Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  16 Jumada I 1446 Na: 1446/08
M.  Jumatatu, 18 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ni Rasmi: Mamlaka nchini Tunisia Zinasaidia Amerika na Umbile la Kiyahudi katika Mauaji ya Halaiki dhidi ya Watu Wetu huko Gaza na Palestina yote
(Imetafsiriwa)

Mji wa Vicenza wa Italia ulishuhudia hafla ya kusainiwa kwa itifaki ya mwisho ya taratibu za kupanga mazoezi ya kijeshi ya Simba wa Afrika 2025 nchini Tunisia. Makubaliano hayo yalitiwa saini kati ya Kanali Mwandamizi wa Tunisia Mguidich Mejid na Kanali wa Marekani Drew Conover, Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jopo Kazi la Jeshi la Marekani la Kusini mwa Ulaya.

Ni muhimu kutaja kuwa mazoezi ya Simba wa Afrika ndiyo oparesheni kubwa zaidi za pamoja za mafunzo zinazosimamiwa na vikosi vya Marekani barani Afrika. Wakati huu, yataandaliwa na Tunisia, Morocco, Senegal, na Ghana, na kushirikisha wanajeshi 7,500 kutoka nchi 28.

Kuhusu umuhimu na malengo ya mazoezi haya, Meja wa Marekani Jay Jackson, mpangaji mkuu wa mazoezi hayo, alisema: “Kupanga pamoja na washirika wetu wa Tunisia kumekuwa muhimu sana katika kuhakikisha kwamba Simba wa Afrika inaimarisha utayari wetu wa pamoja na usalama wa kikanda... Kupitia mazoezi kama haya, tunaweza kuboresha mikakati yetu ya uendeshaji na uimarishaji ushirikiano ambao ni muhimu kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vinavyojitokeza kote Afrika Kaskazini.”

Lengo lililotajwa la mazoezi haya, kwa mujibu wa Meja Jackson, ni “hatimaye kuunda kikosi chenye nguvu zaidi cha kimataifa,” akimaanisha kwamba Amerika inataka kulinda eneo la magharibi la ulimwengu wa Kiislamu kwa kudumisha udhibiti wa majeshi yake ili kulinda maslahi yake na kulinda Upande wa umbile la Kiyahudi linapoendelea na mauaji na uharibifu wake, kuyaelekeza majeshi ya eneo hili kutenda kulingana na maagizo yake.

Hili ndilo lengo la sasa la Marekani: kudhibiti majeshi ya Waislamu katika Afrika Kaskazini na uongozi wao.

Hili linathibitisha kwamba:

Mazoezi ya kijeshi ya Marekani, “Simba wa Afrika,” yameundwa ili kupenya jiografia ya magharibi ya nchi za Kiislamu na pwani yake ya jangwa. Haya ni mazoezi ya kivitendo ya uwanjani yanayolenga kuwapa wanajeshi wa kikoloni wa Kimarekani uzoefu wa ardhi hiyo.

Jambo linalokera zaidi na la kulaumiwa zaidi ni kuiwezesha Marekani kujipenyeza katika majeshi ya mataifa ya Waislamu, kuelekeza upya uaminifu wa maafisa wao, na kuwatumia katika kutumikia mipango ya kikoloni ya Marekani!

Baya zaidi ya yote, Marekani mhalifu, muuaji—ndege zake, droni, makombora, na mabomu—ndizo silaha zilezile zinazotumiwa kutuangamiza!

Wakati huo huo kanali wa Tunisia, chini ya amri za “Mkuu wa Majeshi,” alipokuwa akitia saini makubaliano na kanali wa Marekani, viongozi wa kijeshi wa Marekani walikuwa upande mwingine wakisimamia kuangamizwa kwa watu wetu huko Gaza na kote Palestina, na kuiangamiza Lebanon kupitia magenge ya Kiyahudi wanayoyafadhili kwa silaha na pesa. Ikiwa tutazingatia kwamba mazoezi haya yatafanyika baada ya Donald Trump kuchukua wadhifa na chini ya uongozi wa Waziri mpya wa Ulinzi, Pete Hegseth – mpiganaji wa kimsalaba aliyetangazwa ambaye amechorwa nembo ya Wanajeshi wa Msalaba (Msalaba wa Jerusalem) kifuani mwake, sambamba na maneno “Mungu akipenda,” kauli mbiu iliyotumiwa na Wanajeshi wa Msalaba wakati wa uvamizi wao wa Jerusalem katika zama za Khilafah ya Kiislamu—inadhihirika kwamba wanajeshi na maafisa wameburutwa bila kujua katika vita vya msalaba vya Marekani dhidi ya Jerusalem na kwa upana nchi za Waislamu.

Enyi Waislamu katika Ardhi ya Zeituna, Enyi Maafisa, Enyi Wanajeshi, Enyi Vizazi vya Mujahidina Mashujaa:

Kushiriki katika mazoezi hayo ya kijeshi ni kuhusika moja kwa moja katika kuwaangamiza Waislamu nchini Palestina na Lebanon. Yanawezesha udhibiti wa kafiri Kruseda juu ya ardhi za Uislamu. Je, mutakaa kimya kuhusu viongozi bandia wanaokabidhi majeshi yenu kwa adui yenu katika kipindi cha vita?!

Mnawezaje kukubali majeshi yenu kuwekwa chini ya udhibiti wa adui yenu na uongozi wake? Mnawezaje kuvumilia kutumiwa vibaya ili kuitumikia Amerika ya kikoloni katika kuzikalia kimabavu ardhi zenu, kuua watu wenu, kupora mali yenu, na kisha kupora Afrika na kuwakandamiza watu wake waliokandamizwa, waliotiishwa - kulinda mfumo wake wa dhalimu wa ulimwengu, kutetea utaratibu wake dhalimu wa kikoloni, na vibaraka wake? أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿ “Basi je, hamzingatii?” [Al-Baqara:44]. 

Heshima iko wapi? Utu uko wapi? Uanaume uko wapi? Watoto wetu na wanawake mjini Gaza wanakulilieni msaada wenu—je, mutajibu maombi yao kwa kumsaidia muuaji wao? Mna nini? Mnahukumu vipi?!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma'ida:51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu