Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  25 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 15
M.  Jumapili, 02 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Ziara ya Putin nchini Uzbekistan Yamaanisha Nini?
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 26/5/2024, kwa mwaliko wa Rais Shavkat Mirziyoyev, Rais wa Urusi Vladimir Putin alifanya ziara ya kiserikali nchini Uzbekistan. Hii ni ziara ya tatu ya kigeni ya Putin baada ya kuchaguliwa kuwa rais. Ziara zake za awali zilikuwa China na Belarus. Ziara hiyo ilijumuisha wajumbe wengi sana, karibu nusu ya serikali, kama Putin anavyosema. Matukio makuu ya ziara hiyo yalifanyika mnamo tarehe 27/5/2024. Kilichovutia vyombo vya habari wakati huu ni ukweli kwamba Mirziyoyev na Putin walifanya mazungumzo ya moja kwa moja nje ya muda uliopangwa wa ziara hiyo. Kwa mujibu wa habari, walifanya mazungumzo hadi saa tisa asubuhi. Mirziyoyev pia alimwalika Putin nyumbani kwake mwenyewe.

Inaweza kusemwa kuwa sababu ya ziara hii ni wasiwasi unaoongezeka wa utawala wa Putin kutokana na kuimarishwa hivi karibuni mahusiano ya Magharibi na Asia ya Kati, hasa Uzbekistan. Ukweli kwamba ziara ya kwanza ya Putin baada ya kuchaguliwa kwake ilikuwa Uzbekistan kati ya nchi za Asia ya Kati unaonyesha kuwa Uzbekistan ni muhimu sana kwa Urusi. Ukweli kwamba mazungumzo ya nchi mbili kati ya marais hao wawili yalizidi muda wao uliopangwa, na nia ya Mirziyoyev kumkaribisha Putin nyumbani kwake, inaonekana kuonyesha kuwa rais wa Uzbekistan bado ni mtiifu kwa Urusi. Huku Mirziyoyev akienda likizo siku moja kabla ya ziara ya David Cameron, na hakuweza kukutana naye. Ijapokuwa Putin alipokelewa kwa mapokezi makubwa na ingawa inasemekana kuwa ziara hiyo ilikuwa ya kihistoria na ilipata matokeo makubwa, hakuna uwezekano kwamba Putin hatahisi kusikitishwa sana na serikali inayoongozwa na Mirziyoyev kwa sababu ujenzi wa kinu cha nyuklia uliahirishwa na serikali ya Uzbekistan kwa miaka 6. Kwa hivyo, Putin ilibidi aje mwenyewe ili kurekebisha kandarasi ya hapo awali. Baada ya yote, ujenzi wa mtambo wa nyuklia, ambao utagharimu mabilioni ya dolari, ni muhimu sana kwa Warusi sio tu kwa kiwango cha kiuchumi, bali pia katika kiwango cha kisiasa. Walakini, wanaharakati wengi katika nchi yetu wanaelezea wasiwasi wao juu ya ujenzi wa kinu cha nyuklia, wakisema kuwa utaongeza utegemezi kwa Urusi. Kwa kuongezea, Uzbekistan bado si mwanachama wa Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO) na Muungano wa Forodha wa Eurasia unaotawaliwa na Urusi. Hivi majuzi, waenezaji propaganda wa Urusi walitoa taarifa mbalimbali za vitisho kuelekea Uzbekistan.

