Afisi ya Habari
Tanzania
H. 22 Dhu al-Qi'dah 1441 | Na: 1441 / 03 |
M. Jumatatu, 13 Julai 2020 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
TUNASIMAMA IMARA NA FAMILIA ZA MAHABUSU
Kufuatia mkutano wa waandishi habari wa wawakilishi wa familia tatu za mahabusu: Omar Salum Bumbo, Ramadhan Moshi Kakoso, na Waziri Suleiman Mkaliaganda mnamo 09 Julai 2020 huko Magomeni Makuti, Dar es Salaam, Tanzania ili kuelezea huzuni na uchungu wao juu ya jamaa zao watatu ambao wanazuiliwa pasi na mashtaka kwa takriban miaka mitatu, sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania tunasimama imara kwa mshikamano na familia hizi (za mahabusu) ambao ni wanachama wa Hizb ut Tahrir / Tanzania ili kudai haki kwao.
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania kwa mara nyengine tena tunavitaka vyombo vyote vinavyo husika na utoaji haki nchini Tanzania kuzingatia mchakato sahihi wa mahakama kwa kufikisha ushahidi mahakamani tayari kwa mashtaka ya mahabusu, endapo watakuwa na ushahidi wowote, waachilieni mahabusu hao watatu kwa dhamana, au waachilieni huru mara moja.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Alama Ishara
#StopOppressiveLawsAndAbduction (English)
#KomeshaUkandamizajiWaKisheriaNaUtekaji (Swahili)
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/tanzania/942.html#sigProId13bea5e8d1
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |