Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 16 Jumada I 1446 | Na: HTS 1446 / 23 |
M. Jumatatu, 18 Novemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan Yafanya Maingiliano na Waislamu kwa Kuwahutubia katika Soko Kuu la Port Sudan
(Imetafsiriwa)
Katika umati mkubwa wa watu wakarimu waliohudhuria, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa kaskazini mwa Msikiti wa Ibn Masoud katika Soko Kuu la Port Sudan mnamo Jumatatu tarehe 11/18/2024 M, yenye kichwa: “Uislamu ni mfumo kamili wa maisha”.
Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alizungumza na kueleza kuwa Uislamu umekuja ukiwa kama mfumo mpana wa kushughulikia matatizo ya maisha yote na kusimamia masuala ya watu katika nyanja zote za maisha ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na mengineyo, akinukuu dalili anuwai kutoka nususi za Qur’an na Sunnah. Alisema kuwa kadhia ya Umma leo inawakilishwa katika nukta mbili muhimu:
Ya kwanza: kusimamisha hukmu ya sheria ya Kiislamu kupitia kusimamisha mfumo wa Khilafah kwa njia ya Utume.
Ya pili: kuubeba Uislamu duniani ili kuitoa kwenye giza na kuipeleka kwenye nuru.
Abu Ayman alielezea hatari ya madai ya kidemokrasia na ya kisekula na kile kinachoitwa serikali ya kiraia au ya kijeshi, na akasisitiza kwamba yote ni miradi ya mkoloni.
Abu Ayman aliwauliza waliohudhuria kwa nini leo Umma hautekelezi hukmu za Mola wake Mlezi? Kwa nini mjumbe wa Marekani anakuja kushughulikia matatizo yetu?! Je, Uislamu sio mfumo kamili kwa maisha yote? Waliohudhuria walijibu kwa kusema “Allahu Akbar.”
Mwishoni mwa hotuba hiyo, alitoa bishara njema kwa Umma ya ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kusimamisha Khilafah, kuipa nguvu dini na kuibadilisha ya hofu kwa usalama, na akawataka waliohudhuria washirikiane na Hizb ut Tahrir ili kutimiza ahadi hii.
Kisha kukawa na kipindi cha maingiliano ambapo idadi ya waliohudhuria walishiriki kwa maswali na maoni, na Abu Ayman akawajibu. Hotuba ilimalizika kwa wasikilizaji kupiga takbira, kulia, na kukumbatiana kwa wema na upendo, wakiunga mkono mazungumzo yaliyofanyika.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/4365.html#sigProIdb8f7ba25c7
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |