Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  15 Jumada I 1446 Na: HTS 1446 / 22
M.  Jumapili, 17 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uundaji wa Wanamgambo na Vikundi vyenye Silaha: Hatari Kubwa na Chombo cha Amerika cha Kugawanya Sudan
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumamosi, Novemba 16, 2024, kundi lenye silaha linalojiita Harakati ya Ukombozi ya Al-Jazirah lilitangaza nia yake ya “kulikomboa Jimbo la Al-Jazirah.” Pia lilionyesha uungaji mkono wake kwa vikosi vya jeshi. Katika video iliyosambazwa na vyombo vya habari na baadhi ya wanahabari wanaounga mkono jeshi, kundi hilo liliwataka watu wa Al-Jazirah kukusanyika karibu nalo na kukumbatia malengo yake.

Kama kawaida, uongozi wa jeshi ulilifumbia macho na kujizuia kutoa maoni! Hapo awali, mnamo tarehe 29 Oktoba, kundi linalojiita Batalioni la Mashariki, kundi la kijeshi lenye mfungamano na lile liitwalo Harakati ya Watu ya Ukombozi na Haki, mojawapo ya vuguvugu lililotia saini Mkataba wa Juba mwaka 2020, lilitangaza kupeleka vikosi vyake katika Jimbo la Kassala lililoko mashariki mwa Sudan. Kulingana na gazeti la ‘Sudan Tribune’, Msaidizi wa Kamanda Mkuu wa vikosi hivi alisema, “Hatua hii ilichukuliwa baada ya mashauriano ya kiufundi na kijeshi na vikosi vya jeshi, na vikosi vyetu sasa ni sehemu ya vikosi vya jeshi.”

Hapo awali, mtu mmoja aitwaye Keikil alijiondoa kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka na kutangaza utiifu kwa jeshi lakini aliendelea kufanya kazi chini ya bendera ya wanamgambo wanaoitwa Vikosi vya Ngao ya Sudan.

Kutokana na ufahamu wa kimsingi wa kisiasa, kijeshi na kiusalama, ni dhahiri kwamba kuenea kwa majeshi na makundi yenye silaha ni chombo cha kikoloni kinacholenga kusambaratisha mataifa na kuhujumu usalama wao kwa kuchochea mizozo ya kikabila na kikanda. Ushahidi wa wazi zaidi wa hili ni kujitenga kwa Sudan Kusini na maandalizi ya majimbo mengine ya Sudan kwa matokeo sawa na hayo. Hii ni sehemu ya mpango wa Marekani uliokubaliwa na Rais aliyeondolewa madarakani Omar al-Bashir, ambaye alisema katika mahojiano ya mwaka 2017 na Sputnik kwamba “kujitenga kwa Kusini kulitokana na shinikizo na njama za Marekani, na Amerika inajitahidi kuigawanya Sudan katika nchi tano.” Mpango huu unawiana na kile kinachoitwa Sykes-Picot Mpya, ambacho kinalenga kugawanya zaidi ardhi za Waislamu ambazo tayari zimegawanyika, mpango unaojulikana kama mradi wa Mipaka ya Damu wa Bernard Lewis.

Kwa nini, basi, watiifu ndani ya jeshi wanakubali kuwepo kwa vikosi vyengine chini ya bendera tofauti? Kwa nini vikosi hivi havijaunganishwa chini ya amri na udhibiti wa jeshi? Je, uongozi wa kijeshi haujajifunza kutokana na mateso waliyovumilia watu wa Sudan kutokana na kuundwa kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka kama chombo tofauti na uongozi huru kutoka kwa majeshi?

Umoja wa vikosi vya jeshi ni sawa na umoja wa Ummah na chombo chake. Hili pia linalazimu umoja wa uongozi wake, jambo ambalo halipaswi kulegezwa. Uislamu unahimiza umoja na unakataza mifarakano, kama Mtume (saw) alivyosema:

«إذا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ، فاقْتُلُوا الآخِرَ منهما»

“Pindi Wanapopewa ahadi ya utiifu (bay’ah) makhalifa wawili muueni wa pili wao.” [Muslim].

Ibara ya 66 ya Rasimu ya Katiba ya Khilafah inasema: “Jeshi lote litaunganishwa katika kikosi kimoja, kitakachowekwa katika kambi maalum. Baadhi ya kambi hizi lazima ziwe katika majimbo mbalimbali, nyingine katika maeneo ya kistratejia, huku baadhi ya kambi hizo zikipaswa kuwa kambi zinazohamishika zenye uhamaji wa kudumu, zikifanya kazi kama vikosi vya mashambulizi, kambi hizi zitapangwa katika vikundi vingi, kila moja ikijulikana kama jeshi, vikipewa nambari ipasavyo, kwa mfano, Jeshi la Kwanza au Jeshi la Tatu, au vikipewa jina la jimbo au wilaya.”

Kinachotokea leo, ni kutekelezwa kwa awamu ya pili ya mpango wa jinai wa Marekani wa kuisambaratisha Sudan, kufuatia kujitenga kwa Kusini kutokana na usaliti wa watawala na uzembe wa taasisi zinazohusika na kuhifadhi nchi hii.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tunawatahadharisha watawala dhidi ya kufuata njama hii na tunathibitisha kwamba matokeo ya jinai hii mbaya yataleta fedheha na aibu duniani na adhabu kali kesho Akhera. Pia tunatoa wito kwa wanajeshi wanyoofu kutoa nusra kwa Hizb utTahrir, kiongozi mwaminifu asiyewadanganya watu wake, ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hii itatabikisha hukmu ya Mwenyezi Mungu, itatekeleza Sharia yake, itaunganisha Ummah, na kuwang’oa wakoloni wanaolenga kudhibiti rasilimali zetu na kunyonya mali zetu. Mtume (saw) amesema: «مَن مَاتَ وَليسَ في عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “na atakaye kufa bila ya kuapa kiapo cha utiifu (bay’ah) shingoni mwake atakufa kifo cha kijahiliya.” [Muslim].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu