Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 13 Sha'aban 1446 | Na: 1446/09 |
M. Jumatano, 12 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wakutana na Mkuu wa Harakati ya Wokovu wa Kitaifa
(Imetafsiriwa)
Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inakutana na Bw. Ahmed Najib Al-Shabi, mkuu wa Harakati ya Wokovu wa Kitaifa, jana, Jumanne 11/02/2025. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hizb kwenye makao makuu ya Sakra Ariana, na uliongozwa na Bwana Al-Arabi Karbaka, mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Bw. Al-Habib Hajji, Tamim Noura, Dkt. Faisal Darghouth, na Mhandisi Yasser Al-Anwar, wanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia. Hii ilikuwa ni kutokana na ziara ambayo ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano walikuwa wameifanya kwenye makao makuu ya Harakati ya Wokovu wa Kitaifa hapo awali.
Mkutano huo ulizingatia misingi ya kifikra ya hatua za kisiasa na machimbuko ya sheria katika mgongano wake baina ya Uislamu na fikra ya Kimagharibi. Ujumbe huo ulimweleza mgeni huyo mheshimiwa kwamba wokovu wa binadamu kutokana na dhulma ya urasilimali unaweza kupatikana tu kwa misingi ya Uislamu na masuluhisho yake adilifu.
Ni vyema kutaja mazingira ya kirafiki ambayo mkutano huu ulifanyika na makubaliano ya pamoja juu ya umuhimu wa kuendelea kwa mikutano hii ili kuunda ruwaza ya kina juu ya masuala yanayohusu rai jumla.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |