Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  4 Rabi' II 1442 Na: 1442/18
M.  Alhamisi, 19 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuzuia Swala za Ijumaa ni Uhalifu Usiosameheka

(Imetafsiriwa)

Chini ya shinikizo la kampeni iliyoendeshwa na raia wema wa Tunisia dhidi ya hatua za kufunga misikiti, Wizara ya Maswala ya Kidini ilitangaza uamuzi wa kufungua misikiti Jumatatu, Novemba 23, kutekeleza swala tano za kila siku isipokuwa swala ya Ijumaa.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia, tunathamini sana juhudi iliyofanywa na watu wa al-Khadra katika njia ya dini yao na hadhi ya misikiti yao, kwa hivyo tunawaalika wapaze sauti yao juu ya sauti yetu ili kuhakikisha kwamba misikiti inatimiza umuhimu wake kamili, ambao kilele chake ni (swala za) Ijumaa na jamaa, pamoja na kuchukua hatua za kuzuia maambukizi ya janga la Korona.

Kama ambavyo tunatangaza kuendelea kwetu katika kampeni:

#فاسعوا_لذكر_الله

#بالاسلام_نحيا_وتحيا_مساجدنا

 #NendeniMkamtajeMwenyeziMungu

#KwaUislamuTunahuikaNaMisikitiInahuika

Na tunawaalika watu wetu nchini Tunisia kushiriki nasi katika kampeni hii ili kupata ujira na thawabu. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُون﴿.

"Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa." [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu