Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 22 Rajab 1447 | Na: HTS 1447 / 79 |
| M. Jumapili, 11 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Kuvunjwa Khilafah katika Hoteli ya Al-Busayri Plaza
(Imetafsiriwa)
Kwa mnasaba wa tukio la kupita miaka 105 ya hijriya tangu kuvunjwa kwa Dola ya Waislamu, Khilafah mnamo 28 Rajab 1342 H, na kama mwendelezo wa kuwakumbusha Waislamu faradhi ya kufanya kazi ya kuiregesha kama Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan yatoa heshima kukualikeni kuhudhuria kongamano lenye kichwa:
“Sudan Kati ya Sera ya Mipaka ya Damu na Sera ya Kuwaunda Watu Kuwa Ummah Mmoja”
Kongamano litaanza kwa kusikiliza hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kwa mnasaba wa kupita miaka 105 tangu kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah.
Baada ya hapo, kundi la wabebaji da’wah watajadili, wakati wa kongamano, nyaraka kadhaa muhimu zinazozungumzia masuala kadhaa muhimu.
Wakati: Jumamosi, 28 Rajab 1447 H, sambamba na 17 Januari 2026 M, saa 12:30 adhuhuri, Mwenyezi Mungu akipenda.
Mahali: Port Sudan, Ukumbi wa Mikutano katika Hoteli ya Al-Busayri Plaza, katika Soko Kuu.
Kuhudhuria kwenu ni furaha kwetu na uwepo wenu ni heshima kwetu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



