huko Asia Kusini. India kwa udanganyifu inaiomba Pakistan kujadili upya Mkataba wa Maji wa Indus (IWT) kwa kuibua visingizio hafifu, ilhali ni ndani ya uwanja wa uwezekano wa kisiasa ambapo India inalenga ama kujiondoa kwenye mkataba huo, au kuufanya ufungwe na usifanye kazi. Kwa njia hii, India itaendelea kujenga mabwawa, na miundombinu mingine, juu ya mito ili kutishia usambazaji wa maji na usalama wa chakula wa Pakistan.

Kugawanywa kwa Bara Dogo la India mnamo 1947, ambako kulisimamiwa na wakoloni, kulisababisha kazi kuu za mtandao mpana wa mikondo ya maji kuwekwa nchini India. Hii ilisababisha India kuwa sehemu ya juu ya mto, na Pakistan sehemu ya chini ya mto, katika bonde la Indus. Aidha, Benki ya Dunia iliipa India utawala zaidi kupitia Mkataba wa Maji wa Indus (IWT). Sio tu kwamba India ilipewa udhibiti wa mito mitatu ya mashariki, Ravi, Sutlej, na Beas, mkataba huo pia uliipa India haki ya kujenga miradi ya umeme wa maji juu ya mito mitatu ya magharibi iliyo chini ya udhibiti wa Pakistan, Jhelum, Chenab na Indus, ambayo yote hutiririka kupitia Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Baada ya kuisalimisha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu kwa India mnamo Agosti 2019, watawala sasa wanashughulika mno na mazungumzo na India, chini ya usimamizi na uelekezi wa Amerika.

Enyi Maafisa Wanyoofu katika Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Maji kwa nchi ni kama damu kwa mwili. Hata hivyo, watawala wa Pakistan wanashikilia kisu shingoni mwa Pakistan kwa niaba ya India na Amerika. Amerika imeamua kuipunguza Pakistan hadi mithili ya Bhutan na Nepal ili ijisalimishe kwa India. Mkakati ni ule ule ambao Washington imeuweka Mashariki ya Kati, ambapo imeliacha huru umbile la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wanaopinga. Kwa kudhibiti usambazaji wa maji, Mabaniani wanaowachukia Uislamu wanaweza kutishia idadi yetu inayoongezeka. Hata hivyo, meza zinaweza kugeuzwa kwa matendo yenu madhubuti ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah itaizuia India kutumia maji kama silaha dhidi ya Waislamu. Khilafah itakataa uingiliaji wote wa wakoloni katika usalama wa Waislamu. Itakata mafungamano na taasisi za kikoloni kama vile Benki ya Dunia. Khilafah badala yake itaunganisha Ummah na majeshi yake ili kuikomboa Kashmir Inayokaliwa kwa mabavu, na kuregesha udhibiti kamili juu ya mito mitatu ya Magharibi.

Enyi Maafisa Wanyoofu katika Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Raja Dahir wa leo, Modi, anapigana na Uislamu na Waislamu kwa njia zote. Ama watawala wenu wanatembea kwenye njia ya khiyana ya Mir Sadiq na Mir Jaafar. Wanamsahilishia adui na kuwadhuru Waislamu. Ama nyinyi, enyi Wana wa Muhammad bin Qasim, Dini yenu inakuwajibisheni kutembea kwenye njia tukufu ya Answaar, waliotoa Nusrah kwa ajili ya kusimamisha mamlaka inayotawala kwa Uislamu. Tembeeni katika njia ya Answaar na mkuu wao Saad bin Muadh, Mwenyezi Mungu awe radhi naye. Arshi ya Mwingi wa Rehema ilitikisika wakati wa kifo cha Saad bin Mu’adh, kutokana na Nusrah yake kwa Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) na dori yake katika kusimamisha dola Yake, ambayo ni heshima kubwa na kheri nyingi. Imepokewa na al-Bukhari kwamba Jabir kasimulia kwamba Mtume (saw) amesema:

«اهْتَزَّ عَرْشُ الرَّحْمَنِ لِمَوْتِ سَعْدِ بْنِ مُعَاذٍ»

“Arshi ya Ar-Rahmaan (Mwenyezi Mungu) ilitetemeka kwa kifo cha Sa'd bin Mu’adh.” Yote haya yalitokana na Nusra ya Saad kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Jihad yake katika Njia ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Hivyo, Hizb ut Tahrir inakuombeni mutoe Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, basi itikieni!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu