Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  21 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 1443 / 13
M.  Jumatano, 20 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Astana Tatu, Ubwana wa Utawala wa Mauaji ndio Muhimu, Sio Usalama wa Watu wa Syria!
(Imetafsiriwa)

Hapo jana rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alifanya msururu wa mikutano na rais wa Iran Ebrahim Raisi na rais wa Urusi Vladimir Putin jijini Tehran ambako yuko katika ziara rasmi. Wakati wa mikutano hii, kulikuwa na majadiliano ya masuala ya ushirikiano wa kiuchumi, ukanda wa nafaka ambao ulifunguliwa kutokana na vita vya Ukraine na uwezekano wa operesheni ya kijeshi iliyopangwa dhidi ya kaskazini mwa Syria. Ndani ya wigo wa ziara hiyo, mikutano saba ya Astana ilifanyika, ambayo wa mwisho ulifanyika mnamo Julai 1, 2020. Katika taarifa ya pamoja yenye nukta 16 vya mkutano huo, ambao ulifanyika kwa ushiriki wa Rais Erdogan na Putin, kujitolea kwa pande zote kwa heshima ya eneo na ubwana wa Jamhuri ya Syria, azma yao ya kupambana na ugaidi na imani yao ya pamoja kuhusu uthabiti wa vikao vya Kamati ya Katiba yalisisitizwa. Uturuki, Urusi na Iran, pande zinazoshiriki katika mkutano huo wa kilele wa pande tatu, pia zilielezea imani yao kwamba mzozo wa Syria unaweza kumalizwa tu kupitia mchakato wa kisiasa ndani ya muafaka wa azimio nambari 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na sio kupitia suluhisho la kijeshi.

Operesheni hiyo ambayo imekuwa ikifanyika nchini Syria tangu mwaka wa 2011 ina pande mbili pekee; kwa upande mmoja, kuna Waislamu na watu waasi wa Syria ambao wanasimama upande wa haki. Kwa upande mwingine, kuna utawala dhalimu wa Syria, mchinjani Iran, Urusi inayokalia kwa mabavu, Uturuki inayotoa ushirikiano na nchi nyingine za eneo zinazosimama upande wa ukafiri, yaani upande wa Amerika. Kwa hivyo, kuna upande mmoja pekee katika mikutano ya Astana, sio pande tatu. Upande huu ni Kafiri Amerika. Wale wote walioketi kwenye meza ya Mkutano wa Saba wa Astana uliofanyika Tehran wanafanya kazi kuleta suluhu ya kisiasa ya Marekani nchini Syria. Hawajali kulinda maisha na mali ya watu wa Syria, bali ubwana wa utawala wa Assad, ambao unahusika na vifo vya raia zaidi ya milioni, na heshima ya eneo la Syria. Putin, aliyeketi mezani, ni mwakilishi wa Urusi, iliyoshusha kiburi chake na kujidhalilisha wakati wa vita vya Ukraine. Pia ni Putin, ambaye Erdogan anamwita rafiki yake, ndiye muuaji wa Waislamu walioangamia chini ya mashambulizi ya mabomu nchini Syria. Ama kuhusu uhalifu wa Iran, haukomei Syria pekee, bali Iran inajulikana na kila mtu kwa yale iliyoyafanya katika nchi za Afghanistan, Iraq, Yemen na Lebanon. Kwa sababu hii, ni jambo lisilokubalika kwa Erdogan kumtaja muuaji wa Wasyria, Qassem Soleimani, kama "shahidi shujaa" huku akimwangalia Raisi machoni na kumwita "ndugu yangu", na kuketi kwenye meza hiyo akiwakilisha Uturuki kwa sababu anajua vyema mauaji yaliyofanywa na Iran nchini Syria. Ama Uturuki, ambayo mwanzoni ilisema kuwa iliegemea upande wa watu wa Syria na wanamapinduzi, baada ya kupita muda ilianza kujikusanya kwa uwazi pambizoni mwa meza moja pamoja na wauaji wa Waislamu, na kuusukuma upinzani hadi Idlib kutokana na hatua ilizochukua, majadiliano na maamuzi yaliyochukuliwa, na ilikuwa mshipa wa uhai kwa utawala wa Assad, na kuuwezesha kutawala nchi kwa mara nyengine tena.

Mgogoro wa kiuchumi na kifedha unaoikumba Uturuki unaisukuma serikali kuanzisha uhusiano wa kirafiki sio tu na wauaji hawa, bali pia na wauaji wengine, haswa na umbile la ya Kiyahudi, ambapo ni matokeo ya aibu ya sera ya kigeni ya ubinafsi na isiyo ya kimfumo. Hivyo basi, haiwezekani kimantiki wala kisiasa wala kisheria kukubali mkutano wa Uturuki na watawala hao wauaji kwa sababu ya sera za kieneo za Amerika na malengo ya kiuchumi. Huku nchi zinazowakilishwa na watawala hao zikiwa na tabia ya chuki dhidi ya Uturuki mara kwa mara na wanaeleza hili kwa taarifa zao, vikwazo wanavyovitekeleza na sera zao mbaya. Sera hizi zenye malengo ya kimantiki zitasababisha matatizo makubwa kwa Waislamu nchini Uturuki hasa na kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla. Juu ya haya yote, kwa yakini huu utakuwa ni mzigo mzito wa madhambi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 [وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud:113]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu