Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  26 Rabi' I 1446 Na: HTS 1446 / 10
M.  Jumapili, 29 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakika tutaridhika na Ushindi wa Kweli Siku ya Kusimamisha Khilafah!
(Imetafsiriwa)

Sherehe zilienea katika miji mingi nchini Sudan jana, Jumamosi, 28/9/2024, mjini Shendi, Atbara, Port Sudan, na kwengineko. Sherehe hizo hata zilivuka mipaka ya Sudan hadi Misri kwa furaha kwa ushindi wa jeshi na kuingia kwake katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Al Jaili kaskazini mwa Khartoum, ingawa habari hiyo haijathibitishwa hadi taarifa hii kwa vyombo vya habari ilipoandikwa.

Furaha hii ya watu inathibitisha ukweli kadhaa ambao lazima uzingatiwe:

Ukweli wa kwanza: Watu wa Sudan wamechanganyikiwa na kukosa matumaini kutokana na vita hivi vilivyolaaniwa hivi kwamba wanasherehekea ushindi hata wa kivipande.

Ukweli wa pili: Jeshi lingeweza kumaliza Vikosi vya Msaada wa Haraka tangu kuzuka kwa vita mnamo Aprili mwaka jana, kama halingefungwa na visingizio duni, kama uhusiano wa uongozi na Amerika, ambayo inataka vita kuendelea ili kuondoa ushawishi wa Uingereza na Ulaya nchini Sudan, ndiyo sababu ya kweli kwa nini vita hivi vinaendelea kwa muda wote huu.

Ukweli wa tatu: Watu wa Sudan wanatamani ushindi kwa sababu wao ni sehemu ya umma wa Kiislamu ambao haujui kushindwa, lau si watawala duni ambao wameuza dini yao kwa manufaa ya wengine na wakakubali utumwa kwa Wakoloni makafiri wa Magharibi, wakitekeleza njama zake dhidi ya Ummah na kutozingatia uaminifu au ahadi yoyote kwa watu wao.

Kinachopaswa kuwa wazi kwa watu wetu wa Sudan ni kwamba hali tunayoishi ndani yake tangu kuingia kwa mkoloni kafiri wa Kiingereza nchini mwetu hadi leo ni kwamba tumebadilisha kilicho bora zaidi kwa kilicho kibaya zaidi. Tumeacha Quran, Sunnah za Mtume wetu (saw) na Sunnah za Makhalifa waongofu, ambazo Mtume (saw) amesema:

«فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وسُنَّةِ الخُلَفاءِ الرَّاشِدينَ المَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عليها بالنَّواجِذِ»

“Basi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waongofu, na shikamaneni nazo kwa uthabiti” (Imepokewa na Al-Tirmidhiy, Ahmad, na Abu Dawud). Tumeuacha mwongozo wetu nyuma yetu na kuchukua mifumo ya makafiri wa Magharibi, kama vile demokrasia ya kiraia na kijeshi, na tawala zengine zilizobuniwa na mwanadamu ambazo hazitokani na Uislamu. Tumezitabanni kwa miongo kadhaa, na zimetuongoza kwenye udhalilifu na uduni huu.

Ushindi wa kweli unaostahiki furaha utakuwa siku tutakapokombolewa kutoka kwa mkoloni kafiri Magharibi, kutoka kwa utawala na udhibiti wao, kutoka katika kile kinachoitwa “sheria ya kimataifa”, na tusimamishe utawala wa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Tala’ duniani; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hapo ndipo tuna haki ya kufurahi. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[قُلْ بِفَضْلِ اللهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ]

“Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.” [Yunus: 58].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu