Kundi la Tahrir Al-Sham Limemteka Nyara Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria Nasser Sheikh Abdul Hai
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Alhamisi, tarehe 1/9/2022, Vikosi vya Usalama vya Hay'at Tahrir Al-Sham vilimteka nyara mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Syria, Ustadh Nasser Sheikh Abdul Hai, mbele ya nyumba yake katika mjini wa Atarib; hii ilikuwa ni baada ya kauli zake dhidi ya wito wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, anayeutaka upinzani, kufanya maridhiano na dhalimu wa Al-Sham, na msimamo wa serikali ya Uturuki kuhusu utawala wa Bashar Al-Assad.