Kwa upande mwingine, Urusi iliahidi kutatua matatizo ya usafiri na usafirishaji ya Uzbekistan na kukidhi mahitaji yake ya nishati. Inashangaza hasa kwamba kipengele cha hatari zaidi cha Uzbekistan, ambacho kimekatwa na njia za maji, kinatatuliwa kupitia Ukanda wa Kimataifa wa Usafiri wa Kaskazini-Kusini. Hii ni pamoja na kuongezeka kwa usambazaji wa gesi na vilainishi katika sekta ya nishati. Makampuni ya Kirusi awali yalipata viwanja vikubwa vya gesi katika nchi yetu, kisha uzalishaji wa gesi na makampuni ya serikali ukapungua mwaka baada ya mwaka. Miaka miwili iliyopita, katika msimu wa vuli na baridi, serikali ya Uzbekistan ililazimishwa kutia saini makubaliano ya gesi na Urusi kutokana na mgogoro mbaya wa nishati. Sasa, cha kusikitisha, nchi yetu yenye utajiri wa gesi inaelekea kwenye utegemezi wa gesi ya Urusi. Uagizaji wa bidhaa za mafuta na petroli kutoka Urusi pia unaongezeka mwaka baada ya mwaka.

 Inafaa kuashiria pia kwamba chini ya kivuli cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali nchini Uzbekistan, nia ya kupiga vita Uislamu na Waislamu hivi karibuni imeongezeka. Kabla ya ziara ya Putin, huenda serikali ikachukua hatua mbalimbali dhidi ya Uislamu, na hili tayari limefanyika. Hili, bila shaka, linaashiria kwamba hili lilifanywa ili Mirziyoyev aweze kumjulisha Putin kwamba shughuli zinazolenga kuwatenganisha Waislamu na Uislamu zinaendelea kufanywa nchini Uzbekistan.

Ni wazi kwamba kila Muislamu ana wasiwasi na hatua ovu za Putin katika nchi yetu kwa sababu dola hii ya kikoloni ya kikafiri ya Urusi ni adui wa milele wa Waislamu wa Asia ya Kati na Uzbekistan. Mababu zao wa kikomunisti wapagani waliivamia nchi yetu, wakapora mali zetu, wakabaka wanawake wa Kiislamu, na kufanya mauaji ya kinyama. Kama vile wanavyojaribu kuwabandika Waislamu wanaoeneza ujumbe wa Uislamu kuwa ni magaidi na watu wenye msimamo mkali, babu zetu shupavu waliopigana dhidi ya uvamizi wa Warusi hapo awali walielezewa kuwa ni madhalimu wa Ummah wetu. Leo, kana kwamba hakuna kilichotokea, wanaingilia nchi yetu tena na wanafanya kama mabwana. Serikali ya Uzbekistan pia inashirikiana na maadui zetu bila kujifunza somo lolote kutoka kwa siku za nyuma.

Ili kuwafurahisha, inawakamata watu wetu wajasiri, na inapuuza ukweli kwamba raia wake wanashukumiwa kudhalilishwa na utegemezi katika ardhi ya serikali ya Urusi, hata kulazimishwa kwenda kwenye vita vya Ukraine, na kuchangia mali yetu kwao bure... Kuna kutoridhika sana miongoni mwa watu wetu kuhusiana na mambo haya. Walakini, serikali bado inafanya kazi chini ya udhibiti wa rais wa Urusi. Hii inathibitisha kwa mara nyingine tena kwamba maneno ya mara kwa mara ya Mirziyoyev kwamba ni lazima tuwafurahishe watu si lolote zaidi ya upuuzi.

Kuna jambo moja tu ambalo litawaokoa Waislamu wetu kutoka kwa utegemezi wa Urusi katika nyanja zote, ni pindi Uislamu unatakapotawala. Zaidi ya yote, ukweli kwamba jeshi na vikosi vya jeshi, ambavyo vinachukuliwa kuwa upande wenye nguvu wa Warusi, ni dhaifu sana kuliko wanavyodai wenyewe. Hii imekuwa wazi baada ya vita vya Ukraine. Mwishowe, je, huu si ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu huwasaidia waja wake Waislamu, kwa kutuonyesha udhaifu wa maadui zetu?! Je, hii sio kweli nusura ya Mwenyezi Mungu kwetu?! Hapana shaka kwamba haya yanajumuisha ishara kwa wale wanaotaka kujifunza kutoka kwayo! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَن يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]

“…Na wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa: 141].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu