Jumamosi, 28 Rajab 1447 | 2026/01/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  21 Rajab 1447 Na: HTS 1447 / 78
M.  Jumamosi, 10 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yafanya Visimamo Kadhaa katika Miji Tofauti Tofauti kote nchini Sudan

(Imetafsiriwa)

Ndani ya muundo wa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah mnamo Rajab 1342 H, na kama ukumbusho kwa Ummah wa tukio hili chungu, si kwa lengo la kulia juu ya historia tukufu iliyopotea, bali ili kuchochea azma ili Ummah uweze kutimiza wajibu wake wa kusimamisha Khilafah ili kuishi chini ya sheria za Mola wa Mlezi Walimwengu na kuondoa dhambi ya kifo cha Jahiliyyah kutoka shingoni mwake, Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan walifanya matembezi kadhaa katika miji tofauti kote Sudan, kufuatia swala ya Ijumaa mnamo 20 Rajab 1447 H, sawia na 9 Januari 2026 M, kama ifuatavyo:

Port Sudan, mji mkuu wa utawala, mbele ya Msikiti wa Dhu al-Nurayn katika kitongoji cha Transit, ambapo ilihutubiwa na Ustadh Ya'qub Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.

Mji wa Rabak katika Jimbo la White Nile, mbele ya Msikiti wa Al-Taqwa.

Mji wa Al-‘Abbasiyyah Taqali katika Jimbo la Kordofan Kusini, mbele ya Msikiti wa Al-Fuwailah katika kitongoji cha soko.

Mji wa Al-Obeid, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kaskazini, mbele ya Msikiti wa Soko la Ibn Mas’ud, ambapo ilihutubiwa na Ustadh Muhammad Quni Muhammad, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.

Khartoum Kaskazini (Bahri), mbele ya Msikiti wa Quba’ huko Al-Darushab.

Mji wa Omdurman, mbele ya Msikiti Mkuu katika Soko la Sabreen, ambapo ilihutubiwa na Ustadh Ahmad Abkar, wakili, mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan.

Mji la Al-Qadarif, mji mkuu wa Jimbo la Al-Qadarif, kando ya Msikiti wa Abdul Qadir Abdul Muhsin (Reli) katika soko kuu.

Mashababu walikuwa wamebeba mabango yaliyoelezea tukio hilo na kufafanua umuhimu wa kuishi chini ya kivuli cha Khilafah. Wahudhuriaji walifanya maingiliano na visimamo hivi kwa njia ambayo inathibitisha hamu ya Ummah ya kurudi kwa Khilafah, ambayo kupitia hiyo kuna heshima yake na radhi ya Mola wake Mlezi.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu