Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  10 Rabi' I 1443 Na: 03 / 1443
M.  Jumapili, 17 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Usiri ndani ya Nyumba ya Mwenyezi Mungu: Khiyana ya NTA na Kufichuka kwa Umma kwa Sera dhidi ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Makala katika NRC yaliyochapishwa Ijumaa iliyopita hayakuacha kutotambuliwa. Makala haya yalielezea jinsi kwa uchache manispaa 10, ikiwemo Rotterdam, Zoetermeer na Delft, zilivyofanya uchunguzi wa siri ndani ya misikiti katika miji yake. Manispaa hizi zilituma wachunguzi wa shirika la utoaji ushauri na utafiti "Nuance door Training en Advies" (NTA) kwa misikiti hiyo.

Kwanza kabisa, haishangazi kwamba mashirika ya serikali hukiuka sheria na kanuni kwa makusudi katika majaribio yao ya kuwakandamiza Waislamu au kufanya hali zao kuwa ngumu zaidi. Lakini, njia waliyoifanya ndio inayotia wasiwasi zaidi, ambayo ni, kutumia kampuni ya uchunguzi ya kibinafsi iliyoasisiwa na Waislamu. Umuhimu wa njia hii ulifupishwa katika makala ya NRC bali wa kufurahisha: "Kinyume na maafisa wa manispaa wafanyikazi wa NTA huenda nje, kwenye misikiti na wanafanikiwa kuingia". Mratibu wa ugaidi NCTV pia inazielekeza manispaa kwa sifa maalum za kampuni hii na ni nani anayepaswa kuhusika ikiwa kuna hitaji la habari kuhusiana na matukio yanaofanyika katika misikiti katika manispaa yao.

Sifa maalum ambazo NCTV inayokusudia ni uhusiano wa uaminifu walionao wafanyikazi wa NTA na bodi ya misikiti na wanaoizuru. Lakini, njia ambayo wafanyikazi hawa wameitumia bila aibu ili "kupata habari" inakiuka uaminifu ambao ndugu zao wanaoustahiki. Mtume (saw) alisema:

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يَخْذُلُهُ وَلَا يَحْقِرُهُ» Muislamu ni ndugu ya Muislamu mwengine. Hamdhulumu wala hamchukii. Katika kesi hii maalum shughuli ya mauzo ilifanywa kwa gharama ya ndugu na vile vile kumshawishi kwa kuwa walijifanya kuwa mtu ambaye siye. Wafanyakazi wa NTA wanapaswa kujua kwamba ukiukaji huu wa haki za ndugu zao utalazimika kuhesabiwa Siku ya Kiyama.

Kwa kuongezea, kesi hii inaonyesha ukiukaji wa kimuundo wa kanuni zao katika uundaji wa sera zao dhidi ya Uislamu. Tunaona unafiki huohuo linapokuja suala la ufadhili wa misikiti, uamuzi wa Mahakama ya Ulaya kuhusu marufuku ya hijab mahali pa kazi, marufuku ya vyama "vinavyopinga demokrasia", kumtukana Mtume (saw) na jinsi mashirika ya serikali wavuka mpaka wakati wa kesi ya Cornelius Haga Lyceum hii ni kutaja mifano michache tu.

Hizb ut Tahrir ameelekeza kwenye mizizi ya uovu huu, mara kwa mara na tena na hata kuiorodhesha kama "sera ya kupinga Uislamu" ambayo inasukumwa ili kuongeza shinikizo kwa Waislamu ili wabadilishe kanuni zao za kimsingi kwa "uhuru" wa kisekula.” Tuzani alizungumza katika makala ya zamani ya NRC mnamo 16 Februari 2019 kuhusu utiifu na kwamba ni "motisha / msukumo ambao mara nyingi hudharauliwa" na jinsi fahamu hii ya utiifu ilivyo muhimu katika juhudi dhidi ya "misimamo mikali". Tuzani anapaswa kutambua kuwa utiifu ni muhimu zaidi kwa ajili ya kudumisha uhusiano na Muumba (swt), kwamba utiifu huu umehifadhiwa kwa Uislamu na Waislamu na haupaswi kuuzwa kwa pesa nyingi za mfukoni.

Waislamu wanaoshiriki katika miradi hii ya mashirika ya serikali wanakiuka kanuni muhimu za uadilifu pamoja na kanuni za Uislamu. Tunatoa wito kwa Waislamu kuongeza ufahamu wao wa kisiasa na wasitoe jukwaa kwa watu ambao wanajua kuwa wanafanya kazi kwa uchangamfu ili kuutia makosani Uislamu.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [Surah al-Ma’ida: 51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu